• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watanzania waanza kazi startimes China kukuza lugha ya Kiswahili na Tamaduni za Kichina

  (GMT+08:00) 2017-04-10 15:35:15

  Na Theopista Nsanzugwanko

  WATANZANIA sita walioshinda katika shindano maalum la ubadilishaji wa sauti "Dubbing" wameanza kazi katika kampuni ya Startimes Group ya nchini China kwa mkataba wa kuanzia wa mwaka mmoja.

  Lengo la shindano hilo lilikuwa kupata watanzania 10 watakaofanya kazi kwenye kampuni hiyo kubwa kwa ajili ya kukuza Kiswahili na kupeleka tamaduni za Kichina nchini Tanzania na nchi nyingine zinazozungumza Lugha ya Kiswahili.

  Watanzania hao walikutwa wakiendelea na kazi, mara baada ya waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika kutembelea kampuni hiyo kuona jinsi inavyofanya kazi.

  Makamu wa Rais wa Startimes Communication Network Technology Group, Ziqi Guo anasema hatua ya kuchagua Tanzania kuendesha shindano hilo la kuwapata watu wa kufanya kazi hiyo limetokana na ushirikiano mkubwa na nchi hiyo na mikakati ya kukuza Lugha ya Kiswahili.

  Anasema watanzania hao wanafanya kazi ya kutafsiri na kuingiza sauti katika filamu au programu mbalimbali kwa Lugha ya Kiswahili na Kiingereza ikiwa ni mkakati wa kuimarisha ushirikiano.

  Anazungumzia Kampuni hiyo kuwa inaboresha huduma ikiwemo kutangaza habari za Afrika kwani wanatarajia kuanzisha Vituo vya Luninga na Radio vya kampuni hiyo ili kuongeza idadi ya habari mbalimbali.

  Alisema kwa habari za Michezo, wanaendelea kufanya mazungumzo na vyama mbalimbali vya michezo nkatika nchi mbalimbali za Afrika ambapo wana soko kubwa ili kuonyesha mchezo wa mpira wa Miguu pamoja na kuhakikisha wanaanza kuonesha michezo ya ligi za Ulaya.

  Watanzania sita waliokwishawasili na kuanza kazi ni Abdul Maisala, Happyness Stanslaus (Msanii maarufu ajulikanaye kama Nyamayao) Hilda Malecela na Abraham Richard kutoka jijini Dar Es Salaam na Safiya Ahmed na Rukia Amdani kutoka Zanzibar.

  Kiongozi wa watanzania hao, Richard anasema kwa mwaka mmoja watakuwa wamejifunza masuala mengi ya "Dubbing" kwani hapo wanatumia teknolojia za kisasa tofauti na nchini huku wakitarajia kujifunza tamaduni za nchi hiyo.

  Anasema mchakato wa kuwapata ulianza Septemba 10 mwaka jana na kushirikisha watu zaidi ya 2,000 na kupatikana 18 waliopatiwa mafunzo na kampuni ya Startimes Media ya nchini Tanzania.

  "Vigezo vikubwa walivyokuwa wakiangalia mwanzo kabisa ni sauti kwani waliliita kama shindano la vipaji vya sauti lakini baadaye waliongeza kiwango cha elimu kuwa angalau uwe na Diploma na umri wa kuweza kuajiliwa huku" anaeleza.

  Anasema baada ya hapo, walipatikana 10 lakini wenzao wawili walishindwa kuungana nao kutokana na kuwa na umri mdogo na sheria za kazi za nchi ya China ya kutoajili wasiokuwa na umri wa zaidi ya miaka 24 lakini kampuni hiyo imewapa nafasi ya kuja kutembea nchini humu.

  Anasema mmoja hakuweza kufika kutokana na masuala ya Chuo kwani yuko mwaka wa mwisho na mwingine kutoka Arusha anaendelea kukamilisha taratibu mbalimbali na atawalisi mwezi ujao.

  Anasema baada ya kufika wamepokelewa na kuanza kazi zao huku wakielezwa baada ya kufanya kazi vizuri na kama watapenda kuendelea kufanya kazi hapo wataongezewa mkataba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako