• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wuhu

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:37:56

    Wuhu ni mji ulioko kusini mashariki mwa mkoa wa Anhui, na mji huo una hadhi sawa na wilaya. Ukiwa kusini mashariki mwa Mto Yangtze, Wuhu umepakana na Xuancheng upande wa kusini mashariki, Chizhou na Tongling upande wa kusini magharibi, Hefei kaskazini magharibi, Ma'anshan upande wa kaskazini mashariki, na mkoa wa Jiangsu upande wa mashariki. Idadi ya watu mjini Wuhu ni milioni 3,443,192 kutokana na sensa ya mwaka 2010. Mji huu ni wa pili kiuchumi mkoani Anhui baada ya mji wa Hefei. Mwaka 2011, kiwango cha GDP mjini Wuhu kilifikia Yuan bilioni 165.8, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 ikilinganishwa na mwaka 2010. Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi na Teknolojia la Wuhu lilianzishwa mwaka 1993, na ni moja ya maeneo ya ngazi ya juu ya maendeleo ya kiuchumi na teknolojia mkoani Anhui, pia ni eneo pekee la kusafirisha bidhaa nje ya nchi katika mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako