• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNAPOFIKA 'JIJI LA MAJI' HANGZHOU JIANDAE KWA UTALII WA ZIWANI…

  (GMT+08:00) 2016-09-05 11:07:25

  Elias Mhegera, Beijing

  Nilipofika Hangzhou nilijiona kama kwamba nipo nyumbani katika Jiji la Mwanza, ilikuwa ni kutalii kwenye Ziwa la Magharibi (West Lake) ambalo liliwekwa kwenye orodha ya hifadhi za utalii wa UNESCO mwaka 1987.

  Kama unavyoona humo ziwani kuna vyombo vya usafiri vya aina mbali mbali kwa hiyo wewe unajipima utatumia chombo cha aina gani na utakaa ziwani kwa muda gani, kuna mitumbwi, boti za kawaida hadi meli za kitalii, ni wewe tu na pochi lako, ukitaka kukaa humo ziwani siku nzima ni uamuzi wako, ili mradi kila mmoja wetu alifurahia sana utalii huo.

  Lakini katika ujumla wake utalii wa majini nchini China ni utalii rasmi, na zipo sehemu nyingi za aina hiyo ukiwamo mto Changjiang. Mto huu ndio mkubwa kuliko yote nchini humo na pia ni wa tatu kwa ukubwa duniani baada ya Mto Nile ambao unafuatiwa na Mto Amazon.

  Katika ziara zangu hapa China nimebahatika kufanya utalii ndani ya mto huo mara mbili, ni jambo la kawaida kuwakuta wanafamilia za Wachina wamekaa pamoja nyakati za jioni katika viambaza vya mto huo na kisha hukamilisha siku yao kwa kufanya ziara ndani ya mto huo.

  Raha zaidi huja nyakati za usiku kwa sababu pembezoni mwa mto kuna taa zenye rangi ambazo hupendezesha mandhari lakini pia ni jambo la kawaida kukuta vikundi vya ngoma za kitamaduni wasanii wakiimba na hivyo waendesha boti hulazimika kusimamisha vyombo vya usafiri ili abiria wao wapate kushuhudia sanaa hizo hata kama ni kwa muda mfupi.

  Huleta raha zaidi unapokuwa na watoto ambao licha ya kuonesha furaha tele bali hupenda kuuliza maswali mara kwa mara kutokana na kila wanachokiona ndani ya mto. Labda sasa litakuwa jambo jema kwa wawekezaji wa nchi za Kiafrika kama vile Tanzania kuanzisha au kuendeleza utalii wa aina hiyo kwa sababu tayari zipo ndege ndogo za utalii hivyo haitakuwa kazi kubwa kuanzisha boti pia kwa nia hiyo hiyo ya utalii.

  Lakini si usafiri huo tu bali hata michezo ya majini kwa ajili ya watoto imewekwa sehemu nyingi na hasa pale mtalii anapokuwa amesafiri na watoto. Vinywaji na vyakula huambatana na utalii huo.

  Ni kweli kwamba nchini Tanzania kumekuwapo na michezo ndani ya ziwa na hata baharini isipokuwa imekuwa ikiwahusu matajiri wachache wenye kumudu kununua vifaa na vyombo kwa ajili ya michezo hiyo ya ziwani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako