• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Risala ya Balozi Lv Youqing kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Historia na Utamaduni ya Njia ya Hariri baharini kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2014-12-10 16:12:28

    Wageni waheshimiwa

    Mabibi na Mabwana:

    Leo tunapoadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania, nafurahi sana kushiriki pamoja nanyi kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Historia na Utamaduni ya Njia ya Hariri baharini kati ya China na Tanzania. Kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, ninawakaribisha wote mliokuja kushiriki kwenye ufunguzi wa maonesho haya, ninapongeza kufunguliwa kwa maonesho haya, na ninaishukuru kwa dhati Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania, Jumba la Makumbusho la taifa la Tanzania, pamoja na idara nyingine na watu wote kwa msaada na uungaji mkono wenu kwa ajili ya ufunguzi wa maonesho haya.

    Mabibi na Mabwana,

    Kuna urafiki wa jadi ulio kama wa ndugu kati ya China na Tanzania, nchi zetu mbili siku zote ni wenzi wa ushirikiano wa kimkakati. Tokea nusu karne iliyopita, uhusiano kati ya nchi zetu mbili ulikumbwa na majaribu kwenye mabadiliko makubwa katika hali ya kimataifa, ukiimarishwa siku hadi siku, na umekuwa mfano wa kuigwa kwa uhusiano kati ya China na Afrika na urafiki na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea. Mwezi wa Machi mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya mafanikio nchini Tanzania, na mwezi Oktoba mwaka huu ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini China pia imepata mafanikio makubwa. Marais wa nchi zetu mbili wametoa mwelekeo kwa urafiki na ushirikiano kati ya China na Tanzania, na kuthibitisha malengo ya kimkakati ya kuuendeleza uhusiano kati ya nchi mbili kwenye kiwango cha juu zaidi.

    Mabibi na Mabwana,

    "Uhusiano mzuri kati ya nchi na nchi unatokana na mawasiliano mazuri kati ya wananchi". Ushirikiano kati ya China na Tanzania kwenye sekta za utamaduni na elimu siku zote una mafanikio zaidi katika maendeleo ya uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya nchi zetu mbili. Katika miaka ya hivi karibuni, vyuo viwili vya Confucius vilianzishwa katika Chuo kikuu cha Dodoma na Chuo kikuu cha Dar es Salaam; tamthiliya za China zilizotafsiriwa na kutiwa sauti ya Kiswahili , , na zilioneshwa kwenye Kituo cha Televisheni cha Tanzania; maandalizi ya kuanzishwa kwa Kituo cha Utamaduni wa China yanafanyika kwa pilikapilika, na yatakamilika siku chache baadaye. Udhamini wa masomo wa Serikali ya China utaongezwa kutolewa kwa wanafunzi 120 kutoka 100, ili wanafunzi vijana wengi wa Tanzania wapate fursa ya kwenda kusoma China. Mwelekeo mzuri wa kufanya maingiliano na kufundishana kati ya China na Tanzania unaonekana katika sekta za utamaduni na elimu.

    Mabibi na Mabwana,

    Katika karne kadhaa zilizopita, Njia maarufu ya Hariri baharini ilisaidia kuwepo kwa biashara kubwa ya vito na vitu vingine vyenye thamani kati ya China na Afrika, na kusukuma mbele mawasiliano na maingiliano kati ya pande mbili katika sekta za sayansi na teknolojia, dini na utamaduni.

    Maonesho ya Historia na Utamaduni ya Njia ya Hariri baharini kati ya China na Afrika yanafanyika mara ya kwanza barani Afrika. Kutokana na vitu vya mabaki ya kale ya utamaduni vilivyofukuliwa nchini China na nchini Tanzania, maonesho hayo yanakumbusha historia ya urafiki, mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa China na Afrika, na kuonesha ustawi wa uchumi wa China na Afrika pamoja na kupatana kwa tamaduni mbalimbali kutokana na mawasiliano kupitia Njia ya Hariri baharini, na kueleza matarajio ya siku nzuri za baadaye za China na Afrika, na China na Tanzania kufanya ushirikiano kwa pande zote katika kujenga Njia ya Hariri baharini ya Karne ya 21.

    Mwisho nayatakia maonesho haya mafanikio mema !

    Asanteni sana!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako