Tarehe 14, April, Baraza la Serikali la China liliidhinisha Mpango wa Eneo la Uchumi wa Ikolojia la Ziwa Dongting, ikiwa ni hatua ya kufanya maendeleo ya eneo la Ziwa Dongting kuwa mkakati wa kitaifa. Sehemu zinazojumuishwa kwenye Eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba elfu 60.5 ni pamoja na miji mitatu ya Yueyang, Changde, na Yiyang na wilaya ya Wangchen mjini Changsha, mkoani Hunan, pamoja na mji wa Jingzhou, mkoani Hubei.
Katika mchakato wa kujenga jamii yenye ustawi kwa pande zote nchini China, lengo la eneo la Ziwa Dongting ni kujenga eneo la uchumi lenye mandhari nzuri, na kuanzisha eneo la majaribio la ujenzi wa ustaarabu wa mazingira la bonde la ziwa lenye jukumu la kulinda usalama wa mazingira, maji na chakula katika bonde la Mto Yangtse.
Lakini mazingira mazuri ya Ziwa Dongting yaliharibika kutokana na maendeleo ya kiviwanda na upanuzi wa miji. Katika majira ya joto ya mwaka 2011, ukame uliodumu kwa miezi mitatu ulifanya kina cha maji kwenye Ziwa hilo kiwe chini zaidi katika historia, eneo la Ziwa hilo limepungua, maji yalichafuliwa na mazingira yalizidi kuwa mabaya, na sehemu ya Ziwa ikageuka na kuwa mbuga, jambo ambalo limepiga kengele ya hatari.
Mwaka 2013, takwimu zilizotolewa kwenye utafiti kuhusu kiwango cha ustawi katika miji mitatu ya Yueyang, Changde na Yiyang zinaonesha kuwa, Yueyang ni asilimia 86.8, Changde 87.56 na Yiyang 80.1. Hata hivyo uwezo wa uvumilivu wa ikolojia umepungua na nguvu za kuleta maendeleo mapya hazitoshi. Je, eneo la Ziwa Dongting litachukua hatua gani kukabiliana na changamoto hizo wakati inapolinda na kurudisha mazingira ya ikolojia na pia kukuza maendeleo? Fuatana nasi katika makala maalum kuhusu Eneo la uchumi wa Ikolojia kwenye Ziwa Dongting kuanzia tarehe 14 Septemba
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |