• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vinyago zaidi ya 510 toka Afrika vyavutia Makumbusho ya Taifa China

    (GMT+08:00) 2017-04-05 10:19:07

    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    SANAMU na Vinyago zaidi ya 510 kutoka katika nchi za Afrika zimechaguliwa kuwekwa katika Makumbusho ya Taifa ya China.

    Utamaduni huo kutoka katika nchi zaidi ya 10 za Afrika ya kati, Afrika Magharibi na Kusini mwa jangwa la Sahara nyingi zinamuhusu binadamu na mazingira ya Afrika yanayomzunguka.

    Waandish wa habari kutoka katika nchi za Afrika waliopo nchini China katika kituo cha mawasiliano ya Habari kati ya China ba Afrika (CAPC) Programu maalum walitembelea makumbusho hiyo na kukutana na uchongaji huo wa asili huku kila mmoja akitafuta kutoka nchini mwake.

    Kati ya maswali waliyojiuliza ni kwa jinsi gani vinyago hivyo vilifika nchini humo na kuwekwa katika makumbusho hiyo ambayo wengi wanaamini ilipaswa kuwekwa kumbukumbu za China Pekee.

    Naibu Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo,Bai Yuntao anaeleza kuwa sanamu na vinyago kutoka Afrika zilizochaguliwa kuwekwa katika makumbusho hayo zilipatikana kutokana na ufadhili wa mchina Xie Yanshen aliyezipeleka katika makumbusho hayo zikiwemo sanamu, vinyago na makala mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kila siku.

    Yuntao anasema hatua ya kuwepo kwa sanamu za asili kutoka nchi mbalimbali za Afrika kunafanya watu mbalimbali kufika na kupiga picha katika sanamu hizo zenye mvuto wa aina mbalimbali na zimewekwa katika makumbusho hayo ili kuonesha ushirikiano uliopo baina ya China na nchi za Afrika.

    Nchi zenye sanamu hizo kwa wingi ni pamoja na Nigeria, Mali, Ghana, Siera leone, Mali, Cameroun, Senegal, Togo na nyinginezo.

    Licha ya kuwepo kwa tamaduni hizo muhimu katika makumbusho bado hakuna makumbusho yeyote ya nchi ya Afrika yenye ushirikiano na Makumbusho hiyo.

    lakini anasema nchi zote za Afrika zinaalikwa kuwasiliana na Makumbusho hayo kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika masuala ya utunzaji wa mila na tamaduni za nchi hizo ikiwa ni pamoja na kushiriki maonyesho ya kimataifa yanayofanywa na makumbusho hayo mara 10 kwa mwaka.

    Anasema makumbusho hiyo iliyoanzishwa mwaka 2003 ina ukubwa wa mita 192,000 na kumbi 48 zenye maonesho mbalimbali huku kukiwa na vipengere zaidi ya milioni 1.4 ya vitu vinavyoonyeshwa.

    Alisema makumbusho hiyo ina website ambayo inaonesha vitu mbalimbali huku ikisomwa na watu zaidi ya milioni nne lakini bado wanahitaji kuona kwa mambo kuliko katika mtandao hivyo kufanya kupata watu wengi wanaotembelea.

    Anasema katika makumbusho hiyo inatumika kama sehemu ya kujifunzia kwani asilimia 10 ya wanafunzi wanatumia kwa ajili ya mafunzo nje ya darasa wanayotakiwa kujifunza nchini humo.

    "Hatua hii inasaidia katika kuhamisha mila na tamaduni za kichina kwa vizazi vipya,ambapo watoto uuliza maswali kwa lengo la kufahamu kwa undani "alisema.

    Alisema katika makumbusho hayo yanatembelewa na watu zaidi ya 2000 kila siku,huku kukiwa na makumbusho nchini humo 3800 za serikali na 4,000 za binafsi ambazo nyingi zinalipiwa pale unapoenda kutembelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako