• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Athari za usasa leo zaua Oprah ya Henan

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:41:58

    Mkoani Henan katikati mwa China, sanaa ya Oprah ilikuwa maarufu sana aghalau hadi miaka ya 90.

    Lakini kadri kizazi cha wazee kilipoendelea kuisha ndivyo ulivyopungua sanaa hiyo huku vijana sasa wakiishia kufuata mitindo ya kisasa.

    Katika juhudi za kuweka hai sanaa hiyo Redio ya Zhenh Zhou ambayo yako mji mkuu wa mkoa wa Henan imeanzisha jumba la makumbusho kuhifadhi oprah ya Henan.

    Ronald Mutie anaripoti.


    Nyimbo kama hizi zilienziwa sana miaka ya 80 hapa mkoani Henan.

    Ziliwakilisha utamaduni, uzalendo , na heshima kwa wazee.

    Lakini kutokana na athari ya teknolojia, usasa leo na wasanii kuchukua muziki kama biashara, sauti hizi zimepungua sana.

    Sio tofauti na maeneo mengine duniani, ambapo miziki ya jadi imeendelea kudidimia.

    Wazee nao wakiendelea kuhuzunishwa na muziki huu wa kizazi kipya ulikosa maadili. Enzi hizo bi Chen Xiao Xiang alikuwa mdogo lakini mama yake alikuwa ni hodari wa Oprah. Alisema, hapa mkoani Henan Oprah ilitambuka sana haswa miaka kuasisiswa kuwa jamuhuri .

    "Mama yangu alipoimba kila mtu alishangilia, alipolia pia mashabiki walilia na yeye na nililelewa kwenye mazingira ya aina hii"

    Lakini sasa hana tena Raha.

    "Vijana wanapokea kwa haraka mambo ya kigeni, kama tu vile mjukuu wangu alipokuwa kuwa na umri wa miaka 5 aliweza kuimba vizuri oprah lakini sasa anapenda tu kuimba nyimbo za Korea kama tunakata kuendelea kuhifadhi tamaduni zetu za Oprah lazima tuanze kuwafunza watoto wakiwa la sivyo vijana wetu watakuwa mbali sana na sanaa zetu za jadi"

    Licha ya Kuwa Oprah ya henan inadidimia, pia Kuna matumaini.

    Shen Ping mwenye umri wa makamo ni mmoja wa wasanii wa Oprah.

    Yeye ni kizazi kipya na anaishi kwenye mazingira magumu ya hip hop ambapo ni rahisi kushawishika na kusahahu utamaduni wa Oprah ya Henan.

    "Mwanzoni sikuipenda hata kidogo, nilijifunza maneno matatu tu kwa wiki moja lakini sasa naipenda na ni kama tegemeo langu la kila siku maishani na sijali kama watu wa kizazi hiki watajiunga na mimi au la nitaendelea bila kusita ama kujali"

    Juhudi za Shen Ping zimepata nguvu mpya.

    Mwaka Jana Redio ya Zheng Zhou ilifungua jumba la makumbusho kuhifadhi utamaduni wa Oprah ya Henan.

    Kwenye jumba hili kuna ala za jadi za Oprah, mavazi na maandishi.

    Wapenzi wa Oprah kama Shen Ping wanaweza kufanya utafiti kwenye jumba hili jinsi ya kuboresha uimbaji wao.

    Na wasomi wengi pia hawachagui kutafiti utamaduni wa Oprah kama taaluma zao.

    Lakini Meng Ren ambaye anasomea Phd marekani aliamua kuchukua somo la kutafiti na kuhifadhi muziki.

    Lengo lake likiwa ni kuhimiza utunzaji wa utamaduni hususan Oprah ya Henan.

    "unapotaka kufahamu watu zaidi mojawepo wa vitu vya kujifunza ni utamadini, na kwa hivyo nadhani muziki ni sehemu muhimu ya utamaduni n asana sana opra ambayo inajumuisha fasihi, historian a filosofia ya wachina. Oprah inadidimia kwa sababu hatujawekeza mambo mengi ndani yake kwa kuhifadhi vitu kama maandishi pia mvumo wetu wa elimu hauna masomo mengi ya sanaa. Nadhani cha muhimu sio kufunza sana kuhusu mambo kama treni ya kasi ama uwanja wa birdnest kwa sababu mambo hayo hayasaidii wachina kufahamu utamaduni"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako