• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zhengzhou, mji uliojaa upendo

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:50:00
    William Shakespeare aliwahi kusema, hisani ni alama halisi ya uungwana.

    Mjini Zhengzhou, moyo wa hisani unaenea kila mahali.

    Mwezi Novemba mwaka 2013, kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa, mzee Hans kutoka Uswis aliimba kwa furaha wakati aliposherehekea miaka 80 tangu kuzaliwa kwake, na hii ilikuwa ni mara yake ya sita kusherehekea siku hiyo mjini Zhengzhou. Pamoja naye ni familia moja ya wachina, mwenyeji wake, Song Yang ni mzaliwa wa Zhengzhou. Mwaka 1999, Bw. Song Yang alipokwenda kusoma nchini Uingereza, alipanga kwenye nyumba ya mzee Hans, ambaye wakati huo alikuwa na miaka 66 na kuishi peke yake. Watu hao ambao umri wao unatofautiana kwa miaka 47, rangi tofauti ya ngozi, uraia tofauti na utamaduni tofauti, walianza kuishi pamoja kama familia. Kuanzia hapo, Bw. Song Yang alitoa ahadi hii kwa mzee Hans "Najua mzee Hans hana jamaa, nitaendelea kuwa pamoja naye na kumtunza, ili aweze kuishi maisha ya furaha uzeeni." Baada ya miaka 8, Bw. Song Yang akarudi nchini China pamoja na mzee Hans. Mzee Hans aliishi kwa furaha mjini Zhengzhou kwa miaka 6 kabla ya kufariki dunia kutokana na tatizo la moyo. Wahenga husema "ahadi ni deni", ahadi ya Bw. Song Yang iliyotekelezwa kwa miaka 14, inasifiwa sana katika jamii.

    Mwanzoni mwa mwaka 2013, pia mjini Zhengzhou, mmiliki mmoja wa mkahawa wa tambi aliyepatwa na ugonjwa wa saratani hakutaka kupokea misaada ya bila malipo, badala yake akatoa mwito wa "Kula tambi katika mkahawa wangu", ambao ulipokewa na wakazi wengi mjini Zhengzhou. Watu wengi wa mji huo walienda kwa hiari kwenye mkahawa wake na kuonesha upendo na hisani kwa njia yenye heshima ya kula tambi alizoandaa.

    Bw. Li Zhongmin mwenye umri wa miaka 47 anayeishi pembezoni mwa mji wa Zhengzhou, alipooza sehemu ya chini ya mwili wake, hivyo kushindwa kumhudumia binti yake ambaye bado ni mdogo. Kwa familia hiyo yenye mikosi, mwalimu Fang Guoxin na wanafunzi wake wa chuo cha sayansi na teknolojia cha Zhengzhou kilichoko karibu wanamhudumia Bw. Li Zhongmin kama ndugu wa karibu kwa miaka 15. Huu ni mfano mmoja tu. Mjini Zhengzhou pia kuna jumuiya ya makazi ya Longhai iliyojitolea kumwangalia Bw. Gao Xinhai ambaye alipatwa na kiharusi, Daktari Hu Peilan aliyeendelea kutoa huduma za matibabu kila siku kwa miaka 20 baada ya kustaafu, pamoja na watu wanaojitolea kutoa huduma mbalimbali kote mjini Zhengzhou kila ifikapo wikiendi, kazi walizofanya huenda ni ndogo, lakini zinagusa moyo wa kila mtu mjini humo.

    Zhengzhou, ndio ni mji kama huu ambao umejaa upendo na kutunza kila mtu anayeishi mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako