• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MIUNDO MBINU YA CHINA NI YENYE KUVUTIA SANA

    (GMT+08:00) 2016-08-11 16:44:40

    Na Elias Mhegera, Beijing

    Jumanne iliyopita basi moja lilionekana kwenye barabara ya mji wa Qinhuangdao, ulio kaskazini mwa China. Basi hilo linajulikana kama Basi ya Reli kwa kuwa linaonekana kama daraja, ambalo magari yanaweza kupita chini yake wakati daraja lenyewe likisonga mbele kwenye njia yake iliyojengwa barabarani.

    Jaribio la basi hilo lenye spidi ya wastani ya kilomita 40 kwa saa limevutia ufuatiliaji kwa sababu nyingi tu kwa uwezo wa uvumbuzi wa Wachina katika kupunguza msongamano barabarani, na pia kwa miundo mbinu ya mawasiliano ya nchi hiyo ambayo inajenga miradi mbalimbali katika nchi nyingi duniani.

    Ukiniuliza nikutajie nini kimenivutia zaidi hapa Beijing na China kwa ujumla baada ya kuwa nimekaa katika nchi hii kwa zaidi ya miezi mitano hadi sasa, nitakujibu kwamba ni miundombinu hususani ya barabara na reli.

    Kutokana na kuishi katika Jiji la Dar es Salaam ambalo lina foleni kubwa ya magari mara nyingi nimekuwa nikilazimika kuamka asubuhi na mapema sana walau inabidi saa 11.30 alfajiri niwe barabarani.

    Hali ni mbaya kwa nayakati za asubuhi watu wanapokuwa katika harakati za kuwahi ofisini na katika sehemu zao za biashara na pia nyakati za jioni wanaporejea nyumbani.

    Jiji la Dar es Salaam lina wakazi wapatao milioni tano wakati Jiji la Beijing yalipo makazi yangu kwa sasa lina wakazi milioni 21.7. Pamoja na wingi huu wa watu miundo mbinu ya kisasa imesababisha pasiwepo na foleni kubwa kama ilivyokuwa katika majiji mengi Barani Afrika.

    Pamoja na kuwapo barabara pana ambapo magari manane yanaweza kupishana bila kukwaruzana na pia kuwapo kwa barabara za kulipia zipitazo juu kwa juu, bado kuna treni ziendazo kasi zikipita chini ardhini bado kuna mabasi makubwa ya ghorofa na yasiyo na ghorofa na pia yapo ya umeme na ya kawaida kwa hali hiyo idadi ya Wana-Beijing imemezwa vizur kwa usafiri wa uhakika.

    Lakini miundombinu hiyo si kwa mijini peke yake imetapakaa nchi nzima. Hivi karibuni tulisafiri umbali wa kilometa 1,196.6 kwa treni ya mwendo kasi ambayo ilitumia saa tano kufika katika jiji la Suzhou tukitokea Beijing treni hiyo ina uwezo wa kwenda kilomita 360 kwa saa.

    Nalinganisha umbali huo na kwetu Tanzania naona ni mkubwa kuliko wa Dar es Salaam hadi Mwanza ambao ni kilometa 1,131.7 tu. Gharama ya tiketi ya treni kwenda na kurudi ilikuwa ni Yuani 528 ambazo ni sawa na shilingi laki moja na elfu stini za Kitanzania (160,000) za Kitanzania kwenda na kurudi ina maana ni sawa na sh elfu 80 kwa safari moja, usafiri huo ndiyo tegemeo kuu la wananchi hapa China.

    Pili tulitembelea eneo la viwanda linaloitwa Suzhou Industrial Park (SIP), hilo ni eneo maalumu linalotengwa kwa ajili ya viwanda pamoja taasisi zitakazokuwa na manufaa kwa viwanda hivyo.

    Kwa Tanzania unaweza kulinganisha na Benjamin William Mkapa Special Economic Zone (BWM-SEZ) iliyopo Mabibo eneo la Ubungo External. Eneo hilo la viwanda ilijengwa mwaka 1980.

    Lakini eneo lake ni sawa na nusu ya ukubwa wa Wilaya ya Kinondoni kwa sababu lina ukubwa wa kilomita za mraba 288 wakati Wilaya ya Kinondoni ina ukubwa kilomita za mraba 531.

    Kwa hakika niliona kwamba hata sisi Wa-Afrika tukijipanga kwa fikra kubwa na tukiunganisha nguvu tunazo raslimali za kutosha za kufikia maendeleo kama haya. Idadi ya Wachina kama nchi ni watu bilioni 1.38 kwa takwimu za mwaka 2016 na wakati Afrika bara zima lina watu bilioni 1.11.

    Pamoja na idadi kubwa ya watu lakini Jiji la Beijing bado limeruhusu wakazi wake wenye kutumia piki piki, baiskeli na hata bajaj waweze kufika kwa sababu zipo sehemu wanazozitumia bila kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

    Hata hivyo katika kuepuka uchafuzi wa mazingira piki piki za hapa hazitumii injini za mafuta na kinyume chake zinatumia betri zainazoweza kudumu kwa saa nane mfululizo iwapo zitakuwa katika matumizi na baada ya hapo mtumiaji anaweza kupita katika kituo na kuchukua betri nyingine yenye moto tayari.

    Pichani ni treni ya mwendo kasi ambayo huweza kukimbia hadi kilometa 360 kwa saa. Kwa ujumla usafiri wa treni umerahisisha maisha kwa kiwango kikubwa hapa China.

    Kwa mfano hata ukiamua kupande treni zipitazo ardhini chini kwa chini bado foleni vituoni ni ndogo na hata nauli si kubwa kwa mwendo mrefu wa kwenda na kurudi gharama haiwezi kuzidi shilingi elfu mbili za Kitanzania.

    Ni kweli kwamba usafiri huo ndiyo tegemeo kubwa la watu wengi kwa hisyo siyo lazima upate kiti cha kukaa wakati unapongia lakini ni jambo la kwaida abiria kushuka muwapo niani na hivyo uanweza kupata kiti na kukaa ukiwa njiani.

    Bado usafiri wa taxi umerahishwa kwa sababu unaweza kubonyeza kitufe kidogo katika simu yako na mara madereva wote waliopo jirani nawe watapata taarifa na aliyepo karibu zaidi na wewe ndiye atakuchukua.

    Ipo mifumo kadhaa ya aina hii mmoja wapo uniatwa DIDI ramani ya kidijitali yenye sauti ya kuongoza safari yako wee na dereva wako.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako