• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zhengzhou---Mji uwenye vivutio vingi vya kiutamaduni

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:49:10
    Kwenye sehemu ya chini ya mto mama wa taifa la China Mto Manjano, uko mji mmoja mkongwe na pia wa kisasa Zhengzhou, mji mkuu wa mkoa wa Henan.

    Mji wa Zhengzhou una historia ndefu na raslimali nyingi za kiutamaduni, na zamani uliwahi kuwa kiini cha siasa, uchumi na utamaduni wa taifa la China kwa kipindi kirefu. Mji huo ni chimbuko la tamaduni mbalimbali kama utamaduni wa Peiligang wenye historia ya miaka 8,000, utamaduni wa kijiji cha Dahe wenye historia ya miaka 6,000, utamaduni wa mfalme Huangdi wenye historia ya miaka 5,000, na utamaduni wa enzi ya Xia wenye historia ya miaka 4,000. Mji huu pia umetoa watu wengi mashuhuri katika historia, kama vile mfalme mkubwa Huangdi, mwanafikra maarufu Zi Chan, mwanafalsafa mashuhuri Han Fei, washairi maarufu Du Fu na Bai Juyi na msanifu mashuhuri wa majengo Li Jie. Historia ndefu huhifadhi ustaarabu mkubwa, Zhengzhou ina maeneo 10,315 ya mabaki ya kale, 74 kati yao ni ya ngazi ya uhifadhi wa kitaifa.

    Mjini Zhengzhou kuna sehemu zaidi ya mia moja zenye vivutio vya utalii, na katika miaka ya karibuni sekta ya utalii imepiga hatua kubwa kwa kasi.

    Wachina husema "Kongfu ya kichina ni bingwa duniani, na Kongfu zote zinaanzia hekalu la Shaolin." Hekalu maarufu la Shaolin limekuwa chaguo la kwanza kwa mashabiki wa Kongfu kote duniani. Maonesho makubwa ya "Shaolin Zen Music Ritual" yanayofanyika kwenye mazingira halisi ya mlima Songshan yameonesha mchanganyiko na uwiano kati ya muziki na maumbile.

    Mfalme Huangdi ni mwanzilishi mmojawapo wa ustaarabu wa Kichina. Zhengzhou, ukiwa ni mji ambao mfalme Huangdi alizaliwa, kuanzisha utawala wake na kujenga mji mkuu, kila mwaka mji huo hufanya sherehe kubwa ya kumwabudu mfalme huyo ambayo inavutia wachina wengi kuja kutoa heshima kwa mababu wao wa kale.

    Zhengzhou ni mpaka wa sehemu ya kati na ya chini ya mto Manjano, ambao ni chimbuko la ustaarabu wa China.

    Zhengzhou ulikuwa mji mkuu mkubwa zaidi na uliojengwa mapema zaidi wakati wa enzi ya Shang iliyoanzia mwaka 1600 K.K., na pia ulikuwa mji mkuu wa kwanza uliojengewa ukuta wa kuzunguka mji katika historia ya China. Mpaka leo, mabaki ya mji mkuu huo yenye historia zaidi ya miaka 3,000 bado yanahifadhiwa katikati ya mji wa Zhengzhou.

    Baada ya kupitia historia yenye ustawi na majanga, Zhengzhou ya sasa imejitokeza kuwa mji mkubwa wa kisasa wenye vivutio vingi vya utalii.

    Karibu Zhengzhou!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako