• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawekea Afrika dola za Marekani bilioni 34

    (GMT+08:00) 2017-03-29 15:33:20

    Na Theopista Nsanzugwanko

    Uwekezaji wa China katika nchi za Afrika umefikia kiasi cha dola za Marekani bilioni 34 ikiwa ni mara 60 ya ilivyokuwa imewekeza kwa mwaka 2000.

    Aidha, kutokana na ushirikiano mzuri wa kibiashara Afrika imeendelea kuwa soko kubwa la bidhaa kutoka China.

    Mkurugenzi wa Idara inayohusu nchi za Asia Magharibi na Afrika katika Wizara ya Biashara ya Jamhuri wa Watu wa China,Dong Wang amesema hayo wakati wa mkutano wa wizara hiyo na Waandishi wa habari kutoka Afrika walio katika kituo cha Mawasiliano ya habari kati ya China na afrika.

    Amesema takwimu hizo ni za mwaka 2015 huku katika sekta ya biashara zinazofanywa kutoka China Kwenda Afrika ni dola za Marekani bilioni 220.

    Amesema kwa takwimu hizo inaonyesha kwa jinsi gani uhusiano baina ya China na Afrika unavyozidi kukua kwa kasi hasa katika maeneo ya biashara na uwekezaji.

    Wang amesema kwa kipindi hicho wameendesha program mbalimbali zaidi ya 1,000 ambazo zimesaidia kutoa mafunzo kwa waafrika zaidi ya 8,000 katika Nyanja mbalimbali ikiwemo viwandani,ujenzi wa miundombinu na mengineyo.

    Alisema kutokana na mahusiano mazuri baina ya pande mbili hizo licha ya kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi duniani kwa mwaka 2016 mauzo ya bidhaa yameongezeka kwa asilimia 40 ambayo ni dola za marekani bilioni 3.3 licha ya kuwa hali ya uchumi haikuwa nzuri lakini imesaidia kukua kwa uchumi wa Afrika.

    Amesema kwa kutumia Jukwaa la ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) na kufanya mkutano wao kwa mara ya kwanza mwaka 2015nchini Afrika Kusini waliweka mikakati ya mawaziri kukutana na kuweka mikakati ya utekelezaji wa masuala mbalimbali kulingana na mahitaji ya nchi na wameishafanya mikutano miwili.

    Amesema katika fedha zilizohaidiwa na Rais wa China ,Xi Jinping kwa Afrika katika mkutano wa jukwaa hilo ambalo ni dola za Marekani bilioni 60 zilielekezwa katika masuala mbalimbali ikiwemo viwanda, Kilimo, miundombinu, uwekezaji ,biashara fedha pamoja na ulinzi na usalama.

    Wang amesema asilimia 50 ya fedha hizo tayari zimepelekwa katika miradi mbalimbali kulingana na kipaumbele za nchi husika huku China akiangalia masuala mbalimbali kama mradi huo ni kwa maendeleo endelevu,kuleta maendeleo ya wananchi pamoja na kuwepo mazingira bora ya uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako