• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelezo mafupi kuhusu Jumba la Makumbusho la taifa la Tanzania

    (GMT+08:00) 2014-12-10 16:13:01

    Jumba la Makumbusho la taifa la Tanzania liko kwenye Mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam, jumba hilo pia linaitwa "Jumba la Makumbusho na Familia ya Utamaduni", hii ni idara ya umma inayoendeshwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania, chini yake kuna majumba matano ya makumbusho, kati ya hayo Jumba la makumbusho la Dar es Salaam liko kwenye Jumba la makumbusho la taifa. Mkurugenzi wa sasa wa jumba hilo la taifa ni Bw. Audax Mabulla, naibu wake ni Bibi Adelaide Sallema.

    Jumba la Makumbusho la Dar es Salaam lilianzishwa mwaka 1934, awali lilianzishwa na Serikali ya Tanganyika kwa ajili ya kumkumbuka Mfalme George V, na lilifunguliwa rasmi kwa umma mwaka 1940. Jumba hilo lilifanyiwa upanuzi mwaka 1963, ambapo ziliongezwa sehemu kadhaa za maonesho. Jengo kuu la jumba hilo la maonesho la sasa lilisanifiwa na Kampuni ya ujenzi ya TENGO ya Sweden, ujenzi wake ulikamilika mwaka 2011. Aidha Chuo kikuu cha Stockholm cha Sweden kilitoa fedha maalum kusaidia ujenzi wa Kituo cha mafundisho ya vyombo vya habari kwenye jumba jipya. Katika upanuzi wa mara ya mwisho, majengo yaliyojengwa mwaka 1934 yenye mtindo wa Kiarabu yamehifadhiwa kikamilifu na kubaki kama yalivyo, na bado yanatumika kwa kufanyia maonesho ya historia, ambapo yanang'ara pamoja na majengo ya jumba jipya la sasa.

    Katika mabaki ya kale ya utamaduni yanayohifadhiwa kwenye jumba hili, mabaki ya binadamu wa kale yaliyogunduliwa nchini Tanzania ni yenye thamani kubwa na yanajulikana zaidi duniani; wasimamizi wengi wa jumba hilo waliwahi kupata elimu ya utafiti wa mabaki ya kale, na kwenye jumba hilo pia kuna maabara ya utafiti wa mabaki ya kale kuhusu binadamu wa kale, pamoja na majengo mengine ya kufanyia utafiti. Zaidi ya hayo, ndani ya jumba hilo pia vinahifadhiwa vitu vingi vya mabaki ya kale vilivyogunduliwa huko Kilwa na sehemu nyingine muhimu ya mabaki ya kale ya utamaduni nchini Tanzania, pamoja na baadhi ya mabaki ya kale yaliyoachwa kutoka wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza na Ujerumani. Kinachostahiki kutajwa ni kuwa, mabaki mengi ya vyombo vya kauri yanahifadhiwa pia katika jumba hilo, mabaki hayo ya vyombo vya kauri yote yalifukuliwa nchini Tanzania, hasa kwenye sehemu ya pwani ya mashariki ya Afrika, mabaki hayo yana umuhimu mkubwa kwa ajili ya utafiti juu ya mawasiliano baharini kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako