• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelezo kwa Watazamaji

    (GMT+08:00) 2014-12-10 16:35:00

    Kutoka kundi kubwa la Merikebu lililoongozwa na Zheng He, hadi wataalamu na mafundi waliojenga Reli ya TAZARA bila kuogopa kutokwa na jasho jingi, historia ya mamia na maelfu ya miaka imeonesha kuwa, nia na dhamira ya kuvuka bahari ya mbali waliyonayo wachina, siku zote inasukuma mbele mawasiliano ya amani na maendeleo ya uwiano kati ya nchi zenye tamaduni tofauti. Ingawa safari baharini kutoka China hadi Afrika ni ndefu sana, lakini katika mamia na maelfu ya miaka iliyopita, siku zote binadamu hawajapunguza shauku yao ya kufanya utafiti juu ya dunia ambayo bado hawajaifahamu kikamilifu.

    Hali ya merikebu nyingi zenye matanga zilivyoshindania kusafiri kwenye bahari kubwa ya mbali imepita kwa miaka mingi sana, hata mababu zetu hawakuacha nyayo kwenye bahari yenye mawimbi makali. Lakini cheche ya moto iliyotokana na maingiliano kati ya binadamu wenye tamaduni tofauti imeachwa daima kwenye bahari ya amani na urafiki. Mawasiliano makubwa kati ya China na Afrika kwenye njia ya baharini yalikuwa na historia ndefu na yamekuwa mwanzo mpya, ambayo yanaonesha nguvu kubwa ya uvumbuzi na uhai kwenye njia hiyo ya mawasiliano baharini katika zama za kale, na hakika yatang'ara upya kwa dunia ya karne ya 21.

    [Saa ya Mbingu na Ardhi]

    picha ya mafuta iliyochorwa na He Xun mwaka 2013/ inahifadhiwa kwenye Kituo cha Sanaa za Zama hizi cha Fengchao

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako