• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya kumkaribisha mungu wa utajiri

    (GMT+08:00) 2015-02-11 15:04:05

     

    Msikilizaji mpendwa, leo ni tarehe 23, pia ni tarehe 5 mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kichina. Katika utamaduni wa China, siku ya tano baada ya kuingia katika mwaka mpya ni siku muhimu sana. Mambo makubwa yanayotakiwa kuzingatiwa ni pamoja na kumfukuza mungu wa umaskini, kumkaribisha mungu wa utajiri, na kufungua soko jipya.

    Inasemekana kwamba, watu hufungua milango na madirisha saa 6 kamili usiku wa manane siku hiyo, na kulipua fataki kwa imani kuwa, ukifanya hivyo, bila kujali utaelekea mashariki, magharibi, kusini, kaskazini au katikati, utapata utajiri mkubwa. Baada ya kumpokea mungu wa utajiri, unatakiwa kunywa pombe hadi alfajiri. Kutokana na desturi ya kale ya China, wafanyabiashara hufanya tambiko kwa kufukiza udi mbele ya sanamu ya mungu wa utajiri kuomba kutajirika, na hufungua maduka yao na kuanza biashara ya mwaka mpya baada ya mapumziko kuanzia tarehe 1 hadi 4 ya mwezi wa kwanza.

    Kwa nini wachina wanamkaribisha mungu wa utajiri leo? Inasemekana kuwa, siku ya tano Januari kwa kalenda ya kichina ni siku ya kuzaliwa kwa mungu wa utajiri. Mkazi wa mji wa Guanzhou Bibi Liu anayetembelea Kasri la Sanyuan anasema:

    "Namkaribisha mungu wa utajiri, anatuletea fedha pamoja na baraka katika mwaka huu mzima."

    Sio wachina pekee wanaopendezwa na mazingira haya mazuri ya sikukuu ya Spring, bali pia wageni wanaoishi nchini China wanafurahia utamaduni huo. Mjini Xi'an, katika hekalu la Louguan, wanafunzi wawili kutoka Uturuki wanaangalia sanamu za mungu wa utajiri za 3D. Mungu huyu ameshika upanga mkali mkononi, na amekalia chui.

    "Tunavaa nguo za mtindo wa kale wa enzi ya Han, naona fahari kubwa, watu wa miaka 2,000 iliyopita walikuwa na nguo zinazopendeza."

    "Tukifika hapa tunajisikia utamaduni wa zaidi ya miaka ya elfu mbili wa China, ni nzuri kwa sisi kujisikia utamaduni huo. Nataka kusema, hekalu hili ni zuri sana."

    Hadhithi ya kichina inasema, awali kulikuwa na majua kumi mbinguni, na kila moja linawakilishwa na mungu tofauti, lakini hali hii ilileta joto kali kiasi kwamba, binadamu walisumbuka sana. Kwa hiyo aliibuka shujaa mmoja aitwaye Hou Yi, alitungua miungu tisa kwa mishale na kuacha mmoja tu, miungu iliyotunguliwa ikabadilika kuwa mashetani, ila tu mungu wa utajiri mwenye jina la Zhao Gongming ambaye alibadilika na kuwa na sura ya binadamu. Baada ya kuanguka duniani alitua milimani, na baadaye aliteuliwa na mungu mkuu kuwa mungu anayeshughulikia mali kwa binadamu.

    Kutokana na uwezo wake huo watu wengi hasa wafanyabiashara wanamwabudu kama mungu wa utajiri na kumtambikia. Katika siku hiyo ya tano ambayo pia inaitwa "powu" kwa lugha ya kichina, wachina hutoa takataka zote nje. Mjini Beijing, duka moja la bidhaa za magari linafunguliwa leo. Mapema asubuhi, wafanyakazi wamechapisha kazi zao. Kijana Li anasafisha mbele ya mlango wa duka. Anasema, jambo muhimu la leo ni kufanya usafi.

    "Kuanzia siku ya kwanza ya sikukuu hadi siku ya nne, hatuwezi kusafisha, lakini siku ya tano tunaondoa mungu wa umaskini, na kufanya usafi kamili, ambapo tutaondoa vitu vyote vichafu."

    Nchini China, siku ya kufukuza mungu wa umaskini ni tofauti, kusini mwa China ni siku ya tatu katika sikukuu, kaskazini ni siku ya sita, huko mjini Shanghai ni siku ya tano ambayo ni leo. Mkazi wa mji huo Bibi Wang anatueleza:

    "Naondoa takataka zote zilizokusanywa kuanzia siku ya kwanza ya sikukuu hadi sasa, naondoa mungu wa umaskini."

     

    Bila kujali ni siku gani, watu wote nchini China wanataka kueleza matarajio mema ya kuondoa umaskini na kukaribisha maisha mazuri yenye utajiri. Kutokana na utamaduni wa sikukuu hiyo, mkesha hadi siku ya nne ya sikukuu hiyo, watu hawafanyi usafi, takataka zinatakiwa kuwekwa pembeni tu. Hususan katika siku ya kwanza, fagio haiwezi kutumika, kwa sababu ikitumika bahati nzuri itaondolewa. Ifikapo siku ya "powu", watu wanatoa takataka zote nje ya nyumba, huku wakilipua fataki kutoka ndani ya nyumba hadi nje, wanaweka fataki kubwa sana kwenye takataka hizo ikiwa na maana kuwa, umaskini umeondolewa, na baada ya kazi hiyo kukamilika, watu wanakula chakula.

    Kwa mujibu wa desturi nyingine inayohusu sikukuu ya Spring, watu "hufungua mlango na kulipua fataki" leo, maana yake ni kuwa, kila familia inatakiwa kulipua fataki, ikiwa ni jambo la kwanza baada ya kufungua mlango. Hii ina historia ndefu ya zaidi ya miaka elfu mbili. Watu walisherehekea sikukuu hiyo kwa kulipua fataki ikimaanisha kuwafukuza mashetani, na vilevile kuweka mazingira mazuri yenye furaha na baraka. Sasa nchini China kuna fataki za aina nyingi na matumizi mengi, kwa mfano katika sherehe ya ndoa, kuhamia nyumba mpya, kufunguliwa kwa maduka, na sikukuu mbalimbali ikiwemo sikukuu ya Spring.

    Wachina wengi wanaona, kama hakuna fataki, sikukuu inakuwa na upungufu mkubwa. Lakini kutokana na usalama na uchafuzi wa mazingira sasa watu wengi nchini China wameacha desturi hiyo. Mwaka huu kwa mfano, muda wa kuuzwa kwa fataki uliopangwa na serikali unapunguzwa hadi siku kumi tu. Na kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya raia uliofanyika kabla ya sikukuu ya Spring, asilimia 25 ya watu walioulizwa wameeleza kuwa hawatanunua fataki yoyote.

    "Fataki zinavutia."

    "Kila mwaka uliopita, tuliwasha fataki, watoto wanazipenda, zinaweza kufanya mazingra ya sikukuu yawe na uchangmfu na furaha."

    "Basi tufuate sera inayotungwa na serikali ya mji, yaani tunaweza kuwasha fataki wakati sifa ya hali ya hewa ni nzuri, na sehemu ya kuwasha fataki na kiasi gani. Tutatafuta njia inayokubalika na pande zote."

    "Kwa nini hatuwashi fataki? Kwa sababu hali ya hewa imechafuka sana, na wazee hawapendi hata kidogo sauti za fataki, fataki zikiwashwa nje, nafunga madirisha."

    Kutolipua fataki au kupunguza kiasi cha fataki sio tu chaguo la raia wenyewe, bali inafuatiliwa na watu wengi zaidi kwenye jamii. Imekuwa maoni ya pamoja kwa jamii nzima kuwa, kuhifadhi mazingira kunaanzia kupunguza kulipua fataki.

    Katika sherehe za mwaka mpya, watu hupendekeza kunywa kwa furaha, na kujiburudisha katika mazingira ya sikukuu, wakiwa na matumaini ya kuwa na baraka nyingi na maisha marefu, na mungu wa utajiri, na fataki zimebeba matumaini ya watu ya kutakiana kila la heri maishani na baraka katika mwaka mpya.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako