• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hefei

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:37:20

    Awali, mji wa Hefei ulijulikana kama Ho-fei, Luzhou, au Luchow, na mji mkuu wa mkoa wa Anhui ulioko mashariki mwa China. Mji huo wenye ngazi sawa na wilaya, ni makao makuu ya kisiasa, kichumi, na kiutamaduni ya mkoa wa Anhui. Mji wa Hefei unapakana na Huainan upande wa kaskazini, upande wa kaskazini mashariki unapakana na Chuzhou, kusini mashariki unapakana na Chaohu, na magharibi, mji huo unapakana na Lu'an.

    Hefei una eneo la mraba la kilomita 11,323, na kutokana na sensa ya mwaka 2013, idadi ya jumla ya watu kwenye mji huo ni milioni 7,611.

    Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, mji mkuu wa mkoa wa Anhui ulihamishiwa Hefei kutoka Anqing. Ili kusaidia maendeleo ya mji huo, watu wengi wenye ujuzi kutoka mikoa mbalimbali nchini China walipelekwa mjini humo. Hivi sasa mjini Hefei kuna viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya kutengeneza mashine, vifaa vya elektroniki, madawa, vyuma, nguo, na sigara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako