• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Kenya na China kukamilisha makubaliano ya ujenzi wa barabara mpya

    (GMT+08:00) 2017-03-29 15:32:36

    Eric Biegon in Jiangsu, China

    Kikosi cha maafisa wa serikali ya Kenya wako China kukamilisha mikataba kuhusiana na sheheni ya mwisho ya makocha ya abiria na mizigo zitakazotumika karibuni mara tu reli ya kisasa inayojengwa kutoka Mombasa kuelekea Naivasha itakapozinduliwa

    Wakizungumza baada ya kuzuru kampuni ya China Railway Rolling Stock Corp (CRRC) iliyoko Qishuyan, mkoani Jiangsu, maafisa hao walifichua kwamba wako katika mbio dhidi ya muda ili kuhakikisha makocha na injini zitafika mapema tayari kuanza shughuli tarehe 1 Juni 2017 kama ilivyoratibiwa.

     

    Kwa mujibu wa Kibaara Kaigu, ambaye ni sehemu ya ujumbe, tarehe ya mwisho ya mwezi Juni inakaribia kwa kasi na kuna haja ya kuhakikisha kila kitu inaendelea vizuri kwa mujibu wa ratiba.

    "Tumekuja kuangalia hatua zilizopigwa kuhusiana na injini ya mizigo na makocha yaliyosalia kuhakikisha zitafika Kenya kwa wakati kwa ajili ya uzinduzi." Alisema

     

    Ni hapa ambapo alitoa maelezo zaidi kuhusu hatua ambayo mchakato huo umepiga.

    "Kwa sasa yanafanyiwa mjarabu. Yanafanyiwa marekebisho ya mwisho ili kuhakikisha kila jambo liko shwari." Bwana Kibaara alisema

    Kikosi hicho ambacho wengi wao ni viongozi kutoka idara ya kiufundi ya Kenya Railways na wengine wenye kufanya nyaraka, walifichua kuwa wako chini ya sharti kali kuhakikisha kwamba mtandao wa reli utaanza kuendesha shughuli zake kwa muda wa miezi miwili zijazo bila matatizo.

    "imetubidi tuje tuangalie hatua zilizopigwa. Ingawa sisi tumehakikishiwa kuna maendeleo makumbwa katika shughuli hii tunataka kuthibitisha yote ni sawa. Hatutaki kubahatisha lolote." Alisema

    Kibaara, ambaye pia ni mtayarishaji mfululizo katika Idara ya huduma ya filamu ya Kenya, alisema kuwa makocha zilizonunuliwa ni ya makundi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya watu wote.

    "Tunatarajia kwamba wakati VIPs (Watu mashuhuri) watasafiri, kutakuwa na kocha mteule kwa ajili yao na wengine pia. Hii ikiwa ni pamoja na makocha ya rais." Aliongezea bwana Kibaara

    Hata hivyo alifutilia mbali hofu kwamba kila kitu hakitakuwa tayari kwa muda itakapofika tarehe ya mwisho iliyowekwa ya Juni.

    Alisema kwamba kampuni ya Kichina ambayo imepewa mkataba kuhusu magari ya reli ina uwezo mkubwa kushughulikia oparesheni ya mizigo na abiria akisema rekodi yake inaelezea.

    Kampuni ya China Railway Rolling Stock Corp kufikia sasa imetuma injini 12, makocha ya abiria 32, na makocha ya mizigo 60.

    Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa Kenya Railways Atanas Maina, reli hiyo mpya itanyanyua uchumi wa nchi na kusaidia kushughulikia msongamano barabarani.

    Ujumbe huo pia ulitembelea Chuo Kikuu cha Jiaotong mjini Beijing ambapo wanafunzi 60 kutoka Kenya wanaendelea na mafunzo ya shughuli za reli.

    Chuo hicho ni maarufu sana kwa ajili ya mafunzo ya kiwango cha juu katika masomo ya jumla ya usafiri kote duniani.

    Wanafunzi hao wanapokea masomo hayo chini ya mpango wa udhamini wa kampuni ya China Communications Construction Company ambayo inalenga kutoa mafunzo kwa wakenya 100 katika masomo reli.

    Udhamini huu wa CCCC, kama inavyofahamika, ni mojawapo ya ahadi ya serikali ya China ya kudhamini wanafunzi elfu moja (1000) kutoka Kenya kwa ajili ya masomo ya shahada ya kwanza katika China kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako