• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chemsha Bongo

    (GMT+08:00) 2017-04-14 17:52:40


    Je, unafahamu "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni kifupisho cha nini? Pendekezo hilo lilitolewa chini ya mustakabali gani na litaleta mchango gani kwa jumuiya ya kimataifa? Kuanzia Aprili 15 hadi Mei 5, Radio China Kimataifa imeandaa chemsha bongo kuhusu Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    (unaweza kuchagua majibu zaidi ya moja)

    1. "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni kifupisho cha mambo gani?

    A. Ukanda wa kiuchumi wa Njia ya hariri

    B. Njia ya hariri baharini ya karne ya 21

    C. Njia mpya ya hariri

    2. Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lilitolewa lini?

    A. Septemba 7, 2013, Rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la kujenga "Ukanda Mmoja na Njia Moja" mara ya kwanza wakati akihutubua kwenye chuo kikuu cha Nazarbayev nchini Kazakhstan.

    B. Oktoba 3, 2013, Rais Xi jinping wa China alitoa pendekezo la kujenga "Njia ya hariri baharini ya Karne ya 21" wakati akihutubia Bunge la Indonesia.

    3. Ushirikiano wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" una vipaumbele gani?

    A. Mawasiliano ya kisera

    B. Muunganiko wa barabara

    C. Urahisishaji wa biashara

    D. Mabadilishano ya sarafu

    E. Maelewano kati ya watu

    4. Kanuni za ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni nini?

    A. Kujadiliana kwa pamoja

    B. Kujenga kwa pamoja

    C. Kunufaika kwa pamoja

    5. Hivi sasa, "Ukanda Mmoja na Njia Moja" una shoroba gani za kiuchumi za kimataifa?

    A. China, Mongolia na Russia

    B. Daraja jipya kati ya mabara ya Asia na Ulaya

    C. China – Asia ya Kati – Asia ya magharibi

    D. China – Peninsula ya Indo China

    E. China na Pakistan

    F. Mongolia, China, India na Myanmar

    Njia za kushiriki kwenye Chemsha Bongo:

    1. Kujibu maswali yaliyotolewa kwenye bandiko la Chemsha Bongo katika tovuti au ukurasa wetu kwenye facebook https://www.facebook.com/kiswahilicri/posts/1132710656840246  barua pepe: kiswahili@cri.com.cn

    2. Kutoa maoni, kutuma kwa wengine, kubofya "Like" kwenye bandiko la Chemsha Bongo katika tovuti au ukurasa wetu,

    3. Kutuma maandishi, picha au video vinavyohusiana na "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kupitia akaunti yako binafsi kwenye mitandao ya kijamii, na vilevile kuwatumia wengine bandiko la Chemsha Bongo kwenye tovuti au ukurasa wetu.

    Shiriki kwenye Chemsha Bongo, Shinda Tuzo mbalimbali! Usikose!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako