• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kong Fu inahitaji nguvu, nidhamu na kujitolea

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:39:28

    China inafahamika sana kwa sanaa yake ya Kong-fu ama wushu na watu wengi wanaamini kwamba kila mchina anaifahamu sanaa hiyo.

    Lakini watu wengi hawafahamu kwamba unahitaji mafunzo maalum ili kuwa stadi wa Kong-fu.

    Ili kupata picha ya vile inavyofunzwa sanaa hiyo Ronald mutie alitembelea mojawepo wa shule kubwa zaidi nchini China zinazotoa mafunzo ya Kong fu na hii hapa ripoti yake.


    Miruko ya kitaalam, matamshi mithili ya jeshi, na sauti za upanga wa kichina.

    Ndio makaribisho kwenye shule ya Tangou inayotoa mafunzo ya Kong-fu katika eneo la Deng feng mkoani Henan.

    Wakiwa na mavazi mekundu wanafunzi wanafuata amri za waalimu wao hatua kwa hatua bila kukosea.

    Han Hao Hao kwenye umri wa miaka 17 ni mmoja wa maelfu ya wanafunzi hapa.

    "nafanya mazoezi kwa masaa saba kila siku-jumatatu jumatano na ijumaa ni mafunzo ya sanda yaani kupigana Na jummanne alhamisi na jumamosi ni Taolu yaani mafunzo ya kimsingi. Kong Fu ni sanaa ya kitamaduni ya China ambayo ilianzishwa na mababu zetu na naipenda sana na pia napenda kujifunza"

    Mbali na mafunzo ya Kong Fu pia Kuna masomo ya kawaida kama tu shule zingine.

    Hii ni mojawepo ya shule kubwa zaidi inayotoa mafunzo ya Kong Fu hapa nchini China ikiwa na zaidi ya wanafunzi elfu 30, 000, ambapo iko karibu na hekalu la Shaolin ambalo kwa zaidi ya miaka 1,000 limekuwa mchambuko wa Kong fu.

    Kwenye awamu moja ya mazoezi kunaweza kuwa na zaidi ya makundi 30 ya wanafunzi mia moja wakifanya mazoezi ya Kong Fu.

    Bwana Wang Shuangli mwanzoni alisomea kwenye shule hii ya Tangou na sasa amerejea kupitisha ustadi wa sanaa hii kwa kizazi cha sasa kupitia mafunzo anayotoa hapa.

    "Kwa mafano watoto tunawafunza mambo ya msingi lakini kwa wale wa umri wa miaka 16 hivi tunawafunza Kong fu ya hali ya juu kama sanda..Pia tuna idara ya kupokea wanafunzi wageni kwenye shule yetu na sasa kuna wanafunzi wengi kutoka nje lakini sijui wanatoka nchi gani."

    Siku za nyuma vikundi vya wushu kutoka Afrika na duniani kote vimetbelea hapa ili kujifunza zaidi sanaa ya Kong fu.

    Sehemu hii ya Deng Feng ni maarufu sana kwa Kong fu nchini China na kwa miaka mingi imetoa wasanii watajika waliowakilisha nchi ama kuburudisha kwenye hafla kubwa kama vile ufunguzi wa mashindano ya olimpiki mwaka wa 2008.

    Mzee Liu Bao Shan ambaye sasa ana miaka ya 84 ndiye aliyeanzisha shule hii ya Tangou na kabla ya hapo watu walipata mafunzo tu kwenye hekalu la Shaolin.

    "Serikali ilifahamu kwamba mimi najua sana Kong fu na hivyo kunitaka nianze kuifunza. Mwazoni kulikuwa na wanafunzi wawili au watatu hivi na -sikudhani kama kutakuwa na wanafunzi wengi kiasi hiki . Wakati watoto wangu walipomaliza masomo ya chuo kikuu walirejea hapa kuendelea kuendesha shule na wao pia walianza kujifunza kong fu wakiwa bado wadogo"

    Kong Fu inahitaji nguvu, nidhamu na kujitolea na inachukuliwa kuwa ni sanaa ya kiume.

    Lakini licha ya kuwa kuna idadi kubwa ya wavulana wanaojifunza Kong –fu pia wasichana wamejkakamua kuingia kwenye sanaa hii.

    "Sidhani ati kwamba Kong fu ni ya wanaume. Inaweza kuendelezwa kwa njia mbali mbali na naipenda kwa moyo wangu wote. Baada ya kujifunza Kong Fu tunaweza kushiriki kwenye mashindano na kupata cheti cha kuonyesha uwezo wako na hiyo inaweza kusaidia kupata ajira. "

    Licha ya kwamba Kong Fu ni sanaa yenye ishara za vita wasanii wote wana nidhamu ya hali ya juu na wanatumia mchezo huu kama njia tu ya kujenga afya na kujilinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako