• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China kuhudhuria mkutano wa Baraza la Boao

    (GMT+08:00) 2015-03-18 11:07:51

    Katibu mkuu wa Baraza la Asia la Boao Bw. Zhou Wenzhong jana alisema, rais Xi Jinping wa China na viongozi wa nchi mbalimbali watahudhuria ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia la Boao, na mawaziri zaidi ya 80 kutoka nchi hizo pia wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

    Mkutano huo wenye kauli mbiu "Mustakbali mpya wa Asia: Kupiga hatua kuelekea mustakbali wa pamoja", utafanyika kuanzia tarehe 26 hadi tarehe 29 Machi huko Boao, mkoani Hainan.

    Mkutano huo utafuatilia zaidi sera za kifedha, na kujadili masuala ya kijamii na kisiasa, ikiwemo usalama wa chakula, mapambano dhidi ya ufisadi, virusi na binadamu, hewa chafu na afya, na hifadhi ya mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako