• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziwa Dongting

    (GMT+08:00) 2015-09-10 19:53:17

    Ziwa Dongting ni ziwa kubwa lenye kina kifupi lililoko kaskazini mashariki mwa mkoa wa Hunan, hapa China, na ni bwawa ambalo maji kutoka mto Yangtze hutiririka, hivyo ukubwa wa ziwa hilo hutegemeana na msimu.

    Ziwa Dongting ni maarufu sana kwenye utamaduni wa China, ikiwa ni chimbuko la mashindano ya boti maarufu kama Dragon boat race, pia kisiwa cha Junshan kinapatikana kwenye ziwa hilo, na ni makazi ya Pomboo wasio na pezi, ambao ni samaki walio kwenye hatari ya kutoweka nchini China.

    Eneo hilo linajulikana sana kwenye historia ya China na pia kwenye fasihi. Maana halisi ya "Dongting" ni 'Eneo la Pango', na jina la ziwa hilo lilitokana na pango kubwa ambalo linaaminika kuwepo chini ya ziwa hilo, ambako roho za wake wa mfalme Shun, Ehuang na Nuying zinaaminika kuwa wasimamizi wa pango hilo. Inasemekana kuwa mashindano ya boti za Dragon yalianza kwenye pwani ya mashariki ya Ziwa Dongting ikiwa ni sehemu ya kazi ya kutafuta mwili wa mshairi maarufu wa Chu, aitwaye Chu Yuan, mwaka 340-278 BC, na mfalme wa dragon anayeaminika kuishi chini ya ziwa hilo.

    Kisiwa cha Junshan nacho kimepewa jina la wake wa kiungu wa Shun, ambaye aliishi hapo baada ya kufa maji, ambako waliutafuta mwili wake kutoka chanzo cha mto Xiang ambako alikufa maji, mpaka sehemu ya chini ambayo mwili huo ungeweza kupelekwa ndani ya mto. Kisiwa hiki ni maarufu kwa kuwa na vilele 72 katikati ya Ziwa, pia ni maarufu kwa chai yake maalum iitwayo Junshan Yinzhen. Sehemu ya chini ya Ziwa Dongting na maeneo yanayozunguka Ziwa hilo ni maarufu kwa mandhari nzuri ya kuvutia, ambayo imepata msemo maarufu, "Hunan ya Mito Xiao na Xiang".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako