• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamera zimeongeza usalama barabarani, watembea kwa miguu wanatembea bila hofu …

    (GMT+08:00) 2016-08-25 15:59:11

    Na Elias Mhegera, Beijing

    Miongoni mwa mambo unayoweza kuyashuhudia na kuyafurahia katika miji yote mikubwa ya China, ni uendeshaji mzuri wa magari, kiasi kwamba watembea kwa miguu wanatembea bila wasiwasi.

    Sababu ya kutakuwa na wasiwasi, niliijua baada ya kutembelea kiwanda cha HIKVISION, ambacho kimejikita katika teknolojia nyingi za kipekee kuhusiana na masuala ya kamera za kusimamia mawasiliano barabarani na usalama .

    Miongoni mwa teknolojia hizo ni kamera za barabarani, kamera hizo zimeleta faraja kubwa kwa watembea kwa miguu, kwani wenye magari wanafahamu fika kwamba iwapo wataendesha vibaya basi kamera zitawanasa na mwisho wa siku watalipa faini kubwa, kutumikia vifungo au vyote kwa pamoja.

    Binafsi nimefurahia sana hali hii hususani nikikumbuka matukio mawili ya vifo ambayo yalisababishwa na uzembe wa madereva katika jiji la Dar es Salaam. Katika tukio la kwanza mwaka 2008 dada mmoja alipoteza maisha baada ya kugongwa na basi pale alipokutana nalo uso kwa uso kwenye kona mtaa wa Lugoda kuelekea kiwanda cha majani ya chai, na dereva akashindwa kufunga breki na hatimaye dada huyo akafa papo hapo.

    Katika tukio la pili nilimshuhdia mtoto mdogo mwenye umri wa takribani miaka 10 akikata roho baada ya kugongwa na gari katika maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam dereva alikimbia na hakuweza kukamatwa mara moja.

    Matukio yote haya mawili yalisababishwa na mwendo kasi wa magari husika. Kwa hapa China hali ni tofauti sana, mara nyingi mwenye gari anaweza kulumbana na mwenye gari mwenzake, lakini siyo na mtembea kwa miguu. Hii ni kwa sababu sheria za usalama barabarani zinawalinda vizuri watembea kwa miguu, tena kamera za barabarani zinarekodi matukio yote yanayojiri barabarani.

    Na mara itatokea ajali basi picha za video zitatumika kuonesha nani alifanya nini, na hivyo mhalifu atakuwa hana la kujitetea. Huo ni mfumo mzuri wa upatikanaji wa taarifa za barabarani.

    Lakini pia kampuni hii ya Hikvision inatengeneza kamera ndogo zilizopo katika mfumo wa simu za mkononi lakini zikiwa na uwezo mkubwa wa kuchukua matukio katika mfumo wa video. Kamera hizo zinatumiwa na askari wa usalama barabarani hasa pale wanapoenda kuangalia nini kilitokea barabarani basi watachukua picha na sauti kwa pamoja kwa kutumia rekoda hizo.

    Lakini pia wanatengeneza kamera za kuruka angani maarufu kama 'drones', kamera hizo zinaweza kusaidia kupiga picha maeneo ya juu hususani pale ambapo mwanadamu hawezi kufika kwa mfano iwapo kuna matukio ya moto au milipuko.

    Katika ujumla wake China imejiweka vizuri katika eneo la usalama kwa ktumia njia ya mawasiliano, na ndiyo maana hata katika michezo ya Olyimpiki iliyofanyika Brazil, makampuni ya habari na mawasiliano ya China yalipewa zabuni za kusambaza vifaa vya kulinda na kusimamia usalama.

    Kwa kutumia mfumo wa kielektroniki mashine maalumu zinaweza kumuonesha mtu anayetaka kuegesha gari mahali penye nafasi kwa kubonyeza tu kitufe mara anapofika mahali hapo, ambapo ramani yote inatakuwa katika skrini na huduma hiyo inaweza kuunganishwa kwenye simu yako ya mkononi.

    Jambo la kufurahisha ni kwamba kwa vile mhusika anatakiwa kutembea na kitambulisho chake muda wote, mara anapofika katika eneo hilo mitambo huweza kunasa siyo picha tu, bali hata kumbukumbu nyingine na kama amewahi kuhusika na uhalifu taarifa zote zitakuja mara moja.

    kamera usalama zimeleta mabadiliko makubwa katika huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na usalama barabarani, ulinzi majumbani na hata huduma za benki

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako