• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya China na Afrika sasa umekua

    (GMT+08:00) 2016-08-25 15:48:55
    Na Elias Mhegera, Beijing

    Siri kubwa ya maendeleo ya uchumi wa China yenye watu zaidi ya bilioni 1.36 ni kuwajali wananchi wake, na kuhakikisha kwamba kila mtu anakuwa na fursa ya kuzalisha chochote katika eneo alipo.

    Katika matembezi yangu wenye wizara ya Biashara, nimejifunza kuwa, licha ya kuwawezesha raia wake walio ndani ya nchi, China pia imewasaidia wale waliopo nje ya nchi wakijishughulisha na mambo kadhaa ya uzalishaji.

    Kwa mujibu wa Bw. Sunny Gang muongozaji wageni chini ya Wizara ya Mambo ya Nje Jimbo la Hainan, China inakuwa na wastani wa wavuvi milioni mbili nje ya nchi kila mwaka.

    Lakini uwekezaji wa China katika Bara la Afrika unaonesha kwamba eneo la ujenzi ndilo yamefanyika maendeleo makubwa zaidi, hususani katika eneo la miundo mbinu ya barabara na majengo.

    "Afrika na China ni marafiki wa kudumu na tunataka twende pamoja katika gurudumu la maendeleo" anasema Afisa Mwandamizi Wizara ya Biashara Bi Yang Peipei ,ambaye pia ni mkurugenzi wa mahusiano ya nje ya kibiashara katika wizara hiyo alipowasilisha malengo ya ushirikiano kati ya Afrika na nchi yake chini ya Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.

    Mwaka 1978 China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango chini ya Rais Deng Xiaoping, sera ambayo imesaidia kwa kiwango kikubwa kulinyanyua taifa hili.

    Mafanikio ya China, sio tu yameinufaisha China bali pia yanazinufaisha nchi rafiki. Kwa mfano katika miaka mitatu ijayo (2015-2018) China imetenga kiasi cha dola bilioni 60 kwa ajili ya Bara la Afrika.

    Katika kipindi cha miaka sita iliyopita zaidi ya dola bilioni 400 zilitumika kwenye uwekezaji katika maeneo ya elimu na afya Barani Afrika, na kuondoa umaskini kwa ujumla.

    Naye Prof. Lu Keli kutoka Chuo Kikuu cha Renmin cha China mara alipozungumza na wanahabari kutoka Afrika. Anayaainisha maeneo kadhaa kama chachu ya maendeleo, kwanza ni ushirikishwaji wa wananchi, katika hili anasema msomi huyo kwamba kwa sasa uwakilishi wa wananchi katika bunge la nchi hiyo ni mkubwa kwa sababu mfumo unaotumika siyo wa vyama bali makundi mbali mbali ya kijamii na taaluma.

    Kwa yeyote ambaye amebahatika kufika China mambo yanayojidhihirisha ni kwamba kwa muda mrefu ujao China litaendelea kuwa taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi kwa sababu hakuna dalili zozote za kutetereka.

     

    Ushirikiano kati ya Afrika na China sasa umekuwa pia kati ya watu kwa watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako