• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing yatetea ubora wa bidhaa Kutoka China

    (GMT+08:00) 2017-04-20 09:41:33
    Beijing yatetea ubora wa bidhaa Kutoka China

    Na Eric Biegon, Guangzhou China

    Ubora wa bidhaa zinazotengenezwa kutoka China na kusafirishwa sehemu nyingi duniani, daima zimepokelewa kwa miitikio tofauti. Kwa mara nyingi bidhaa hizo zimedaiwa kuwa na ubora wa hali duni. Afrika kwa upande mwingine imetajwa kuwa mahala ambapo bidhaa hizo zinarundikwa.

    Sifa hii isiyo ya kupendeza, bila shaka, imechukiza serikali ya China. Usimamizi wa Beijing umetetea vikali ubora wa bidhaa kutoka China huku ukisisitiza kuwa ni ya hali ya juu.

    "Bidhaa za Kichina zina ubora wa juu. Kwa kweli ubora huu unaendelea kuboreka. Bidhaa nyingi zaidi kutoka China zinaendelea kusafirishwa mataifa ya nje." Afisa katika idara ya huduma ya mambo ya nje wa nchi hiyo alisema.

    Hata hivyo, utawala huo wa Beijing umekiri kuwa unatambua kwamba kuna wafanyabiashara na watu binafsi, wote kutoka China na Afrika, waliowepesi kutafuta faida ya haraka.

    "Sisi hatufurahi kuona kwamba baadhi ya bidhaa sisizo na ubora kamili zinasafirishwa Afrika. Hakika tunakerwa na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizo. "Alisema bwana Luo Jun, ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Nje mkoani Guangdong.

    Huku ukidhihirisha kukasirishwa na hali hii ya mambo, serikali ya China unadai kuwa taifa hilo inaumia pakubwa sawia na nchi zinazoendelea barani Afrika na mataifa mengine yaliyoathirika duniani kutokana na biashara hiyo.

    "Bidhaa hizo kwa kiwango kikubwa zinachafua mazingira yetu pamoja na kudhoofisha sifa nzuri ya bidhaa za China." Yeye alilalama. Afisa huyo alithibitisha kuwa miaka michache iliyopita imeshuhudia kuongezeka kwa gharama za kazi na athari zake kwa ujumla ni kuwa bei ya bidhaa zimepanda. Ili kujipatia fedha za haraka, baadhi ya watu wanauza nje bidhaa za ubora wa hali ya Chini barani Afrika.

    Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Guangzhou, bwana Luo alisema kuwa China imeweka sheria inayotoa adhabu kali kwa yeyote anayehusika na biashara ya bidhaa duni kwani ni kosa la jinai.

    Kwa maoni yake, itakuwa vigumu sana kwa mtu kutenda kosa na kuepuka kirahisi huku akifutilia mbali madai kwamba China inakosa mfumo wa kukabiliana na uhalifu huu.

    "Kwa sasa bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi zinachunguzwa na Utawala Mkuu wa Ubora, Usimamizi, Ukaguzi na Karantini ya China (AQSIQ). Kila mfanyabishara ni lazima apate hati ya asili."Alisema.

    Waraka huu kwa mujibu wa mamlaka ya Kichina ni lazima kwa watu wote wanaoshiriki katika mauzo ya nje ya bidhaa. Na hii ndio sababu kuu hasa ya Beijing kutoa wito wa tahadhari kwa maafisa wa forodha katika nchi ambazo zimefungua milango yake kwa bidhaa kutoka China.

    "Katika mipaka, tunataka mamlaka iangalie bidhaa. Lazima iangalie cheti yao ya asili. Wajue ni wapi zilikotoka. Kama zina rekodi mbaya tujulishwe." Yeye alisema.

    "Bidhaa duni yasiruhusiwe kuhamishwa. Cheti cha asili ni muhimu sana. Kama hakuna hati ya asili imetolewa, bidhaa hizo lazima zifungwe." Bwana Luo aliongeza.

    Lakini kuna changamoto nyingine kwani inaonekana kwamba inazidi kuwa ngumu kuthibitisha bidhaa binafsi na zile na kufanyiwa biashara.

    "Bado tuna matatizo. Watu wanatuma bidhaa kutoka China kuelekea Afrika kwa barua kwa njia ya vifurushi. Haya hayaangaliwi kama bidhaa ya kibiashara. Hati ya asili haitakikani." yeye alisema.

    Hata hivyo idadi kubwa ya wale wanaotuma bidhaa kwa njia hii yaonekana hawaneni ukweli. Kulingana na yeye baadhi ya watu wanadai kutuma vifurushi kwa familia na hakuna haja ya kuangalia.

    Yeye anatahadharisha kwamba kila mtu lazima awe macho na mwangalifu hasa bei ya bidhaa unaokithiri unapokuwa mdogo mno.

    Lakini mbali na bidhaa duni, changamoto nyingine kubwa inayokabili China na bidhaa zake ni bidhaa bandia. Taasisi za umma zinahofia kwamba baadhi ya bidhaa zimepewa alama ya usajili ya Kichina ilihali asili yake si ya Kichina.

    Hili kupambana na biashara hii haramu, China ilipitisha sheria ya utawala na makosa ya jinai.

    Mbinu za utawala inahusika hasa katika hali ambapo kiasi kidogo cha fedha inahusika. Hapa, utawala unaweza kutoza adhabu wanaopatikana na hatia. Kwa mfano, unaweza kutwaa bidhaa bandia, au kutoza faini ndogo kwa wanaoueneza.

    Mbinu ya Jinai inashughulikia matukio yanayohusiana na kiasi kikubwa cha fedha. Kesi hizi huonekana kama uhalifu mkubwa na watu wanaohusika wanapata adhabu kali ya jinai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako