• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko hapa kwa ajili ya Amani -- Taarifa kwa Mkutano wa Kilele wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2015-11-09 12:28:17

    (Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China   New York, Septemba 28, 2015)

    Rais Obama,

    Katibu Mkuu Ban Ki-moo,

    Wapendwa wafanyakazi wenzangu,

    Namshukuru Rais Obama kwa juhudi zake za kuitisha mkutano huu wa kilele wa kulinda amani.

    Amani ni matumaini ya kawaida na ni lengo kubwa lililopo kwa kila binadamu. Ni kutokana na madhumuni ya kupata amani ndio Opresheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zikaanzishwa. Hivi sasa zikiwa kama ni njia muhimu ya kushikilia amani na usalama duniani, operesheni hizi za kulinda amani zimeleta imani kwenye maeneo yanayokabiliwa na migogoro, na kutoa matumaini kwa wahanga wa maeneo hayo.

    Katika wakati huu tunaozungumza, watu kwenye maeneo mengi yenye migogoro duniani bado wanaendelea kuteseka. Wanatamani sana amani, na wana matumaini makubwa na Umoja wa Mataifa, na matarajio makubwa kwa operesheni zake . Ifuatayo ndio misimamo ya China:

    - Kanuni za msingi za kulinda amani zinapaswa kufuatwa kwa madhubuti

    Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kanuni za Hammarskjold- ni miongozo ya msingi katika operesheni za kulinda amani – inapaswa kuendelea kuheshimiwa. Maazimio ya Baraza la Usalama yanapaswa kutekelezwa kwa ukamilifu, na kutoruhusu nchi yoyote kufanya vitendo vilivyo juu ya mamlaka yake. Kazi za kulinda amani zinapaswa kuendelezwa kulingana na hali ya sehemu na utayari wa wenyeji. Mikakati ya kuondoka inahitaji kupangwa na kutekeleza kwa mujibu wa wakati uliopangwa.

    - Mfumo wa kulinda amani unahitaji kuboreshwa.

    Operesheni zinapaswa kupangwa kwa mfululizo huku kukiwa na kinga za kidiplomasia na ujenzi wa amani, na wakati huohuo ziende sambamba na wapatanishi wa kisiasa, utawala wa sheria, mapatano ya kitaifa, na kuboreshwa kwa hali ya maisha. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linapaswa kuwa makini zaidi na mawazo ya pande zote zinazohusika moja kwa moja, na mitazamao ya nchi zote ambazo zinachangia wanajeshi. Ushirikiano mzuri wa kulinda amani unapaswa kuanzishwa kati ya Umoja wa Mtaifa na mashirika husika ya kikanda.

    - Mfumowa kukabiliana haraka na migogoro unahitaji kukuzwa

    Kikundi cha kwanza cha askari wa operesheni ya kulinda amani kinachosambazwa, kinaweza kuleta mtazamo mzuri wa amani na kupata muda zaidi wa kuokoa maisha. China inakaribisha Umoja wa Mtaifa kwa kuanzisha mfumo wa Uwezo wa Kuwa Tayari, na kuzitaka nchi zote wajumbe kujiunga kwenye mfumo huo.

    - Uungaji Mkono mkubwa na msaada vinapaswa kutolewa kwa Afrika.

    Afrika ina mahitaji makubwa ya kulinda amani. Katika muda mrefu, Jumuiya ya Kimataifa na Umoja wa Mataifa zinapaswa kuzisaidia nchi za Afrika katika kuongeza uwezo wao wa kuimarisha amani na utulivu, ili masuala ya Afrika yaweze kutatuliwa kwa njia ambazo zinaendana na mahitaji ya Afrika.

    Wafanyakazi wenzangu,

    Ikiwa kama mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China imeshiriki katika operesheni za kulinda amani kwa miaka 25. Sisi ni wachangiaji wakuu wa wanajeshi na fedha kwenye operesheni hizi. Ili kuunga mkono uboreshwaji na uimarishwaji wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, ninatangaza kwamba:

    Kwanza, China itajiunga kwenye Mfumo wa Uwezo wa Kuwa Tayari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa. Tumeshaamua kuwa viongozi wa kuanzisha kikosi cha kudumu cha polisi wa kulinda amani na kujenga kikosi cha dharura chenye wanajeshi 8,000.

    Pili, China itazingatia vizuri maombi ya Umoja wa Mataifa ya kutaka wanajeshi zaidi wahandisi na usafiri na wahudumu wa afya kushiriki kwenye opesheni za kulinda amani za Umoja wa Mtaifa.

    Tatu, katika miaka mitano ijayo, China itatoa mafunzo kwa wanajeshi 2,000 wa kulinda amani kutoka nchi nyingine, na kuendeleza program 10 za usaidizi wa kutegua mabomu ambazo zitajumuisha utoaji wa mafunzo na vifaa.

    Nne, katika miaka mitano ijayo, China itatoa msaada wa kijeshi Dola za Kimarekani milioni 100 kwenye Umoja wa Afrika ili kuunga mkono ujenzi wa Kikosi cha Dharura cha Afrika na Kikosi cha Afrika cha Kukabiliana Haraka na Migogoro.

    Tano, China itatuma kikosi chake cha kwanza cha helikopta za kulinda amani kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa katika Afrika.

    Sita, sehemu ya pesa za amani na maendeleo ya China na Umoja wa Afrika zitatumika katika kusaidia operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

    Wafanyakazi wenzangu,

    Askari kumi na nane wa China wanawake na wanaume wamepoteza maisha yao kwenye operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa. Miaka mitano iliyopita, tulimpoteza He Zhihong, polisi mwanamke wa kulinda amani katika Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mtaifa nchini Haiti. Amemwacha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne na wazazi wake ambao ni wazee. Aliwahi kuandika: "Katika ulimwengu huu mkubwa, naweza kuwa kama unyoya mdogo. Lakini hata hivyo, nataka huu unyoya ubebe matumaini ya amani."

    Hili ndio tumaini lake, na pia ni ahadi ya China ya amani.

    Asanteni!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako