• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Droni za Kilimo kutoka China kunufaisha wakulima

    (GMT+08:00) 2017-04-26 14:22:41
    Na Eric Biegon, Guangzhou China

    Sekta ya kilimo inaendelea kupitia mabadiliko mengi. Kuongezeka kwa idadi ya watu duniani inatoa wito wa kuongeza uzalishaji wa chakula. Hata hivyo ahadi hii inaandamwa na vikwazo chungu nzima.

    Changamoto hizi zimeendelea kupanda na mwishowe imesababisha mapinduzi ya viwanda, ambayo ilizaa mageuzi ya kilimo. Kilimo rahisi imebadilika na kuwa endelevu na kuhitaji jitihada kubwa ambayo sasa inashirikisha vifaa vya kisasa.

    Kampuni ya Kichina Dajiang Innovation, maarufu kama DJI, imejiunga kwenye orodha kubwa ya taasisi yenye nia ya kutoa ufumbuzi dhahiri katika sekta hii.

    Uzalishaji wa droni za Raia

    Baada ya kuzinduliwa mwaka 2006, ikiwa na lengo kuu ya kutengeneza vyombo vya kuruka na kunakili picha ya mifumo, kampuni hii imehusika katika uzalishaji wa droni za raia. Hadi sasa imeweza kutengeneza miundo tofauti ya vyombo hivyo ambavyo vinatumika kwa kiasi kikubwa katika upigaji picha na utayarishaji wa filamu. Droni maarufu aina ya Phantom ni mojawapo ya vifaa hivyo.

    Lakini baada ya miaka 10 katika biashara, kampuni hiyo umezidisha shughuli zake, huku ikipanua mtazamo wake kama hivi karibuni ilipozindua droni ya kilimo kwa mara ya kwanza. Mashine hii, Agras MG-1, huendeshwa kama droni, na imedhamiriwa kufanya unyunyizaji wa dawa kwa mazao kwa njia nafuu, salama na yenye ufanisi zaidi.

    "Mchanganyiko wa kasi na nguvu kwa chombo hiki ina maana kwamba eneo la ekari 7-10 inaweza kunyunyizwa kwa urahisi na unaweza kufikiwa kwa muda wa chini ya dakika 10 tu. Hii ni mara 40 hadi 60 kwa kasi zaidi kuliko operesheni sawia na aina nyingine." Msimamizi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Oliver Wang alisema.

    Unyunyizaji Sahihi

    Kwa mujibu wa kampuni hiyo, hii droni ni mojawapo ya mashine bora zaidi kwa matumizi ya unyunyizaji angani ikilinganishwa na ndege ambayo yametumika kwa miongo wakati wa unyunyizaji wa madawa ya kuulia wadudu na unyunyizaji mbolea kwa mashamba makubwa ya mazao.

    Agras, ambayo gharama yake takriban Millioni 10 Dola za Marekani, imetengenezwa hasa kwa ajili ya kilimo cha mashamba makubwa, na kampuni ya Dajiang inasema wakulima watapata thamani ya pesa zao kwani mashine hii inatekeleza kazi kwa usahihi.

    "Droni inaweza kukagua ardhi chini na kudumisha umbali sahihi kutoka kwa mazao na kunyunyiza dawa kiasi sahihi ya kioevu. Tanki yake kita 10 ina uwezo wa kubeba maji ambayo yanaweza kunyunyiza sehemu kubwa ya ardhi." Bwana Wang alieleza

    Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ubunifu uliotumiwa kutengeneza kifaa hicho kinauwezesha kuongeza kasi ya dawa huku ikipanua sehemu itakayofikia katika mashamba makubwa. Vipengele muhimu vilivyoezekwa ndani ya chombo hiki kinauwezesha kutumika kwa maelfu ya masaa ya unyunyizaji wa dawa sahihi bila ya uharibifu.

    Kumbukumbu

    Lakini yaonekana faida kubwa inayotokana na chombo hiki ikilinganishwa na ndege zingine za kilimo ni uwezo wake wa kurekodi na kukumbuka viwianishi vya awali jinsi inavyoendelea kufanya kazi shambani.

    "Iwapo kifaa hiki kitasimama kutokana na itilafu, kwa mfano kutokana na kumaliza betri au kioevu dawa, unaweza kurejelea shughuli tena kwa urahisi kutoka hatua ya mwisho katika kumbukumbu yake baada ya kubadilisha betri au kujaza upya mizinga yake." Wang alifafanua.

    Akizungumza baada ya mkutano wa kuonyesha utendaji kazi wa kifaa hicho ya kisasa ya kilimo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, bwana Wang alibainisha kuwa Agras inafanya vizuri kwa mazingira tofauti. Anasema inatekeleza kazi nzuri katika ardhi ya eneo tambarare au kwenye misheni maalumu sana, ambapo anayeitumia anaweza kuiendesha katika hali ya mwongozo.

    Kwa maoni yake, bei ya chombo hiki inaonekana ghali kwa watu binafsi hasa katika mataifa ya Afrika. Hata hivyo anasema kuwa ikiwa itanunuliwa katika makundi au kwa makampuni, bei yake hatimaye inaonekana ndogo mno ikilinganishwa na kazi inayotekeleza.

    Kilimo kinachoongoozwa na data

    Zaidi ya hayo yote, DJI inasema kuwa chombo hiki ambacho zamani kilikuwa uvumbuzi wa technologia ya kijeshi, inaweza kutumika kukamata na kuzalisha data kuhusu mazao kwa njia ya kamera yake vyema.

    Picha za uangavu ambazo zimechukuliwa kutoka vyombo hivi vinaweza kuonyesha kila kitu kutoka kwa matatizo ya kilimo cha unyunyizaji hadi shida kwenye udongo. Aidha data hii inasaidia kupunguza matumizi ya maji na kemikali katika mazingira.

    "Sisi tunazingatia kutafuta miradi ambayo inawakilisha ubora na ubunifu zaidi juu ya soko na wateja wetu." Wang alisema

    Kwa maneno yake mwenyewe, wamiliki wa mashamba makubwa ya mahindi, chai, kahawa, ndizi, mananasi, mchele na ngano barani Afrika watafaidika zaidi kutoka uvumbuzi huu ambao unatumika kwa sasa Marekani, Japan, Korea na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako