• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VIONGOZI MAHIRI WAMININIKA HANGHZHOU

    (GMT+08:00) 2016-09-05 11:08:44

    Na Elias Mhegera-Hanghzhou

    Siku ya Jumamosi tarehe 03 Septemba jiji la Hanghzhou liligeuka na kuwa kitovu cha Dunia baada ya kupokea idadi kubwa ya viongozi wanaounda ushirika wa kiuchumi wa G20.

    Kwa wanahabari kutoka sehemu mbali mbali duniani hiyo ilikuwa ni siku ya kufahamishwa malengo ya mkutano wa G20. Nilibahatika kuonana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Uchumi na Maendeleo (OECD) Bw. Angel Gurria na tukafanya mazungumzo naye.

    Akizungumzia kwa ufupi historia ya OECD alisema mnamo Disemba 14 1960, mataifa 20 yalisaini makubaliano ya kuunda umoja huo ambao kwa sasa una jumla ya wanachama, 15 yenye ushawishi mkubwa katika uchumi duniani.

    Bw. Gurria alisema malengo mahsusi ya mkutano huu unaoendelea ni kuzuia mgogoro unaoweza kusababishwa na mataifa au taifa moja kuuza bidhaa nyingi kwa mpigo katika mataifa fulani na kuwanyima wengine haki hiyo.

    Pia akaongeza kwamba hata haki ya kuagiza malighafi haitakiwi kufanywa kwa siri na akafafanua kwamba taifa linaweza kuitwa limeendelea kutokana na kufanya biashara zinazozingatia maadili, na pia kupima pato la ndani la taifa hilo na uzalishaji wake kwa ujumla (GDP).

    Aidha alisema kwamba lengo ni kuzingatiwa kwa makubaliano kadhaa kama yalivyofikiwa na shirikisho la kimataifa la biashara WTO ili kuzuia rushwa, na mikataba mibovu. Lakini pia ni kujenga utamaduni wa uwazi katika miktaba mbali mbali na suala zima la ulipaji wa kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako