• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Risala ya naibu waziri wa utamaduni ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya Mabaki ya kale ya Utamaduni ya China

    (GMT+08:00) 2014-12-10 16:11:35
    Ingawa China na Afrika zimetenganishwa kwa bahari kubwa yenye mawimbi makali, bahari hiyo haiwezi kuzuia utafiti unaofanywa na pande hizi mbili. Mapema wakati wa kipindi cha Enzi ya Song zaidi ya miaka 700 iliyopita, vyombo vya kauri vya China vilisafirishwa hadi kwenye sehemu ya pwani ya mashariki ya Afrika, msafiri maarufu wa Enzi ya Yuan Bw. Wang Dayun aliwahi kutembelea Kisiwa cha Zanzibar; na Bw. Zheng He aliongoza kundi la merikebu kufanya mawasiliano ya kirafiki na watu wa Afrika mashariki zaidi ya miaka 600 iliyopita, ambaye alirudi nyumbani China na Twiga, wanyama waliowashangaza watu wa China. Njia hii ya mawasiliano ilivuka bahari kubwa na kuunganisha China na Bara la Afrika, ambapo watu wa pande mbili walifanya biashara ya kubadilishana vito na vitu vingine vyenye thamani, ilisukuma mbele maingiliano kati ya mabara ya Asia na Afrika katika mambo ya utamaduni, sanaa na teknolojia.

    Huu ni mwaka wa 50 tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika miaka 50 iliyopita, nchi hizi mbili zimeongeza siku hadi siku mawasiliano na mashirikiano katika sekta ya utamaduni. Mwaka 2013, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara rasmi nchini Tanzania, ziara hiyo iliimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki kati ya China na Tanzania, na kuongeza maelewano na urafiki kati ya nchi hizi mbili. Katika zama za kale, watu wa China walitumia ufundi wa "kuongoza merikebu kwa kufuata nyota" na kufanya safari ndefu baharini. Ili kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania, tumekuja hapa na mabaki ya utamaduni ya mamia na maelfu ya miaka iliyopita, tukishirikiana na Jumba la Makumbusho la taifa la Tanzania kufanya "Maonesho ya Historia na Utamaduni ya Njia ya Hariri baharini kati ya China na Tanzania". Hii ni mara ya kwanza kwa China kufanya maonesho ya mabaki ya kale ya utamaduni katika Afrika ya mashariki, pia ni mara ya kwanza kwa China na Tanzania kufanya kwa pamoja maonesho kama haya. Ni matumaini yetu kuwa, maonesho haya yatathibitisha historia ya urafiki kati ya nchi zetu mbili, na kuleta uhondo wa utamaduni kwa wananchi wa Tanzania.

    Maonesho haya yamepata uungaji mkono mkubwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania na Ubalozi wa China nchini Tanzania. Kwa niaba ya Idara ya mabaki ya kale ya utamaduni ya Jamhuri ya Watu wa China, nawashukuru watu wa sekta mbalimbali wa China na Tanzania kwa juhudi zao ili kufanikisha maonesho haya. Nina matumaini ya dhati kuwa maingiliano ya utamaduni kati ya China na Tanzania yataendelea kufanyika kwa kina siku hadi siku.

    Ninayatakia maonesho haya mafanikio!

    Naibu waziri wa utamaduni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mabaki ya kale ya Utamaduni ya China

    Li Xiaojie 5/11/2014

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako