• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazingira ya mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2016-09-05 11:29:13

    Na Elias Mhegera-Hanghzhou

    Pamoja na hayo yaliyojiri katika mkutano wa wakuu wa G20 uliofunguliwa Jumapili (Septemba 4) wanahabari wa kimatifa walipata wasaa wa kutembelea sehemu mbali mbali za jiji la Hangzhou ili kujionea mandari nzuri na utunzaji wa mazingira hususani katika mradi wa Jiangyangfan Eco-park.

     

    Huu ni mradi ulioanzishwa rasmi kwa ajili ya kuzuia uchafuzi wa mazingira katika Ziwa West Lake ambalo ni kivutio kikubwa cha jiji. Ilionekana kwamba maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka milimani yalimwaga mchanga ziwani na hivyo kuhatarisha uhai wa ziwa lenyewe.

    Leo vyanzo hivyo vya maji vimepandwa aina ya miti ambayo inachuja mchanga na pia kuyasafisha maji kabla hayajaingia ziwani. Pia yapo maua ambayo yamepandwa katika maeneo hayo na kupata matumizi mahsusi katika utengenezaji wa dawa, sumu za kuulia wadudu na manukato.

    Usalama katika eneo zima la mkutano ni mkubwa na uwepo wa magari ya kusafirisha wahudhuriaji wa mkutano wa kada zote wakiwamo wanahabari ni kuwaridhisha sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako