• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya biashara ya nyumba ya China yapanua biashara zao Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-24 17:54:07

    Kampuni ya China Jiangsu International Economic and Cooperation Group, CJI, sasa inataka kupanua shughuli zake ndani ya bara la Afrika katika sekta ya mali isiyohamishika.

    Kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza biashara zake Africa kwa miaka 30 iliyopita huku ikishughulika hasa katika miradi ya msaada wa kigeni pamoja na uhandisi wa kimataifa.

    Kwa mujibu wa takwimu, soko la Afrika inaonekana kuupokea uwekezaji zaidi kutoka China. Na sasa China Jiangsu International imetangaza itapanua shughuli katika bara hili kwa mujibu wa serikali ya rais Xi Jinping kuhusu mkakati wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na pia "upenyezi wa kimataifa".

    Ni kwa sababu hii naibu rais wa kampuni hiyo ya CJI Gu Yuesheng alitangaza alhamisi kwamba kampuni yake itazindua miradi ya maendeleo ya mijini nchini Kenya na Msumbiji.

    "Kuna mahitaji makubwa katika sekta ya mali isiyohamishika. Sisi tumechambua mapungufu. Nasasa tunataka kujaza mapengo haya". Alisema bwana Gu.

    Akiwahutubia waandishi wa habari kutoka barani Africa katika ofisi ya kampuni hiyo jijini Nanjing, Mkoani Jiangsu, bwana Gu alisema kampuni hiyo itaanza uwekezaji katika sekta hii nchini Kenya kabla ya kuelekea Msumbiji, huku akifichua kuwa wawakilishi wa kampuni hiyo tayari wako jijini Nairobi kukamilisha mikataba mbalimbali kabla ya uzinduzi rasmi.

    "Utafiti wetu unaonyesha kuwa kuna soko kubwa nchini Kenya. Sisi tulichagua Nairobi kama hatua ya mwanzo kwa sababu hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Kenya ni imara. "Alisema

    Baada ya kusajili mafanikio katika shughuli zake kwa nchi 15 za Afrika katika kipindi cha muda mrefu, Gu alielezea imani yake kuwa mradi huu mpya hautakuwa tofauti.

    "Tulishatambua viingilio na tuna siri kuhakikisha mafanikio yetu katika sekta hii." Aliongeza.

    Mwezi uliopita, kampuni mbili za Kichina, China National Aero-Technology International Engineering Corporation na Jiangxi Water & Hydropower Construction Co Ltd, zilitangaza kuwekeza mabilioni ya Dola za Marekani katika ujenzi wa Two Rivers Investment Mall jijini Nairobi.

    Fani hii mpya kwa makampuni ya Kichina barani Afrika imeibuka huku naibu huyo wa rais was CJI akiziondolea lawama makampuni ya Kichina yanayoendeleza shughili barani Afrika kwa madai ya uagizaji wa wafanyakazi wake kwa gharama ya wenyeji.

    "Uwiano wa Kichina kwa wafanyakazi wa ndani katika makampuni yetu nje ya nchi ni moja kati ya kumi (1:10). Wakati mwingine ni moja kwa hamsini (1:50). Hii inaonyesha wazi kuwa makampuni ya Kichina inawaandikisha kazi watu zaidi kutoka jumuiya ya maeneo yao ya kazi. "Alisema.

    Alisisitiza kuwa wawekezaji wa Kichina wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni wanazingatia wajibu wa kijamii kama ilivyoainishwa na rais Xi Jinping wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako