• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ataka maslahi ya mataifa madogo yazingatiwe

    (GMT+08:00) 2016-09-05 11:25:58

    Na Elias Mhegera-Hanghzhou

    Mkutano wa wakuu wa G20 ulifunguliwa jumapili mjini Hangzhou, mashariki mwa China, ambapo viongozi wa nchi hizo ambazo jumla ya uchumi wao zinachukua zaidi ya asilimia 80 ya ile ya dunia nzima wanakaa kwenye meza moja kujadili ongezeko endelevu, shirikishi na lenye uwiano la uchumi wa dunia.

    Katika hotuba yake Rais wa China Xi Jinping ambaye ndiye mwenyeji alisema kwamba biashara kwenye ngazi za kimataifa zinatakiwa kuzingatia usawa na kuhakikisha kwamba mataifa madogo hayaumizwi na mfumo uliopo.

    Lakini pia akayarejea maneno hayo siku ya pili Jumapili ya tarehe 4, Septemba wakati akimkaribisha mwenyekiti wa mkutano Rais wa India Bw. Shri Narendra Modi

    Waziri Mkuu wa Australia Bw. Malcom Turnbull alisisitiza juu ya ushirikiano ili kukabiliana na uhamishaji haramu wa pesa na ukwepaji wa kodi wa makampuni makubwa ya kimataifa.

    Lakini Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim alisistiza kwamba uchumi wa Dunia unatakiwa uwe shirikishi na uzingatie usawa. Na pia akasema ugaidi duniani limekuwa tatizo kubwa kwa sababu kuna watu wenye nguvu wanayafadhili makundi ya kigaidi.

    Zaidi ya hayo alizungumzia juu ya uwekezaji katika miundombinu, na ushirikiano katika kuondoa umaskini na kukabiliana na chanagamoto za Tabia Nchi. Alisifia juu ya lindi la ubunifu linalofanywa na wenyeji Serikali ya China.

    Na zaidi ya hayo akaasa kwamba wahudhuriaji wote wageuke kuwa mawakala dhidi ya ukiritimba katika biashara za kimataifa na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako