• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huangshan

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:40:50

    Huangshan ni mji ulio kwenye milima iliyoko kusini mwa mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. Mji huo umejengwa kwenye milima inayotokana na vitu vilivyotolewa baharini wakati wa enzi za Mesozoi, miaka milioni 100 iliyopita.

    Mji huo ni maarufu kutokana na mandhari yake nzuri, kuzama kwa jua, vilele vya milima vyenye maumbo ya ajabu, miti aina ya misonobari ya Huangshan, chemchemi za maji moto, barafu wakati wa baridi, na mwonekano wa mawingu. Mara nyingi mji wa Huangshan umetumika kwenye michoro ya kitamaduni ya China pamoja na hadithi, vilevile mji huo unapendwa sana na wapiga picha wa kisasa.

    UNESCO imeuorodhesha mji wa Huangshan eneo la urithi wa dunia, na moja ya vivutio vikuu vya utalii nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako