• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safari ya treni ya mizigo kati ya Zhengzhou na Ulaya

    (GMT+08:00) 2015-08-10 19:53:41

    Si jambo geni kwa China na Ulaya kuzindua treni ya mizigo ya moja kwa moja. Safari ya treni ya mizigo kati ya Zhengzhou na Ulaya si ya kwanza katika historia ya China, lakini baada ya kuzinduliwa kwake, imeonesha mwelekeo mzuri wa maendeleo. Safari ya kimataifa ya treni ya mizigo kutoka Zhengzhou hadi Ulaya ilizinduliwa tarehe 19 Julai, mwaka 2013. Safari hii yenye umbali wa kilomita 10,214 inaanzia Zhengzhou na kuvuka mpaka wa nchi kupitia forodha ya Alataw mkoani Xinjiang, kisha inapita Kazakhstan, Russia, Belarus, Poland na mwishoni kufika Hamburg, Ujerumani. Safari hiyo kati ya Zhengzhou na Ulaya inasifiwa na Wajerumani kuwa ni "kichwa cha treni kinachovuta dunia", na Chiris Fanter ambaye ni naibu menaja wa kituo cha uchukuzi wa shehena cha Billwerder mjini Hamburg amesema "safari hiyo imebeba matarajio mengi ya biashara kati ya Asia na Ulaya, na ujio wake ni tukio kubwa kwa Hamburg." Kutoka uingizaji wa magari hadi uuzaji nje wa mazao ya kilimo, kutoka safari moja kila mwezi hadi safari mbili kwa wiki, kutoka safari ya kwanza ya kupeleka bia ya Ujerumani mjini Zhengzhou hadi safari ya kwanza ya kusafirisha shehena ya friza nje ya nchi, safari ya treni kati ya Zhengzhou na Ulaya imefungua mlango wa mawasiliano ya kibiashara kati ya pande hizo mbili, na kuifanya sekta ya usafirishaji wa bidhaa zinanahifadhiwa kwenye ubaridi kwa treni ya Zhengzhou iingie kwenye soko la kimataifaMafanikio ya safari ya treni kati ya Zhengzhou na Ulaya yamevutia ufuatiliaji mwingi. Kongamano la kimataifa la ujenzi wa kitovu cha uchukuzi kati ya China na Ulaya katika Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri lilifanyika tarehe 28 Novemba mwaka jana mjini Zhengzhou, ambapo aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jin Yongjian amesema "kutokana na kuongezeka kwa maingiliano, China na Ulaya zimepanua wigo la mikakati yao, na kama pande hizo mbili zenye nguvu kubwa ya kiuchumi zitafanya kazi kwa pamoja, nchi na sehemu zilizopo kwenye njia ya hariri zitanufaika moja kwa moja na ustawi unaotokana na biashara na uwekezaji." Pia wasimamizi wa kampuni za treni kutoka Russia, Belarus na Kazakhstan walitoa mapendekezo yao kuhusu kurahisisha uchukuzi na biashara katika Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri. Naibu mwenyekiti wa kampuni ya treni ya Russia amesema "Zhengzhou ina hali bora ya kijiografia, tuna hamu kubwa ya kufanya ushirikiano na China, na tunapanga kuongeza idadi ya mizigo inayosafirishwa kati ya nchi hizo mbili mwaka 2015."

    Kutoka tairi, pazia, meza na viti vya ofisini hadi vipuri vya roboti, laptop na vifaa vya kupokea data za satelaiti, "bidhaa zinazotengenezwa China" zinapelekwa kwa wingi hadi nchi zilizo katika njia mpya ya Hariri. Safari ya treni kati ya Zhengzhou na Ulaya imekuwa daraja muhimu linalounganisha kiuchumi pande mbili za Mashariki na Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako