• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukurasa wa Kwanza

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:48:25
    Kila mtu ana mji anaoupenda.

    Mji wa Zhengzhou ulioko katikati ya China, ni mji mkuu wa mkoa wa Henan. Mji huo ulioko kando ya mto Manjano ambao ni mto mama wa China, uko mashariki mwa mlima Songshan, maarufu na wenye hadhi muhimu kiutamaduni kwa China.

    Tarehe 1 Agosti mwaka 2010, mkutano wa 34 wa urithi wa dunia uliofanyika huko Brasilia, Brazil, ulitangaza kuorodhesha rasmi kundi la majengo ya kihistoria linaloitwa "Katikati ya mbingu na ardhi"(The Center of Heaven and Earth) kuwa sehemu ya Urithi wa utamaduni wa dunia. Kwa mujibu wa fikra za kale za wachina kuhusu ulimwengu, China ni nchi iliyoko katikati ya mbingu na ardhi, na mji wa Zhengzhou uko katikati ya mbingu na ardhi, ndiyo maana mji wa Zhengzhou ulichaguliwa kuwa mji mkuu wa enzi za kifalme za kale. Mji huu pia ni chimbuko la ustaarabu wa China na kituo cha mkusanyiko wa tamaduni za China.

    Historia ya mji huu mkongwe.

    Katika karne ya 21KK, Enzi ya kifalme ya Xia ilianzishwa huko Zhengzhou na kuwa dola ya kwanza kuunganisha China nzima, na kufungua ukurasa wa zama za ustaarabu wa kitaifa wa China. Katika miaka 3,600 iliyopita, Enzi ya kifalme ya Shang ilichagua mji wa Zhengzhou kuwa mji mkuu wake na kufanya ustaarabu wa Shaba nyeusi wa China ufikie kilele. Katika enzi ya madola ya kivita ya Zhou, madola mbalimbali kwa nyakati tofauti yaliuchagua mji wa Zhengzhou kuwa mji mkuu wao, na kuifanya Zhengzhou iwe mji tajiri na maarufu. Historia hizo zote zinaonesha wazi duniani uvumbuzi mkubwa wa wenyeji wa Zhengzhou wa wakati huo, na kuthibitisha nafasi muhimu ya Zhengzhou katika maendeleo ya ustaarabu wa taifa la China. Kutokana na manufaa ya kijiografia ya kuwa katikati ya China, Zhengzhou siku zote ni kituo muhimu cha mawasiliano ya kiutamaduni nchini China. Katika mazingira yanayojumuisha tamaduni kutoka sehemu mbalimbali za China, mji wa Zhengzhou uliotesha falsafa asili za kichina, ambazo ni minara mikubwa katika utamaduni wa China.

    Maendeleo ya mambo ya kisasa.

    Katika miaka 100 iliyopita, mji wa Zhengzhou ulianza kubadilika na kupiga hatua ya kuwa mji wa kisasa. Mwanzoni mwa karne ya 20, baada ya kukamilika kwa njia mbili kuu za reli a Kaskazini-kusini na magharibi-mashariki ambazo zinakutana mjini Zhengzhou, kuliufanya mji huo uwe kituo muhimu cha mawasiliano na uchukuzi nchini China, kwa hiyo Zhengzhou pia unajulikana kama "Mji uliotokana na shughuli za treni".

    Hivi leo katika juhudi za kuendeleza Ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri, mji wa Zhengzhou unaendelea kuimarisha hadhi yake katika sekta ya uchukuzi nchini China, ukizindua eneo la kwanza la majaribio la kiuchumi la uwanja wa ndege nchini China na kujijenga kuwa kituo cha ugavi cha kimataifa. Vilevile, kufunguliwa kwa safari za treni za mizigo kutoka Zhenghai hadi Ulaya kumeunganisha sekta ya biashara kati ya pande hizo mbili. Wenyeji wa Zhengzhou pia wanajitahidi kuendeleza uchumi wa mji huo na sekta nyingine, hasa utengenezaji magari, chakula barafu na nguo. Aidha, Soko la kubadilishana bidhaa la Zhengzhou na masoko ya mauzo ya jumla mjini humo vimeonesha nguvu kubwa ya ushawishi nchini China.

    Zhengzhou, ambao ni mji mkongwe zaidi duniani, sasa uko mbioni kujitokeza upya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako