• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya kijamii yaliyojitolea kusaidia Waafrika Kuishi China

    (GMT+08:00) 2017-04-24 08:50:36
    Na Eric Biegon, Guangzhou China

    Ni jinsi gani Waafrika ambao husafiri nje ya nchi katika kutafuta malisho mazuri hufanikiwa kuishi kati ya watu wageni kutoka asili mbalimbali pamoja na tamaduni tofauti?

    Kukubaliana na hali ya maisha katika nchi ya kigeni, kama wengi walivyogundua, si rahisi. Hali hii ya mpito wakati mwingine ni ya kuvutia lakini lakini ni ya kutoa kijasho. Mara kwa mara, wale waliosafiri nje ya mataifa yao Afrika wanakabiliwa na matatizo unaosababishwa na ukosefu wa ufahamu wa msingi wa watu na taratibu katika nchi mwenyeji.

    Katika China, idadi kubwa ya taasisi zimeanzishwa kwa madhumuni ya kusaidia wageni wanaosafiri kuelekea taifa hilo la mashariki mwa dunia kwa shughuli mbalimbali. Moja ya mashirika hayo ni Dengfeng Community Family Integrated Services Center. Lengo lake ni kuhakikisha kwamba mtu yeyote anayesafiri kwenda China lazima ajisikie nyumbani.

    Rekodi katika taasisi hii inaonyesha kwamba idadi kubwa ya raia wa kigeni, katika Guangzhou kwa mfano, wanatoka Afrika. Zaidi ya Waafrika 7000 tayari wapokea msaada kutoka shirika hili.

    "Watu wengi kutoka Afrika huja China, hasa Guangzhou, kufanya biashara na kufanya kazi. Wengine huja kuendeleza masomo yao. kazi yetu ni kuwafanya imara kama iwezekanavyo."Akasema Bw Hai Ge Wang, ambaye ni mfanyakazi wa jamii katika Guangzhou, Mkoa wa Guangdong.

    Bwana Hai Ge, anasema lengo kuu la DCFISC ni kuwawezesha wote wanaotafuta msaada kutoka kwake kupata zana muhimu na ujuzi ili kukabiliana na changamoto ambayo kwa urahisi huja na kuishi katika sehemu nyingine kando ya nyumbani.

    "Wageni wanaoishi katika Guangzhou wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na mambo kama jinsi ya kuomba visa ya Kichina na kibali cha makazi, kutafuta makazi na kupata matibabu. Kwa hiyo, sisi tunawaandaa na kuwasaidia kwenda kuweza kushughulikia masuala haya." Yeye alisema

    Masomo ya Lugha ya Kichina ya bure

    Hata hivyo Lugha inaonekana kuwa kizuizi kikubwa juu ya changamoto zinazokabili mtu kusafiri kwenda China kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wake huzungumza Kichina. Kuvunja kikwazo hii, kundi la jamii la Dengfeng inatoa masomo ya msingi wa lugha ya kichina kwa raia wa kigeni bila malipo.

    "Mafunzo ya lugha ni muhimu sana. Tunawafundisha lugha hili waweze kuelewa jinsi ya kuwasiliana na kufanya biashara. Madarasa ya Kichina huanza kutoka Jumatatu hadi Ijumaa. Sisi huwafundisha jinsi ya kuelewa lugha ya Kichina kwa urahisi na haraka zaidi." Alifichua bwana Hai Ge.

    Ili kukwepa changamoto ya afya ambayo huwapata wanaoishi nje ya nchi, kundi hilo linaandaa mihadhara kuwafundisha kuhusu afya na huduma zinazopatikana za matibabu.

    Utamaduni Tofauti

    Bwana Hai Ge, ambaye pia ni msimamizi wa mradi huo, hata hivyo anafichua kuwa changamoto kubwa inayolikabili shirika hilo ni kujaribu kuweka daraja kwa sababu ya kutoelewana kiutamaduni ambayo wakati mwingine hufanyika kati ya wageni na wenyeji. Kupatanisha asili hizi mbalimbali za kitamaduni imemlazimisha yeye na kundi lake kuanzisha miradi ili kukuza jitihada hizi.

    "Sisi huandaa burudani, sherehe, matumbuizo ya gitaa na michezo ya soka. Tunatumia vikao hivi kutoa nafasi ya wao kuwasiliana na kushirikiana na watu wa ndani. Hii inawasaidia kuelewa kila mmoja zaidi na zaidi na kuondoa mvutano baina yao." Bwana Hai Ge alibainisha.

    Masuala ya sheria na utaratibu haiwezi kupuuzwa katika hali hii kutokana na kwamba wengi wamejikuta katika upande mbaya wa sheria angalau bila kujua.

    Afisa huyo anasema wafanyakazi wa kijamii katika Dengfeng huandaa mihadhara kwa ajili ya kundi hilo ili kuwasaidia kuelewa sheria ya Kichina. Kwa kufanya hivyo wanajifunza nini ni halali na nini ni kinyume cha sheria. Hii, anasema, ni kwa ajili ya mema yao wenyewe kwani hali katika nchi tofauti si sawa daima.

    Lucy Njoki, kutoka Kenya, ni mfanyabiashara katika moja ya maduka katika Guangzhou, na alinifichulia kwamba ingekuwa vigumu sana kwa ajili yake kukaa katika wilaya hiyo kusingekuwa na DCFISC.

    "Wao walifanya mabadiliko yangu rahisi kuliko mimi nilivyotarajia. Walinifundisha hali ya maisha ya Kichina juu ya kunifundisha lugha yao. Sasa naweza kufanya biashara yangu kwa uhuru." Yeye alisema.

    Dengfeng Community Family Integrated Services Center hata hivyo haipo peke yake katika safari hii. Idadi kubwa ya mashirika nchini China ya umma au yasiyo ya kiserikali yameanzishwa kushinikiza ajenda hii mbele.

    Katika mji mkuu wa China, shule ya Beijing International Chinese College (BICC) imekuwa ikisaidia vikosi vya wanadiplomasia na wageni ambao muda wao ni mrefu katika China. Haitoi tu masomo ya lugha ya Kichina, lakini imesifika katika kuwapa elimu juu ya mila ya Kichina na utamaduni.

    Kutembelea nchi hiyo yenye utajiri wa maeneo ya torathi imekuwa rahisi kwa njia ya msaada wa wataalamu wanaofanya kazi katika hii taasisi iliyo ya hali ya juu sana.

    Taasisi hizi hakika zimefanya kusafiri na kuishi China kuwa ya kuvutia, na kupunguza matatizo yatokanayo na mbio na zogo la kujaribu tu kukaa na kuishi katika nchi ya kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako