• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mipango Henan ya kushiriki Ukanda mmoja na njia moja

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:40:49

    Mkoa wa Henan ulioko katikati mwa China uko mbioni kuanzisha miradi ya miundo mbinu ili kuunganisha mipango yao na mvumo wa taifa wa ukanda mmoja na njia moja ulioanzishwa mwaka jana na Rais Xi Jingping wa China.

    Mipango hiyo ni kama kujenga uwanja wa ndege reli na wilaya mpya ya kisasa.

    Ronald Muitie anaripoti.


    Ukiwa na zaidi ya watu milioni mia moja mkoa wa Henan uko katikati mwa china.

    Kutokuwepo na bahari kwenye mkoa huu, kunaukata na uwezerkano wa kusafirisha bidhaa kwa njia ya bahari kufika kwenye nchi zilizko kwenye njia ya Hariri ya baharirni liliopendekezwa na Rais Xi Jing Ping wa China mwaka jana.

    Licha ya kuwa na viwanda vya kutengeneza bidhaa kama vile elektroniki, nguo na fenicha, gharama ya kuzisafirisha nje ni kubwa kutokana na iliopo Henan kijiografia.

    Lakini licha ya kutokuwa na bahari, mamlaka za mji mkuu wa mkoa wa Henan, Zheng Zhou zimeweka mipango kadhaa ya kuhakikisha biashara inafanyika kwa urahisi.

    Hiyo ni kutokana na wito serikali kuu wa kuzitaka sehemu mbalimbali kutumia uwezo wao kuunganisha mipango yao na mpango wa mzima wa taifa wa ukanda mmoja na njia moja. Bwana Xue Yunwei ni naibu meya wa mji mkuu wa Henan-Zheng Zhou, Anasema

    "Chini ya mpango wa ukanda mmoja na njia moja tunapanga kujenga mji wa Zheng Zhou kuwa kituo cha usafirishaji cha reli na ndege hivyo tumejenga uwanja mpya wa ndege na reli inayounganisha China na ulaya. "

    Hata hivyo kuna tatizo lingine la ndani.

    Mji wa Zheng Zhou una karibu watu milioni 10.

    Msongamano wa magari barabarani ni mkubwa na maeneo mengi bado hayajapangwa vizuri.

    Hali hii inapunguza uwezekano wa kuvutia wawekezaji na kampuni za kimataifa.

    Kutokana na hali hiyo sasa mamlaka imetenga wilaya mpya ambapo watafanya ujezi wa kisasa ndani ya mji wa Zheng Zhou.

    Bwana Wang Wanpeng ni katibu wa wilaya mpya ya Zhong Yuan.

    "Tunajenga eneo jipya la maendeleo ili kupata maendeleo ya jumla ya mji wetu na kuvutia wawekezaji kutoka nje tumepanga kutoa huduma bora zaidi kwa makampuni ya nje katika sekta mbalimbali za maisha na kuzisaidia kuanza biashara pindi tu wanapofika"

    Wazo la njia moja na Ukanda mmoja liliotolewa na rais Xi Jinping wa China mwaka 2013, linasisitiza kuwa China na nchi husika ni zenye hatma moja na hivyo zinatakiwa kuwa na ushirikiano wa kunufaishana na ustawi wa pamoja kimaendeleo. Meya Xue anasema.

    "Uwezo wa China wa kiviwanda ni mkubwa na kwa hivyo China inafaa kugawa uwezo huu kwa nchi zinazozunguka nchi za njia moja- ukanda mmoja"

    Lakini pia inafahamika kuwa mahitaji na uwezo wa kila nchi kushiriki biashara kupitia kwa njia ya moja na ukanda mmoja ni tofauti.

    Nchi za Afrika kwa mfano hazina viwanda vingi na hivyo zinaweza kuuza kwa biadhaa za kilimon na madini ambazo zinazalishwa kwa wingi barani humo. Lakini miji kama Zheng Zhou kulingana na Meya Xue imetafiti na kutambua maeneo ya ushirikiano barani Afrika.

    "Kenya ni nchi yenye raslimali nyingi za utalii na hiyo ndio fursa ya kushirikiana zaidi ili kunufaishana kati yetu"

    Takwimu za wizara ya biashara ya China, zinaonyesha kuwa thamani ya biashara kati ya China na nchi zilizoko kwenye ukanda wa kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri ya baharini ya karne ya 21, imefikia dola za kimarekani bilioni 236 katika robo ya kwanza ya mwaka huu huku kukiwa na zaidi ya maeneo 70 ya ushirikiano yanayojengwa kwenye nchi zilizoko kwenye Ukanda mmoja na Njia moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako