• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya Rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa viongozi wa dunia kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

    (GMT+08:00) 2015-11-09 12:24:04

    Katibu Mkuu Ban Ki Moon

    Mkurugenzi Mtendaji Phumile Mlambo Ngcuka

    Wenzangu wote

    Mabibi na mabwana

    Marafiki

    Katika maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa mataifa, na maadhimisho ya miaka 20 ya mkutano wa nne kuhusu wanawake uliofanyika Beijing, ni muhimu kwa kuitisha mkutano wa viongozi wa dunia kuthibitisha ahadi zetu kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, na kuweka mipango kwa ajili ya siku nzuri za baadaye.

    Wanawake ni wazalishaji wa mali za kiroho na vitu, na ni nguvu muhimu ya kusukuma mbele maendeleo ya kijamii. Bila wanawake hakutakuwa na maendeleo ya binadamu na jamii yake. Kutafuta usawa wa kijinsia ni mkondo mkuu. Historia inatuonesha kuwa bila ukombozi na maendeleo ya wanawake, ukombozi na maendeleo ya binadamu hayawezi kupatikana. Tumepita njia ngumu Ili kufikia lengo la usawa wa kijinsia. Tangu azimio la haki za wanawake litolewe miaka 200 iliyopita, had siku ya kimataifa ya wanawake Machi 8, na kutoka ilipoanzishwa kamati ya Umoja wa mataifa ya kusimamia hadhi ya wanawake hadi kupitishwa kwa azimio kuondoa ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanawake, kila hatua imepigwa kuhimiza usawa wa wanawake imekuwa ni hatua kubwa kuelekea maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.

    Miaka 20 iliyopita mkutano wa nne wa wanawake ulifanyika mjini Beijing na kupitisha Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji, na kuweka malengo ya kimkakati na mpango wa sera kuhimiza usawa wa kijinsia na kuhakikisha haki za wanawake. Leo moyo uliohimizwa na mkutano wa Beijing umehimiza mabadiliko mazuri duniani. Makubaliano kati ya nchi mbalimbali duniani kuhusu kutafuta usawa wa kijinsia yanazidi kupata nguvu. Hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuhimiza maendeleo ya wanawake, na mazingira ya kijamii ya ubora wa maisha ya wanawake na maendeleo yao vinaendelea kuboreka. Kutokana na sababu hiyo wanawake wa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kupongezwa.

    Kutokana na juhudi thabiti za miaka kadhaa, ndoto ambazo zamani ilikuwa vigumu kuzitimiza sasa zinatimizwa. Nchi 143 zimeingiza usawa wa kijinsia kwenye sheria zao, na kuondoa vikwazo vya kisheria kwenye ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kisiasa na kiuchumi, na sasa kuna makubaliano ya jumla duniani kuwa wanawake wanatakiwa kupata elimu na ajira, na kujiamulia kuingia kwenye ndoa.

    Hata hivyo katika sehemu nyingi duniani, bado kuna tofauti, na bado hakuna usawa kati ya wanaume na wanawake kwenye upande wa haki, fursa na kupata raslimali. Bado uwezo, vipaji na mchango wa wanawake havijatambuliwa kikamilifu. Wanawake ni zaidi ya nusu ya watu milioni 800 wanaokabiliwa na umaskini duniani. Wanawake bado wanaendelea kuathiriwa zaidi na vita na magonjwa, na wanaathiriwa zaidi na ugaidi na vurugu. Hata tunavyoongea sasa, aina mbalimbali za ubaguzi dhidi ya wanawake unaendelea kufanyika. Vitendo vya ukatili na kutendewa vibaya bado vinaendelea. Yote haya yanayonesha kuwa bado tuna safari ndefu kufikia usawa wa kijinsia. Tunatakiwa kufanya kazi bila kuchoka kupanua matarajio ya kufanikisha kazi hii.

    Mabibi na Mabwana,

    Marafiki,

    Kwenye ajenda ya maendeleo ya milenia baada ya mwaka 2015 ambayo tumeipitisha, suala ya usawa wa kijinsia limewekwa katika kila kipengele. Tunatakiwa tusisitize moyo wa mkutano wa Beijing na utekelezaji mpya bila kupoteza muda katika kazi ya kuhimiza usawa wa kijinsia na maendeleo ya wanawake kwa pande zote.

    Kwanza, tunatakiwa kupigania maendeleo ya wanawake sambamba maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maendeleo hayawezi kupatikana bila wanawake, na manufaa yanayoletwa na maendeleo yanatakiwa kutumiwa pamoja. Tunatakiwa kutunga mikakati mizuri na inayojumuisha wengi na inayozingatia hali halisi ya kila nchi, tofauti za kijinsia, mahitaji maalum ya wanawake, na kulenga kuhakikisha wanawake wananufaika na matunda ya maendeleo. Hatua za kisera zinatakiwa kuboreshwa kila mara ili kuhimiza uwezo wa wanawake na ushiriki wao katika mchakato wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Uzoefu wa China unaonesha kuwa ushiriki wa kiwango kikubwa wa wanawake kwenye mambo ya kijamii na uchumi kunasaidia kuinua hadhi yao, na uzalishaji wao katika jamii na hata kuhimiza uchumi.

    Pili, tunatakiwa kulinda haki za wanawake na maslahi yao. Haki na maslahi ya wanawake ni haki za msingi za binadamu. Wanawake wanatakiwa kulindwa na sheria, na ulinzi huo unatakiwa kuingizwa kwenye taratibu za taratibu na desturi za taifa na jamii. Tunatakiwa tuunge mkonouwezo wa wanawake kutoa mchango kwa jamii na kwenye mambo ya uchumi, kuhimiza uwezo wa wanawake katika kufanya maamuzi, na kuwaunga mkono kuwa viongozi kwenye sekta za siasa, biashara na elimu. Tunatakiwa pia kuhakikisha kuwa huduma za msingi za afya kwa wanawake zinakuwa za kutosha, na hasa kufuatilia mahitaji ya afya ya wanawake wa vijijini, wanawake wenye ulemavu, wanwake wahamiaji, wanawake wenye umri wa kati na wazee, na wanawake wa makabila madogo. Tunatakiwa pia tuhakikishe kuwa gharama za shule zinakuwa nafuu na shule zinakuwa na usalama kwa kila msichana, na kuendeleza mafunzo ya ufundi kazi na elimu ya muda mrefu kwa wanawake ili kuwawezesha waendane na mabadiliko ya jamii na soko la ajira.

    Tatu, tunatakiwa kupigania kujenga jamii zenye masikiliano na shirikishi. Wanaume na wanawake wanatakiwa kuishi katika dunia moja. Jamii isiyo na ubaguzi dhidi ya wanwake kwa kawaida ni shirikishi na yenye kuendelea. Tunatakiwa tuondoea ukatili wa aina zote dhidi ya wanawake, ikiwa ni pamoja na ukatili wa nyumbani. Tunatakiwa kuangalia kwa makini usawa wa kijinsia na kuachana na mawazo yaliyopitwa na wakati na tamaduni zinazokwamisha maendeleo ya wanwake. Ninapongeza sana juhudi za katibu Mkuu Bw Ban Ki Moon za "Mvulana kwa ajili ya Msichana" na kutumani kuwa wanaume wengi watashiriki na kuchukua hatua.

    Nne, tunatakiwa kuhimiza mazingira ya dunia yanyofaa kwa maendeleo ya wanawake. Wanwake na wasichana ndio wanaoathirika zaidi amani na utulivu vinapovurugika. Tunatakiwa kupigania kidete amani, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana, kulinda amani kwa nguvu, na kuhakikisha kuwa kila mwanamke na mtoto anafurahia mwanga wa furaha na utulivi.\

    Mashirika ya wanawake katika nchi mbalimbali yanatakiwa kuimarisha mawasiliano kuhimiza urafiki kati yao, kupigania maendeleo, na kufikia maendeleo kwa pamoja. Tunatakiwa kuendelea na utekelezaji wa ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo unaonauhusu wanawake. Nchi zilizoendelea zinatakiwa kuongeza msaada wa kifedha na kiufundi kwa nchi zinazoendelea, na kupunguza pengo la maendeleokati ya wanawake kwenye nchi mbalimbali.

    Mabibi na mabwana,

    Marafiki,

    Wakati wachina wanapigania maisha ya furaha, kila mwanamke mchina ana fursa ya kufanikiwa kimaisha na kutimiza ndoto zake. China itafanya kazi zaidi kuhimiza usawa wa kijinsia katika sera yake ya msingi ya taifa, ili kuwawezesha wanawake kutoa mchango wao wa "nusu ya mbingu" na kuwaunga mkono kutimiza ndoto zao na matarajio yao kwenye kazi na katika maisha. Wanawake nchini China, kupitia maendeleo yao pia watatoa mchango mkubwa kwenye harakati za wanawake duniani na kutoa mchango mkubwa kwenye usawa wa kijinsia duniani.

    Ili kuunga mkono maendeleo ya wanawake duniani na kazi za Shirikisho la wanawake la Umoja wa mataifa, China itachangia dola milioni 10 za kimarekani kwa Shirika la wanawake la Umoja wa mataifa kwa ajili ya utekelezaji wa Azimio la Beijing na mpango wake wa utekelezaji na kitimizwa kwa maelngo yanayohusika ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Katika miaka mitano ijayo China itazisaidia nchi nyingine zinazoendelea kujenga miradi 100 ya "afya ya wanawake na watoto", kutuma vikundi vya wataalamu wa afya kutoa huduma, na kutekeleza "mradi wa kampasi za furaha" 100 ili kufadhili elimu kwa wasichana maskini na kuongeza idadi ya wasichana wanaoandikishwa shule. Vilevile tutawaleta wasichana elfu 30 kutoka nchi zinazoendelea kuhudhuria mafunzo nchini China na kutofa fursa laki 1 za mafunzo kwenye jamii za kienyeji kwenye nchi zinazoendelea. Chini ya mfuko unaofadhiliwa kwa pamoja kati ya China na Umoja wa mataifa, kutakuwa na program maalum za kuwajengea uwezo wanawake kutoka nchi zinazoendelea.

    Mabibi na mabwana,

    Marafiki,

    Tufanye kazi kwa pamoja na kufanya haraka kujenga dunia nzuri zaidi kwa wanawake na watu wote. Nautakia mkutano wa viongozi wa dunia mafanikio.

    Asante.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako