• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji unaojitokeza kwa viwanda na biashara

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:51:52
    Zhengzhou, mji mkuu wa mkoa wa Henan, ulioko katikati ya China, kusini mwa mto Manjano na mashariki mwa mlima Songshan, inapakana na miji mikongwe ya Kaifeng na Luoyang.

    Zhengzhou ikiwa ni mji muhimu wa viwanda kwenye sehemu ya katikati ya China, sekta yake ya viwanda ni pamoja na viwanda vya magari, utengenezaji wa vifaa, upashanaji habari, vyakula, vitambaa na nguo. Kampuni kubwa zaidi ya utengenezaji wa mabasi ya abiria duniani - kampuni ya Yutong ipo mjini Zhengzhou, na hali kadhalika kiwanda kikubwa zaidi cha chakula barafu nchini China - Kampuni ya chakula ya Sanquan. Hivi sasa, moja kati ya simu sita za mikononi za Iphone zinazouzwa duniani inatengenezwa huko Zhengzhou. Kiwanda kilichojengwa na kampuni ya Foxcom mjini Zhengzhou kimeharakisha hatua ya maendeleo ya viwanda vya upashanaji habari. Ujio wa Kampuni ya vifaa vya umeme ya Gree na Kampuni ya utengenezaji wa magari ya Haima pia umesukuma mbele maendeleo ya viwanda vya kisasa mjini Zhengzhou. Hivi sasa, mji wa Zhengzhou una kampuni 11 zenye mapato yanayozidi dola bilioni 1.6 za kimarekani kila mwaka, na moja yenye mapato yanayozidi dola bilioni 16 za kimarekani kwa mwaka. Mji huo pia una kampuni 37 zinazoorodheshwa kwenye soko la hisa, kampuni 84 kati ya kampuni bora 500 duniani zimewekeza au kufungua matawi mjini humo.

    Zhengzhou pia ni mji wa biashara unaojulikana sana hapa China. Soko la kubadilishana bidhaa la Zhengzhou ni la kwanza la bidhaa zinazokabidhiwa siku za baadaye (Futures market) nchini China, "Bei ya Zhengzhou" siku zote ni bei inayoelekeza utengenezaji na biashara ya nafaka duniani. Urahisi wa mawasiliano na hali bora ya kijiografia zinahimiza maendeleo ya kasi ya sekta ya maonesho mjini humo. Zhengzhou inasifika kama mji mwenyeji wa maonesho mbalimbali kwenye sehemu ya kati ya China, ambapo kila mwaka maonesha mia kadhaa hufanyika mjini humo. Maingiliano kati ya sekta ya maonesho na sekta nyingine husika mjini humo yameongeza zaidi nguvu ya ushindani ya viwanda vya Zhengzhou. Eneo la biashara huria la Xinzheng mjini Zhengzhou ni eneo la kwanza la biashara huria lililoko katikati ya China, na eneo la majaribio la biashara huria la uwanja wa ndege la Zhengzhou ni la kwanza la maendeleo ya kiuchumi la uwanja wa ndege ambalo linachukuliwa kuwa sehemu ya mkakati wa kitaifa.

    Mji wa Zhengzhou unatarajiwa kupiga hatua kubwa zaidi katika siku za baadae.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako