• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utangulizi kuhusu "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2015-04-13 16:25:31

    Kati ya mwaka 200 K.K. na 100 K.K., njia ya wafanyabiashara iliyoanzia nchini China na kunganisha mabara ya Asia, Ulaya na Afrika ilianza kutandaa katika ramani ya dunia. Njia hiyo iliyojulikana kama "Njia ya Hariri" ilishuhudia mawasiliano na ushirikiano wa watu wa nchi mbalimbali. Katika siku za hivi karibuni wazo jipya la kimkakati la kujenga kwa pamoja "Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri" na "Njia ya Hariri Baharini ya Karne 21", na kuanza kuonekana katika ramani ya sasa ya kiuchumi na kisiasa.

    Wazo hilo lililotolewa na rais Xi Jinping wa China mwaka 2014, linasisitiza kuwa nchi husika zinazohusiana katika maslahi na hatma zao zinatakiwa kuwa na ushirikiano wa kunufaishana, na kutafuta maendeleo na ustawi wa pamoja.

    Wazo hilo ambalo chimbuko lake ni la kihistoria linalounganisha China na nchi nyingine, na kufuata mkondo mkuu wa zama hii wa amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana. Wazo hilo linabeba ndoto ya nchi mbalimbali za kutimiza maendeleo na ustawi, na kuifanya Njia ya Hariri iliyokuwepo zamani iwe na maana mpya inayoendana na zama hizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako