• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namna ya kusalimiana wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China

    (GMT+08:00) 2015-02-11 14:48:10

     

    Kutakiana heri ya mwaka mpya ni desturi muhimu katika jamii ya wachina. Watoto wadogo wanawatakia heri na baraka wakubwa, jamaa na marafiki wanatembeleana na kusalimiana, na kusherehekea sikukuu hiyo kupitia kuambiana maneno hayo yenye baraka.

    Hadithi inasema kuwa zamani watu waliogopa mnyama wa ajabu aiitwaye "nian" aliyekula binadamu kila ilipofika usiku wa mkesha wa mwaka mpya, hivyo walificha nyumbani usiku kucha na kutoka nje baada ya jua kuchomoza ambapo mnyama huyo alikuwa ameondoka, watu wakasalimiana na kutakiana heri kwani walikuwa bado uhai. Inasemekana kuwa huu ndio mwanzo wa desturi ya kutakiana heri katika siku ya kwanza ya mwaka mpya.

    Siku hiyo, watu wadogo huwa wanawatembelea wakubwa, na kuwatakia afya njema na maisha marefu. Watu wanapokutana mtaani wanasalimiana kwa kuongea maneno yenye baraka, na majirani au marafiki huwa wanatembeleana au kukusanyika kwa pamoja kula chakula au kunywa pombe kusherehekea sikukuu.

    Hata hivyo kadri mtindo wa maisha unavyobadilika na maeneo wanayoishi watu kupanuka, ndivyo njia za kusalimiana kwa watu kwenye sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China zinavyobadilika. Watu wenye umri mkubwa wanaendelea kushikilia desturi ya kuwatembelea marafiki zao na vijana wanapendelea njia za kisasa kusalimiana. Njia mbalimbali za kusalimiana zinazounda mtandao wa kijamii, na kutoa hisia fulani kunalingana na umbali wa mioyo kati ya watu.

    Desturi ya jadi: kuwatembelea ndugu na marafiki, udhati mkubwa wa moyo, lakini kunatumia muda na kuna usumbufu kidogo

    Awali maeneo waliyoishi watu yalikuwa ni madogo ikilinganishwa na ya siku hizi, na vyombo vya mawasiliano pia vilikuwa vichache, hivyo kutumia sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ili kukutana na jamaa na marafiki ambao hawajakutana kwa mwaka mzima, na kuongozana na wakubwa na wadogo kuwatembelea marafiki na jamaa kunaonesha udhati mkubwa wa moyo. Watu waliwasalimia wengine nyumbani kwao wakiwa na sigara na pombe, pipi au nyama walizotengeneza kwa mikono na kugonganisha vikombe kwenye sauti ya fataki na mbele ya vyakula vingi vitamu mezani kuna kionjo kikubwa cha sikukuu.

    Akikumbuka sikukuu ya mwaka mpya wa jadi katika siku za utotoni mwake, Mzee Yao mwenye umri wa miaka 80 anasema kila ifikapo mwaka mpya wa jadi wa China, alikuwa na hamu kubwa ya kwenda kuwasalimia babu, bibi, mjomba na wengine wanafamilia kwani aliweza kupata sukari na pesa kutoka kwao zikiwa ni kama zawadi ya sikukuu. Anasema,

    "Zamani, hali ilikuwa ya kimaskini, sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China ni jambo kubwa, watoto waliweza kupata pesa za baraka au vitu vipya kwa kuwatembelea watu wazima, na jamaa na marafiki walitembeleana, jambo ambalo lilikuwa zuri sana. Lakini siku hizi vijana hawapendi kutembea tembea, wanaona ni usumbufu kidogo. Kwangu mimi, naweza kuelewa, kwani wanafanya kazi kwa jasho, na mwisho wanapata mapumziko ya sikukuu, wanataka kupumzika nyumbani, pia ni nzuri."

    Mtindo wa makazi ya watu wa kisasa pia unaathiri njia za kusalimiana za sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Siku hizi, watu wengi wanaishi katika majengo ya ghorofa, na kila familia inaishi katika nyumba yake inayofungia mlango, hali ambayo inasababisha watu kutokuwa na hali ya kufahamiana na kukaribiana. Hata hivyo, jamaa na marafiki pia wanapendelea kutembeleana wao wenyewe, kwani kulingana na simu au mtandao wa internet, hii inaonesha urasmi na udhati. Na watu wengi wameanza kujirudishia mtindo huo ulio wa zamani lakini wenye hisia nzito, kwani kuzidisha upendo hakuhitaji vitu vyenye pesa nyingi, cha muhimu ni kuzungumza uso kwa uso.

    Njia inayotumiwa kwa wingi: Ujumbe wa siku za mkononi, lakini maneno yanajirudia na hakuna mapya

    Hivi sasa wachina wengi zaidi wanatakiana heri ya mwaka mpya kwa kutumia ujumbe wa simu za mkononi. Uchunguzi uliofanywa kupitia mtandao wa internet unaonesha kuwa, asilimia 77.78 ya watu wanachagua ujumbe wa simu za mkononi kuwa njia ya kwanza ya kusalimiana. Katika siku moja ya mkesha wa mwaka mpya wa 2013, wachina walituma ujumbe zaidi ya bilioni 12. Lakini ujumbe wa simu ya mkononi ambayo ni njia rahisi na inayoweza kupokelewa bila kujali mahali unakoishi pia ina mapungufu mengi, maneno ya ujumbe yanajirudia na hakuna mambo mapya, bei inakuwa kubwa kama ukiwatumia watu wengi, na pia baadhi ya wakati, unashindwa kutuma kutokana na idadi kubwa ya ujumbe kwa wakati mmoja kwenye mkesha wa mwaka mpya.

    Watu wengi wanaona hawawezi kusikia furaha ya mwaka mpya wanapopokea ujumbe, na hata baadhi yao wanachukia kupokea salamu kupitia ujumbe wa simu za mkononi, ambapo neno moja la "heri ya mwaka mpya" au maneno yale yale wanayopokea kutoka kwa watu mbalimbali tofauti, haviwafanyi kuhisi udhati wa salamu.

    Kijana Che mwenye umri wa miaka 30 anasema hapendi kupokea salamu kupitia ujumbe wa simu za mkononi, kwani anaona salamu ya aina hiyo haiwezi kuonesha udhati wa moyo, lakini ni kama "nidhamu", na kwamba haifai kutosema chochote wakati wa sikukuu, hivyo wanalazimika kutumia ujumbe kutoa salamu zao zisizotoka mioyoni mwao. Anasema

    "Nachukia kupokea salamu ambazo ni dhahiri kwamba maneno wanayonitumia ni sawa tu na ya wengine, kwani nahisi kwamba wanachukulia kunitumia salamu ni kama kazi ya lazima, hivyo napendelea kuwasalimia kwa kuwapigia simu, na hata nikituma ujumbe, natunga maneno mimi mwenyewe, na kuwasalimia watu tofauti kwa maneno tofauti." Vilevile mtu aliyejiandikisha kwenye tovuti kwa jina la "Yi Qi Yi Hui" ametoa maoni yake, akisema "baadhi ya wakati napokea ujumbe kunitakia heri ya mwaka mpya kutoka kwa mtu mwenye nambari nisiyoifahamu, naona kama nikimwuliza yeye ni nani, itakuwa si adabu, lakini kama nikipokea, nitawajibu bila kujali yeye ni nani, na hata kuwatumia wengine ujumbe mmoja kwa wote."

    Njia ya mtindo wa kisasa zaidi: kutumia Microblog (kitu kama twitter) au Wechat, mchanganyiko wa picha, maneno na sauti usiotumia pesa na kupunguza muda

    Microblog na wechat zikiwa programu za mtandao wa kijamii zinafanya njia za watu kudumisha mapenzi yao kuwa ya aina mbalimbali. Vijana wengi wanapenda kubaki nyumbani wakati wa sikukuu, na kutuma salamu zao kwenye microblog na Wechat, salamu hizo sio maneno tu, pia zinajumuisha picha, au sauti zao wanazorikodi wao binafsi. Wanatumia mtandao wa internet ambao ni jukwaa lisiloonekana kujieleza na kuwasiliana kimapenzi.

    Sababu kuu ya vijana kupendelea kutumia mtandao wa kijamii kusalimiana ni kuwa hili ni jukwaa muhimu la kuongeza mshikamano kati ya watu. Kijana Li mwenye umri wa miaka 20 bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu, na yeye ni shabiki wa kutumia microblog na wechat kutoa salamu zake kwenye sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Anasema,

    "Tunapokutana na marafiki zangu tunajipiga picha na kuweka kwenye mtandao, huku tukionesha maisha yetu kwa wakati mmoja. Kusoma microblog na kundi la marafiki la watu wengine kwenye Wechat, "kubonyeza like", kubakiza ujumbe wako chini, inaonekana kuwa kila mtu anaweza kujiunga kwenye shughuli za wengine za kusherekea sikukuu, na pia mambo hayo hayatumii pesa." Ikilinganishwa na simu, ujumbe wa simu za mkononi, kuibuka kwa njia za kutumia microblog na wechat kutoa salamu kunatokana na gharama ya internet inayozidi kupungua nchini China.

    Kusalimiana katika mwaka mpya ni shughuli muhimu yenye mila katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, ingawa siku hizi kuna aina nyingi za njia za kusalimiana, ambazo zinaonesha sifa ya karne mpya, lakini udhati wa moyo wa wachina wa kusalimiana hautabadilika kamwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako