• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yashiriki Maonesho ya Utalii China na kudhamilia kuongeza idadi ya watalii

    (GMT+08:00) 2017-04-04 15:58:46

    Na Theopista Nsanzugwanko,Beijing

    TANZANIA imeshiriki kwa mara ya tano katika maonesho ya China Outbound International tourism Travel Exhibitio na kuweka mikakati ya kusaka soko la watalii nchini hapa na kuingiza watalii 300,000 kwa mwaka .

    Katika maonesho hayo Tanzania iliwakilishwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro,Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Kampuni Nne binafsi.

    Kiongozi wa Msafara kutoka Tanzania ambaye ni Naibu Mhifadhi kutoka Hifadhi ya Ngorongoro,Nicholaus Bangu alisema kwa miaka mitano Tanzania imeshiriki katika maonesho hayo.

    Alisema lakini mwaka huu imekuja kwa kudhamiria jinsi ya kupata soko la watalii chini humo kutokana na kuwa licha ya China kuwa na watalii wengi wanaotembelea nchi mbalimbali wanaofika Tanzania ni wachache.

    Alitoa mfano kwa mwaka jana watalii milioni sita kutoka China walisafiri nje ya nchi hiyo kufanya utalii lakini kwa Tanzania walitalii 20,000 pekee.

    Bangu alisema wameanza kufikiria kutumia sherehe za Wachina za mwezi Oktoba na Februari kutangaza vivutio vya utalii nchini ili mpaka mwakani kutoka watalii hao 20,000 hadi kufikia 100,000 na ikifikika mwaka 2025 wawe wamefikia watalii 300,000 wanaingia nchini kutoka China.

    Bangu alisema katika wiki moja waliyokuwepo nchini humo,Balozi wa Tanzania nchini China ,Mbelwa Kairuki amewasaidia katika kuweka mikakati ya kupata watalii nchini China.

    Alisema wameweza kukutana na wadau wa utalii nchini China waliotoa mawazo mbalimbali kusaidia kuongeza idad ya watalii Tanzania ikiwemo kutafuta namna ya kupunguza gharama za usafiri,kujitangaza katika mitandao ya kijamii nchini China,kutumia wasanii au watu maarufu China kutangaza vivutio vingi vilivyopo Tanzania .

    Alisema wakiwa katika maonesho hayo,banda la Tanzania limetembelewa na wananchi wengi wa China kutaka kufahamu utalii wa Tanzania na kuuliza kama utalii uko mwaka mzima kutokana kuwa wakenya wameelezea utalii wao ni kuhama kwa nyumbu kwa makundi kwa muda Fulani lakini Tanzania wanazunguka muda mrefu.

    "Kuna wachina wameaminishwa kuwa kama unataka kuwaona wanyama ni lazima kwenda muda fulani lakini kimsingi sisi tumefuta hiyo kwa kueleza watalii toka China kuwa Tanzania unaweza kwenda muda wowote na kuwaona wanyama"alisema

    Alisema pia watoa huduma za utalii wameuza kazi zao kwani kuna mtoa huduma mmoja amepata wateja 40 na makundi yanayotaka kuja kwa wingi.

    Naye,Ofisa Utalii wa Bodi ya Utalii,Irene Mville alisema masoko yanayoongoza kwa kuleta watalii ni nchini ni Marekani,Uingereza na Ujerumani lakini soko la China ni soko linalokuwa kwa kasi kwa takwimu muongezeko wa watalii ni mkubwa.

    Alisema kabla ya miaka mitano iliyopita watalii walikuwa wachache lakini miaka miwili tu wamefikia 20,000 hivyo nchi ikiongeza bidii katika soko la chini kuna uwezekano wa kuongeza watalii.

    Mville alisema watalii wa China wanawalenga wake watu wa kipato cha juu na kati katika miji mikuu ya china na kumekuwa na changamoto ya gharama ya usafiri sababu ya kutokuwepo kwa ndege ya moja kwa moja kutoka China mpaka Tanzania.

    Maonesho hayo ni mara 13 kufanyika na Tanzania imekuwa ikishiriki kwa miaka mitano mfululizo kwalengo la kutengeneza fursa kukutana na wafanyabiasha wa masuala ya utalii na wananchi wan chi hiyo kuelezea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako