• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Anqing

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:39:51

    Anqing ni mji wenye ngazi sawa na wilaya ulioko kusini magharibi mwa mkoa wa Anhui. Unapakana na Lu'an upande wa kaskazini, Hefei na Wuhu upande wa kaskazini mashariki, Tongling upande wa mashariki, Chizhou upande wa kusini mashariki, mkoa wa Jiangxi upande wa kusini, na upande wa magharibi, mkoa wa Hubei. Mji wa Anqing ni muhimu kwa viwanda vya nguo, spea za magari, chakula, na chai.

    Opera ya Huangmei ni mojawapo katika opera maarufu aina tano nchini China, na pia ni opera kuu mkoani Anhui. Katika sehemu mbalimbali za China, zikiwemo mikoa ya Hubei, Jiangxi, Zhejiang, Jiangsu, Taiwan na hata eneo la utawala maalumu la Hongkong, pia kuna makundi ya waigizaji wataalamu na wale wanapenda kuimba opera hiyo, ambao wanapendwa sana na wakazi wa huko. Opera ya Huangmei ilikuwa ni opera ya mitaani ya mji wa Anqing, na baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, opera hiyo ilikua kwa kasi na kuwa yenye ushawishi mkubwa nchini China, na hata kuenea nje ya nchi. Mwaka 2006, opera ya Huangmei iliorodheshwa kuwa urithi wa utamaduni usioshikika wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako