• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dini ya kibudha na Kong fu zinafanya hekalu la Shaolin kuwa maarufu duniani.

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:36:07

    Hekalu la shaolin ni mojawepo wa vivutio maarufu za utalii wa ndani na nje hapa nchini China.

    Hii kutokana na kwamba kwenye hekalu hilo ndio chumbuko la aina moja ya Kong Fu ya China na pia ilitumiwa na mwingizaji Jet Lee kutayarisha filamu yake "Shao Linsi".

    Hivi karibuni mwandishi wetu Ronald Mutie alitembelea hekalu hilo na anaeleza zaidi.


    Katika mlima wa Song mkoa wa Henan nchini China ndipo linapopatikana Hekalu la Shaolin.

    Hapa ndipo chimbuko la sanaa marufu ya Kong fu na sasa ni kivuto kikubwa cha utalii.

    Licha ya kuwa hekalu la Shaolin ni la kale bado majengo, sanamu na minara yake iko imara pengine kutokana na ufundi wa hali ya juu uliotumika kulijenga.

    Vizazi hadi vizazi wamekuja hapa kwa mambo mawili kujifunza kungfu na dini ya kibudha.

    Mtawa Yan Ju amekuwa hapa kwa zaidi ya miaka kumi akijifunza dini.

    "Hekalu la shaolin lilijengwa mwaka wa 495 kabla ya kristo kama makao ya watawa wa ngazi ya juu kutoka India kuishi hapa na kuelimisha watu. Kila siku tunaamnka saa kumi na nusu alfajiri na kufanya somo la asubuhi ambalo ni kusoma misahafu ya Budha na baadaye usiku tunafanya somo linguine. Wakati wa sikukuu kama vile ya wafanyikazi zaidi ya watu 30, 000 wanakuja hapa"

    Miongoni mwa jamii, watawa wa Shaolin walikuwa maarufu kwa ujuzi wao wa kupigana ambao waliutumia kupambana na wavamizi na wezi.

    Walizingatia sana mazoezi , mafunzo ya kiroho na maadili.

    Yan Ju anaeleza uhusiano wa kehalu la Shaolin na Kungfu.

    "Hekalu la Shaolin ni mahali patakatifu pa dini ya kibudha na kwa hivyo lengo kuu ya watawa ni kuchunguza misahafu ya budha. Wanakaa kwa muda mrefu kila siku wakisoma na hivyo wanachoika sana kwenye mgogo na mwili wote kwa jumla. Kutoka na hali hiyo ya uchovu wanafanya Kungfu ili kuondoa uchovu na kulainisha viungo vya mwili"

    Umaarufu wa Shaolin pia umevuka mipaka ya China na kusambaa kote duniani.

    Kupitia kwa filamu iliotengenezewa hapa na mwingizaji maarufu wa Kong fu wa China, Jet Lee hekalu hili limepata umaarufu mkubwa na kila mwaka wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali hufika hapa kujifunza Kong fu na dini ya kibudha.

    Mabri Valeri amekuwa akijifunza Kong fu nyumbani nchini Ivory Coast lakini baada ya kupata udhamini wa hekalu hili ameweza kufika kwenye kitovu cha sanaa hii.

    "Utamaduni wa Shaolin na ule wa China kwa jumla ni maarufu sana na kwenye karne ya 21 watu wengi wanataka kujifunza utamaduni huo na hiyo ndio maana hata mimi nimekuja hapa . Baada ya kujifunza tutapeleka utamaduni huu wa China Afrika "

    Mbali na kufunzwa Kongfu wanafunzi wa Afrika pia wanasoma kichina ili kuelewa kwa undani maneno ya waalimu wao.

    Emmanuel kutoka Cameroon amekuwa kwenye hekalu la Shaolin kwa miaka 2 na sasa anaongea kichina vizuri.

    Familia yake ilidhani akipata fursa ya kwenda China atasomea taaluma kama ya uhadisi ama mafunzo yanayohusiana na miundo mbinu.

    Lakini anasema tayari alikuwa amekata kauli kutimiza lengo lake maishani.

    "Kuja hapa kwenye hekalu la shaolin ni kutimiza ndoto yangu. Mwanzoni nilidhani ningejifunza hata kuruka kama ndege kwenye hili hekalu lakini nilipokuja nikangundua unaweza kujifunza mambo mawili moja ni kungfu na pia dini ya kibudha. Jambo muhimu sio kuamoini dini yenyewe lakini ni kuheshimu watu wengine"

    Hekalu la Shaolin lina idara na miungu tofauti ambao wanatimiza maombi mbalimbali kama utajiri, mavuno mazuri na afya njema.

    Na pia kuna idara ya matibabu ambayo ina zaidi ya madawa 1, 000 ya miti shamba yaliotafitiwa na watawa kwenye hekalu hili.

    Hata hivyo watawa wanashauri siku zote kutafuta amani na utulivu wa kimawazo kama dawa bora zaidi kwa binadam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako