• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Timu ya Brazil ambayo ni waandaaji wa kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2014-06-05 16:36:36
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zitakazocheza kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, tuliizungumzia timu ya taifa ya Aljeria au "Mbweha wa Jangwani" jinsi ilivyoweza kufuzu michezo ya safari hii na jinsi ilivyofanya vibaya katika michuano ya kombe la dunia iliyopita. Bila kusahau mechi mbalimbali ilizoshiriki katika michuano mbalimbali duniani. Na kwa ujumla wiki iliyopita tulikamilisha nchi zote tano zitakazoshiriki michuano hii mikubwa duniani labda kwa kuwakumbusha tu nchi hizo ni kama vile Cameroon, Cote dlivoire, Nigeria, Ghana na Aljeria. Na leo hii katika kipindi tutaizungumzia timu ya Brazil ambayo ni waandaaji wa michuano hii na kuona jinsi ilivyofanya katika michuano iliyopita ya kombe la dunia lakini kabla ya kuendelea mbele tumpishe

    Kwa vile Brazil wao ni waandaaji wa kombe la dunia safari hii, imelegezewa sheria kwenye michuano ya kufuzu ya Amerika Kusini. wakizingatia hilo na kuelewa matarajio makubwa waliyonayo wananchi wa Brazil juu ya kunyakua ubingwa wa kombe hili la mwaka huu, upangaji wa timu ya taifa ya Brazil umesababisha wasiwasi hususan mechi za kirafiki ilizocheza na timu za mbalimbali soka. Hata hivyo katika jaribio lao kubwa wakiwa njiani kuelekea kwenye michuano ya mwaka huu, Brazil ilishindwa ilitolewa katika michuano ya Copa Amerika ya mwaka 2011 katika hatua ya robo fainali na kutolewa na Paraguay.

    Kama tulivyosema awali Nchi ya Brazil ndio muandaaji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2014, timu yake ya taifa kwa mwaka huu inapewa nafasi ya kushinda kombe hili. Brazil ni maarufu kama "Samba Boys" kutokana na aina ya mchezo wake, na ndio timu pekee ambayo imeshiriki katika kila fainali za kombe la dunia toka lilipoanza. Yaani imeshiriki kombe hili mara 19. Timu hii ina historia ya kipekee kwa kuwa imeshalitwaa kombe hili mara tano, mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002. Mara mbili imeweza kumaliza ikiwa nafasi ya pili mwaka 1950 na 1998. na katika viwango vya FIFA ipo nafasi ya 4. Katika kombe la dunia la mwaka 1994 Brazil iliwaduwaza wengi, baada ya kukaa kwa miaka 24 bila ya kuchukua ubingwa wa dunia au hata kushiriki katika hatua fainali, kwani iliweza kutwaa tena ubingwa kwa mara ya 4 huko nchini Marekani walipovaana na Italy.

    Brazili iko kwenye kundi A katika michuano ya mwaka huu, kundi lake linaundwa na timu ya taifa ya Croatia, Mexico na vinara wa Afrika wa siku nyingi timu ya taifa ya Cameroon. Kundi hili linatajwa kuwa la kipekee kutokana na timu zinazounda kundi lake kama vile Mexico na Croatia ambazo ni timu ngumu kufungika.

    Mshambuliaji wake Neymar, tayari ametajwa kama kinda ambaye atawika na timu yake ya taifa iliyopata ubingwa mara tano kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao na chenga za maudhi uwanjani. Pia katika upande wa mashambulizi yuko mchezaji Robinho anayekipiga katika klabu ya Santos, huku Dani Alves anayecharaza soka katika klabu ya Barcelona akihesabiwa kama mchezaji machachari wa timu hiyo, mbali na hao pia kuna mlinda mlango mkongwe, Julio Cesar. Na kwa kipindi cha zamani wachezaji waliovuma ni pamoja na Garrincha, Pele, Bebeto na Ronaldo De Lima.

    Ingawa Brazil ilishinda katika kombe la Superclassic of the America la mwaka 2012, kufuatia matokeo mabaya ya mwaka 2012, Novemba 23 mwaka huohuo kocha Mano Menezes alifukufuzwa kwenye timu hiyo, chama cha mpira nchini humo kilitakiwa kitangaze mtu wa kuchukua nafasi yake Januari mwaka jana, lakini badala yake Novemba 28 walimteua Luiz Felipe Scolari kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil. Mechi ya kwanza iliyocheza Brazil chini ya kocha huyo mpya ambayo ilikuwa Februari 6 mwaka jana, Brazil ilibanjuliwa mabao 2-1 na England katika uwanja wa Wembley.

    Brazil ilifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia la mwaka 1958 nchini Sweeden, Chile mwaka 1962, Mexico mwaka 1970, Marekani mwaka 1994, Korea na Japan mwaka 2002 ambapo walikuwa mabingwa. Pia imefanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 ambapo mwaka 1983 ilishiriki kule nchini Mexico, pia ile iliyofanyika kwenye nchi za kisovite mwaka 1985, Australia mwaka 1993, falme za kiarabu mwaka 2003 ambapo walikuwa mabingwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako