• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usafiri wa ndege mjini Zhengzhou

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:51:21
    Usafiri wa ndege unafanya miji iwe karibu zaidi na sehemu nyingine duniani, kwa hiyo miji mingi duniani ina ndoto ya kuendeleza usafiri wa ndege.

    Mwaka 2013, eneo la kwanza la majaribio ya kiuchumi la kituo cha usafiri wa ndege la China lilizinduliwa mjini Zhengzhou. Eneo hilo linawanufaisha wakazi wa sehemu ya katikati ya China. Mwezi Aprili mwaka huu, kituo cha biashara ya kimataifa ya mvinyo kilizinduliwa katika eneo hilo, na baadaye tarehe 13 Mei ndege iliyobeba maembe na mafenesi ya Thailand ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Zhengzhou, na kuonesha uwezo mkubwa wa mawasiliano ya uwanja huo.

    Eneo la majaribio ya kiuchumi la kituo cha usafiri wa ndege la Zhengzhou liko kilomita 20 kusini mashariki mwa katikati ya mji huo, ukubwa wake ni kilomita 415 za mraba. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zhengzhou pia uko katika eneo hilo, ambao una safari 185 za ndege zinazokwenda miji 97. Uwanja huo pia una safari 32 za ndege za mizigo, na 28 kati ya hizi ni safari za kimataifa.

    Mwezi Oktoba, mwaka 2012, kampuni ya usafirishaji wa mzigo UPS ilizindua safari yake ya kwanza kutoka Zhengzhou kwenda Anchorage, Marekani kupita Incheon, Korea Kusini. Safari hiyo inapunguza muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka Zhengzhou kwenda Anchorage kutoka zaidi ya saa 50 hadi saa 14. Zhengzhou imekuwa kituo cha 5 cha Kampuni ya UPS nchini China baada ya Shanghai, Shenzhen, Chengdu na Qingdao.

    Thamani ya jumla ya biashara katika eneo hilo kwa mwaka ilifikia dola za kimarekani bilioni 37.9 mwaka jana, ambayo imeongezeka kutoka chini ya dola za kimarekani milioni 100 za mwaka 2010. Thamani hiyo inachukua zaidi ya nusu ya thamani ya jumla ya biashara na nje ya mkoa wa Henan.

    Utengenezaji wa smartphone mjini Zhengzhou umefikia karibu milioni 100 kila mwaka, na kila moja kati ya smartphone 8 zinazouzwa duniani, imetengenezwa mjini Zhengzhou. Hali hii inatokana na uwezo mkubwa wa usafirishaji wa mizigo kwa ndege.

    Mji huo pia una makampuni mengi ya biashara ya mtandao wa Internet, na hii ndio sababu kuu ya mji huo kuendeleza biashara ya mtandao wa Internet. Biashara hiyo ya kimataifa ya mtandao wa Internet inasaidia ukusanyaji wa kasi wa mizigo, na kasi ya usafirishaji na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo, ambayo ni njia ya kuunganisha China na dunia nzima.

    Mwaka huu miradi 21 ya usafirishaji wa mizigo, miradi miwili ya utengenezaji vifaa wa ngazi ya juu na miradi 46 ya huduma za kisasa itaingia katika eneo hilo, ujenzi wa miundo mbinu na huduma za umma kama vile awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege na awamu ya tatu ya ujenzi wa eneo la majaribio ya kiuchumi la kituo cha usafiri wa ndege la Zhengzhou unaendelea. Mji wa Zhengzhou unajiendeleza kuwa mji wa kisasa ambao uchumi wake unategemea sekta ya usafari wa ndege.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako