• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upendo usiokuwa na mipaka

    (GMT+08:00) 2015-03-10 21:08:18

    Tangu China ilipotuma kikundi cha madaktari barani Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1963, China imeendelea na kazi hiyo kwa miaka 51. Mwaka 2013 Rais Xi Jinping alipokutana na ujumbe wa madaktari hodari waliotoa msaada wa matibabu nchi za nje alisema, kutoa msaada wa matibabu ni sehemu muhimu ya diplomasia ya China, madaktari wa China si kama tu wamehimiza maendeleo ya jukumu la afya la nchi walipotoa msaada na kuinua kiwango cha afya za watu wa huko, bali pia wamehimiza urafiki kati ya wananchi wa China na nchi nyingine.

    Mlipuko wa Ebola ulitokea kwenye nchi za Afrika magharibi kuanzia mwezi Februari mwaka 2014. Ili kukabiliana na msukosuko huu wa afya wa kimataifa, serikali ya China imepeleka wataalamu wa matibatu na vikundi vya madaktari kwa mara 10, ambao idadi yao imezidi 1,000. Hatua hiyo ya serikali ya China imesifiwa na jumuiya ya kimataifa hasa nchi za Afrika na wananchi wake.

    Kwenya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola, licha ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola, madaktari wa China wamefanya juhudi kutoa mafunzo kwa madaktari wa huko kuhusu mbinu za kukinga na kudhibiti ugonjwa wa Ebola. Wameonesha sura ya wachina ya kupenda amani na kustahi maisha ya watu, pia wameonesha imani ya wachina kuhusu kukabiliana na matatizo pamoja na waafrika.

    Ili kuonesha moyo wa kibinadamu wa kimataifa, kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China na shirikisho la urafiki wa wananchi wa China kwa nchi za nje zimeendesha shughuli za "Upendo unaopita mpaka, kutafuta madaktari wazuri waliotoa msaada wa matitabu kwa nchi nyingine".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako