• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa Jimbo la Jiangsu, China na Afrika waimarishwa na kampuni 400

    (GMT+08:00) 2017-03-24 08:43:35

    Ushirikiano baina ya jimbo la Jiangsu nchini China na Afrika umezidi kuwa imara ambapo mpaka sasa kuna kampuni 400 kutoka jimbo hilo zimewekeza Afrika huku kampuni nyingine zikionesha nia ya kwenda kuwekeza Africa.

    Uwekezaji wa kampuni hizo 400 umegharimu zaidi ya dola za Marekani bilioni 400 huku kukiwa na wafanyakazi 4000 kutoka katika jimbo hilo,wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali Africa.

    Jimbo hilo lililopo Pwani ya Mashariki ya nchi hiyo limeeleza mikakati yake katika ushirikiano na nchi za Afrika kuwekeza katika miradi mbalimbali.

    Makamu wa Rais katika ofisi ya Masuala ya mambo ya nje,Yan Gao amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokituo cha Mawasilianoya Habari kati ya Tanzania na Africa ameeleza kuwepo mikakati ya kuwekeza katika nchi nyingi zaidi.

    Alisema katika nchi ya Ethiopia na Tanzania wametengeneza maeneo huru ya uwekezaji yatakayoongeza makampuni ya uwekezaji Afrika ambapo kwa Tanzania watafungua Jiangsu Shinyanga Economic Zone Pack itakayoingiza kodi serikalini zaidi ya dola za marekani milioni 10 kwa mwaka.

    Pia katika nchi hiyo kutokana na Ushirikiano uliopo Madaktari kutoka jimbo hilo wamefika kutoa huduma kwa wananchi wa hali ya chini katika maeneo mbalimbali ikiwemo Zanzibara.

    Alisema kwa takwimu zilizopo mwaka jana makampuni 400 kutoka jimbo hilo waliwekeza barani Afrika kwa thamani ya dola za marekani sh. Bilioni 400 na wafanyakazi 4000 wako wakifanya kazi katika maeneo mbalimbali.

    Alisema kwa nchini Tanzania makubaliano yalifikiwa wakati wa ziara ya Rais wan chi hiyo Xi Jinping alipotembelea Tanzania na baadaye Waziri Mkuu wa Tanzania alipofanya ziara nchini china na kusaini mkataba wa makubaliano na kushuhudiwa na waziri mkuu wa China.

    Alisema zaidi ya wananchi wa jimbo hilo zaidi ya 1,000 watafanya kazi katika maeneo hayo huku wakiwekeza zaidi ya dola za marekani milioni 200.

    Alisema nchini Ethiopia kuna makampuni 17 kutoka jimbo hilo yakifanya kazi ambapo wamewekeza kwa dola za marekani milioni 216 na nchi hiyo ikipata kodi ya dola za marekani milioni 51.

    Alisema biashara kubwa wanayofanya na nchi za Africa ni Madini,Chuma na nyinginezo.

    Amesema kati ya kampuni zilizoonesha nia ya kwenda kuwekeza ni pamoja na kampuni kubwa ya kutengeneza Mashine za Ujenzi Xuzhou Construction Machinery Group (XCMG) ambayo iko katika mikakati ya kujenga viiwanda katika nchi mbalimbali Africa.

    Kampuni hiyo iliyopo katika mji wa Xuzhou na inashika nafasi ya tano duniani huku ikiwa ya kwanza nchini China kwa kutengeneza mashine mbalimbali.

    Meneja Mkuu wa kampuni hiyo,Hanson Kiu amesema Africa ni sehemu nzuri kwa uwekezaji kwa kuwa katika miaka ijayo ni lazima kukimbilia Africa lakini kuna mambo wanayoangalia kwa nchi wanazotaka kuwekeza ikiwemo sera za kifedha zinazowezesha kubadilisha na kusafirisha fedha pamoja na usalama wa nchi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako