• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufanya kazi kwa pamoja ili Kuunda Ushirikiano Mpya wa kunufaisha pande zote na Kujenga Jumuiya ya Pamoja kwa ajili ya vizazi vijavyo -- Hotuba katika Mjadala Mkuu wa Kikao cha 70 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2015-11-09 12:26:00

    (Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China    New York, Septemba 28, 2015 )

    Miaka sabini iliyopita, kizazi kilichopita kilipigana vita kishujaa na kushinda mapambano dhidi ya ufashisti duniani na kufunga ukurasa kwa kiza katika historia ya binadamu. Ushindi huo haukuwa rahisi.

    Miaka sabini iliyopita, kizazi hicho, chenye maono na mtizamo wa siku za usoni, kilianzisha Umoja wa Mataifa-mpango kamwe haukuwa umefanyika kabla. Shirika hilo la kimataifa linalowakilisha wote limeleta matumaini tumaini kwa wanadamu na kufungua ukusara wa zama mpya za ushirikiano.

    Miaka sabini iliyopita, kizazi hicho kiliweka pamoja hekima yao na kuidhinisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kuwekewa msingi wa utaratibu wa kisasa wa kimataifa, na kuanzisha kanuni za msingi za mahusiano ya kisasa ya kimataifa. Hayo yalikuwa ni mafanikio yenye athari kubwa.

    Mheshimiwa Rais,

    Ndugu Viongozi wenzangu,

    Tarehe tatu ya mwezi Septemba, watu wa China, pamoja na wengine duniani, waliadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya ushindi katika vita ya Watu wa China dhidi ya Uchokozi wa Japan na Vita Kuu vya Kupambana na ufashisti. Kama ukumbi kuu katika eneo la Mashariki mwa dunia, China ilishiriki kwenye mapambano hayo kwa kujitolea kwa hali ya juu na raia wake milioni 35 walijeruhiwa katika mapambano yake dhidi ya vikosi vya kijeshi vya Japan. China sio tu iliokoa nchi na watu wake kutoka kwa uvamizi wa Japan, lakini pia ilitoa msaada kwa vikosi vilivyokuwa vikikabili Uvamizi eneo la Ulaya na Pasifiki, na hivyo kufanya mchango wa kihistoria kwa ushindi huo.

    Historia ni kioo. Ni kupitia kupata mafunzo kutokana na historia ndio dunia inaweza kuepuka kurudia migogoro ya siku za nyuma. Tunapaswa kutazama historia na hofu na kupitia kwa misingi ya dhamiri ya binadamu. Siku zilizopita haziwezi kubadilishwa, lakini zile baadaye zinaweza kutengenezwa. Kubeba historia katika mawazo sio kuendeleza chuki. Badala yake, lengo lake ni kuhakikisha kwamba watu hawasahau mafunzo yake. Kukumbuka historia haina maana kuwa umejawa na hofu ya siku za nyuma. Badala yake, katika kufanya hivyo, lengo letu ni kujenga maisha bora ya baadaye na kupitisha mwenge wa amani kutoka kizazi hadi kizazi.

    Mheshimiwa Rais,

    Ndugu Viongozi wenzangu,

    Katika kipindi cha miongo saba Umoja wa Mataifa umefanikiwa katika mambo mengi. Umeshuhudia juhudi zinazofanywa na nchi zote za kuzingatia amani, kujenga nchi zao wenyewe, na kujiingiza kwenye ushirikiano. Baada ya kufikiwa kwanzo mpya wa kihistoria, Umoja wa Mataifa unahitaji kushughulikia suala kuu la jinsi bora ya kukuza amani duniani na maendeleo katika karne ya 21.

    Dunia inaenda kupitia mchakato wa kihistoria wa kuharakisha mageuzi. Mwanga wa amani, na maendeleo vitakuwa nguvu ya kutosha ili kuondoa uwezekano wa vita, umaskini na ukosefu wa maendeleo. Jitihada za maendeleo za nchi mbalimbali, kuongezeka kwa masoko yanayojitokeza na nchi zinazoendelea imekuwa mwenendo wa kupendeza wa kihistoria. Utandawazi wa uchumi na ujio wa teknolojia ya habari na mawasiliano zimefungua fursa mpya uzalishaji kwenye.

    Utandawazi wa uchumi na teknolojia ya habari vimeunda fursa ya kipekee ya maendeleo lakini pia kuibua changamoto na vitisho vipya ambazo lazima tuzikabili.

    Kama usemavyo msemo mmoja wa kale wa Kichina, "Lengo kubwa ni kuwa na dunia ambayo kiukweli inawashirikisha wote." Amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru ni maadili ya kawaida kwa wanadamu wote, na malengo ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo malengo haya bado hayajapata mafanikio makubwa; Kwa hiyo ni lazima tuendelee za juhudi zetu. Katika dunia ya leo, nchi zote zinategemeana na kushiriki hatima ya pamoja. Tunapaswa kujitolea upya kwenye dhamira yetu ya maazimio na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kujenga mtindo mpya wa mahusiano ya kimataifa yanayoangazia maslahi ya kila upande, na kujenga jamii ya baadaye pamoja . Ili kufikia lengo hili, tunahitaji kuelekeza jitihada zetu kama ifuatavyo:

    - Tunapaswa kujenga ushirikiano ambao unatendeana nchi zote kwa usawa, kushiriki katika mashauriano na kuonyesha maelewano. Kanuni ya usawa inaongezwa msisitizo na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Mustakabali wa dunia lazima ushirikishe nchi zote. Nchi zote ni sawa. Zilizo kubwa, zenye nguvu na matajiri hazipaswi kudhulumu zile ndogo, wanyonge na maskini. Kanuni ya uhuru inamaanisha uhuru na mipaka ya nchi zote unafaa kuheshimiwa na maswala yake ya ndani hayawezi kuingiliwa.

    Pia ina maana kwamba nchi zote zina haki ya kufanya uchaguzi wao wenyewe wa mifumo ya kijamii na njia ya maendeleo, kwamba haki hiyo lazima inzigatiwe, na kwamba juhudi za nchi zote za 'kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuboresha maisha ya watu zinapaswa kuheshimiwa.

    Tunapaswa kujitolea kwenye ushirikiano wa kimataifa lakini sio kila nchi kuwa kivyake. Tunapaswa kupitisha maoni mapya ya kutafuta matokeo mazuri kwa wote, na kukataa ya mawazo kizamani ambayo inafaidi upande mmoja na kuleta hasara kwa upande mwingine. Kushauriana ni muhimu kwenye demokrasia, na ni lazima pia kuwa njia muhimu ya utumiaji utawala wa kisasa wa kimataifa. Tunapaswa kutatua migogoro na tofauti kwa njia ya mazungumzo na mashauriano. Tunapaswa kuwa na ushirikiano wa dunia katika ngazi za kimataifa na kikanda, na kukumbatia mbinu mpya ya mahusiano ya nchi nan chi ambayo inahusu mazungumzo badala ya mapambano, na yenye ushirikiano badala ya muungano. Nchi kubwa zinapaswa kufuata kanuni za kutokuwa na mgogoro, mapambano, kuheshimiana kwenye ushirikiano na mahusiano yao.

    Nchi zenye uwezo mkubwa zinafaa kuzitendea kwa usawa nchi ndogo na siku zote kuweka haki kabla maslahi yao wenyewe.

    - Tunapaswa kukuza usalama unaoshirikisha, haki, ushiriki wa pamoja na faida kwa wote. Katika wakati huu wa utandawazi wa uchumi, usalama wa nchi zote unahusiana nan chi zote. Hakuna nchi inaweza kudumisha usalama kikamilifu kwa juhudi zake mwenyewe, na hakuna nchi inaweza kufikia utulivu kwa kusababisha migogoro kwa nchi nyingine. Sheria mbaya inadhoofisha wale wasio na nguvu na kusalia kutegemea wenye nguvu; hiyo siyo njia zuri ya nchi yoyote kufanya mahusiano nan chi nyingine. Wale ambao wanachukua mwelekeo wa ubinafsi na kutumia nguvu watatambua kwamba wanainua jiwe na kuliacha ligonge miguu yao wenyewe .

    Tunapaswa kuachana kabisa na mawazo ya Vita Baridi, na kuendeleza maoni mapya ya pamoja, ushirika na usalama endelevu. Tunapaswa kutumia kikamilifu jukumu kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama katika kumaliza mgogoro na kutunza amani, na kuwa na zaidi ya mbinu moja ya kutafuta ufumbuzi wa amani kwa migogoro na kuchukua hatuamwafaka, ili kubadilisha uadui kuwa urafiki. Tunapaswa kuendeleza ushirikiano wa kimataifa katika nyanja za kiuchumi na kijamii na kuchukua mfumo wa jumla wa kushughulikia vitisho vya jadi na vilivyoko kwa sasa, ili kuzuia migogoro.

    - Tunapaswa kukuza, ubunifu na umoja wa maendeleo ulio wazi na wenye faida kwa wote. Mgogoro wa kifedha wa kimataifa wa mwaka 2008 ulitufundisha kwamba kuruhusu mitaji bila kuwa na makini ili kujipatia faida kutasababisha machafuko, na kwama ustawi wa kimataifa hauwezi kujengwa juu ya misingi dhaifu wa soko lisilo na maadili.

    Kuongezeka kwa pengo kati ya matajiri na maskini sio haki na sio endelevu.

    Ni muhimu kwetu kutumia mbinu mbalimbali ili kuunda ushirikiano kwenye masoko na majukumu ya serikali, na kujitahidi kufikisha ufanisi kwa wote na kwa usawa.

    Maendeleo yatakuwa na maana pale yatakapojumuisha kila mmoja na kuwa endelevu. Ili kufanikisha maendeleo kama hayo inahitaji uwazi, kusaidiana na kushirikiana. Katika dunia ya leo, watu karibu milioni 800 bado wanaishi katika umaskini mkubwa, karibu milioni sita wana kufa kabla umri wa miaka mitano kila mwaka, na karibu watoto milioni 60 hawapati huduma ya elimu. Mkutano uliokamilika hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo uliidhinisha Agenda ya Maendeleo ya baada ya mwaka 2015.

    Lazima tubadilishe ahadi zetu kuwa vitendo na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata mahitaji yake, anapata maendeleo, na anaishi kwa heshima.

    Tunapaswa kuongeza mabadilishano baina ya ustaarabu wetu ili kukuza maelewano, kuweza kuwashirikisha wote na kuheshimu tofauti zetu. Dunia inapendeza zaidi kutokana na utofauti wake wa kiutamaduni. Utofauti unaleta kubadilishana, kubadilishana kunajenga ushirikiano, na ushirikiano unaleta maendeleo.

    Katika mwingiliano, ustaarabu lazima ukukubali tofauti za kila mmoja. Ni kwa njia ya kuheshimiana, kujifunza kuheshimiana, na usawa mshikamano ndipo dunia inaweza kudumisha utofauti wake na kustawi.

    Kila mtindo wa kijamii inawakilisha maono ya kipekee na mchango wa watu wake, na hakuna mtindo bora kuliko mwingine. Lazima staarabu tofauti zishiriki katika mjadala na mabadilishano badala ya kujaribu kuwatenga au kuchukua nafasi wengine.

    Historia ya mwanadamu ni mchakato wa kubadilishana, mwingiliano, na ushirikiano miongoni mwa staarabu tofauti.

    Tunapaswa tuheshimu ustaarabu wote na kuupea umuhimu kwa sawa.

    Tunapaswa kuteka msukumo kutoka kwa kila mmoja ili kuongeza ubunifu kwenye maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.

    - Tunapaswa kujenga mazingira yanayozipa raslimali asili zetu kipa umbele na kuwa na uchumi unaojali mazingira. Mwanadamu anaweza kutumia raslimali asili na hata kujaribu kuigeuza. Lakini atagundua kwamba sisi ni sehemu ya asili. Tunapaswa kutunza mazingira. Tunapaswa kupatanisha maendeleo ya viwanda na asili na kuingiza maelewano kati yetu na asili ili kufikia maendeleo endelevu duniani kote na maendeleo ya pande zote ya ubinadamu.

    Kujenga mazingira yetu ni muhimu kwa vizazi vijavyo. Wanachama wote wa jumuiya ya kimataifa wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga ikolojia zuri ya kimataifa. Tunapaswa kuheshimu asili, kufuata njia za asili, na kulinda asili.

    Tunapaswa kuzingatia zaidi uzalishaji unaojali mazingira, utoaji wa chini ya gesi ya kaboni, na maendeleo endelevu. China itabeba sehemu yake ya wajibu na kuendelea kujitahidi kwenye swala hili la mazingira. China pia inaomba nchi zilizoendelea kutimiza majukumu yao ya kihistoria, kutekeleza ahadi zao za kupunguza utoaji wa gesi chafu, na kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

    Mheshimiwa Rais,

    Ndugu Viongozi wenzangu,

    Zaidi ya watu bilioni 1.3 wa China wanajitahidi kutimiza ndoto ya Kichina ya kuwa na taifa jipya. Ndoto ya watu wa China ina uhusiano wa karibu na ndoto za watu wengine duniani. Hatuwezi kutimiza ndoto ya Kichina bila mazingira yenye amani duniani, utaratibu imara wa kimataifa, na ufahamu uungwaji mkono na msaada wa nchi zingine duniani. Kufanikiwa kwa ndoto ya Kichina kutaleta fursa kubwa kwa nchi nyingine na kuchangia amani na maendeleo ya kimataifa.

    Hata mazingira yawe magumu kiasi gani duniani na hata China iwe na nguvu kiasi gani kamwe haitataka kutawala dunia lakini itaendelea kushiriki katika ujenzi wa amani duniani.

    Nia yetu ni maendeleo ya amani.

    China itaendelea kuchangia maendeleo ya kimataifa. Tutaendelea kufuatilia maendeleo ya pamoja na mkakati wa ufunguzi. Tuko tayari kubadilishana uzoefu wetu na fursa kwa nchi nyingine na kuwakaribisha kujiunga nasi katika safari yetu na kusonga mbele pamoja nasi kuelekea maendeleo ya pamoja.

    China itaendelea kutekeleza utaratibu wa kimataifa. Tutaendelea kufuata njia ya maendeleo kwa njia ya ushirikiano. China ilikuwa nchi ya kwanza kuweka sahihi yake kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Tutaendelea kuzingatia utaratibu wa kimataifa na mifumo inayounganishwa na maazimio na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa. China itaendelea kusimama pamoja na nchi nyingine zinazoendelea. Tunaunga mkono kwa dhati uwakilishi mkubwa na sauti kwa nchi zinazoendelea, na hasa nchi Afrika, katika utawala wa kimataifa. Siku zote kura ya China katika Umoja wa Mataifa ni kwa ajili ya kuunga mkono nchi zinazoendelea.

    Napenda kuchukua fursa hii kutangaza uamuzi wa China wa kuanzisha hazina ya miaka kumi ya amani na Maendeleo kwenye Umoja wa Mataifa ya dola bilioni 10 za kimarekani kusaidia kazi ya Umoja wa Mataifa, kukuza ushirikiano wa kimataifa, na kutoa mchango mkubwa wa amani na maendeleo duniani. Napenda kutangaza kwamba China itajiungana na utaratibu mpya wa utayari wa uwezo wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa na na tayari tutaunda kikosi cha dharura cha kulinda amani chenye wanajeshi 8,000.

    Ningependa pia kutangaza kwamba China itatoa jumla ya dola milioni 100 kama msaada kwa jeshi la Umoja wa Afrika katika miaka mitano ijayo ili kusaidia uanzishwaji wa Kikosi cha dharura cha Afrika ili kuwezesha bara hilo kushughulikia kwa haraka migogoro.

    Mheshimiwa Rais,

    Ndugu Viongozi wenzangu,

    Huku Umoja wa Mataifa ukiingia muongo mpya, tuungane kwa karibu zaidi na kuwa na ushirikiano mpya ambao unanufaisha pande zote na jamii inayojali vizazi vya baadaye.

    Tuwe na maono ya ulimwengu usio wa vita na daima tufurahie amani ya kudumu.

    Matumaini ya maendeleo, mafanikio, usawa na haki zienee duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako