• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daktari kutoka China aandika kitabu kueleza miaka 10 aliyoishi na kufanya kazi Afrika, wadau wataka kichapishwe kwa Kiswahili

    (GMT+08:00) 2017-04-27 09:01:09

    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    TATIZO la uhaba wa madaktari kwa nchi za Afrika, imekuwa likitatuliwa na serikali ya China kwa kupeleka madaktari na watendaji katika sekta ya afya wa kujitolea.

    Mmoja wa madaktari waliofika katika nchi hizo kutoka China na kufanya kazi kwa miaka 10 katika nchi tatu ameandika kitabu kuelezea maisha aliyoishi na kufanya kazi changamoto alizopitia, mwingiliano wake na waafrika pamoja na nini cha kufanya.

    Mwandishi wa kitabu hicho kilichozinduliwa wiki hii, Dk Minxian Wu (54) aliyezaliwa eneo la Fufeng, jimbo la Shaanxi alifanya kazi na kuishi Afrika kuanzia mwaka 2001 hadi 2015 akiwa ni mmoja wa timu ya madaktari waliopelekwa kutoa huduma katika nchi za Eritrea,Zambia na Ethiopia.

    Katika kitabu hicho alichokiita "My Ten Years in Africa", Wu ameelezea changamoto mbalimbali alizokabiliana nazo wakati akifanya kazi katika nchi za Afrika hasa katika maeneo ya wananchi wa kawaida, na jinsi alivyokabiliana na ugonjwa na malaria aliougua zaidi ya mara 10 pamoja na hali halisi ya utoaji huduma za afya katika nchi hizo.

    Wu ameandika kitabu hicho kikiwa ni cha pili baada ya cha kwanza alichokiita, "In a country where a Year has 13 Month" alichokiandika akiwa nchini Ethiopia kikielezea miezi 13 ya nchi hiyo ikiwa ni tofauti na kalenda zinazotumika katika nchi nyingi za Afrika.

    Wu ambaye ni daktari wa kwanza kutoka nchini humo kuandika kitabu kinachoelezea kazi hiyo Afrikaanasema amechapisha kitabu hicho kwa lugha ya kichina zikiwa nakala 4000.

    Anasemaka licha ya kuwa huduma za afya zinazidi kuimarika katika baadhi ya nchi Afrika bado kuna changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na kukua kwa teknolojia katika sekta ya Afya kila siku hivyo kuonesha tofauti kubwa kati ya nchi hizo na nyingine duniani ikiwemo China.

    Alishauri kuwa katika kukabiliasha na changamoto alizozieleza katika kitabu hicho ikiwemo uhaba wa watoa huduma za afya ni vema mamlaka zinazohusika na afya Afrika kuongeza ushirikiano na nchi mbalimbali duniani ikiwemo China.

    Naye naibu balozi wa China nchini Tanzania, Haodang Gou anashauri kitabu hicho na vingine vinavyohusu masuala ya ushirikiano wa Afrika na China kutafsiliwa kwa lugha ya Kiswahili.

    Anasema ushirikiano wa China na Afrika na hususan nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili ni wa muda mrefu na pia ili waafrika wengi wapate yaliyomop ni vema katika mipango ya kutafsiri kwa Kiingereza na kifaransa pia iwekwe na Kiswahili.

    Anatoa mfano wa kitabu kinachohusu mahusiano wa Tanzania na China katika ujenzi wa Reli kati ya nchi ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kuwa kinaendelea kutafsiliwa kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi wapate kuelewa mahusiano hayo.

    Gou anasema ni vema kutafsiliwa kwa Kiswahili sababu kuna watu zaidi ya milioni moja kutoka nchi za Afrika Mashariki hususan Tanzania Kenya, Uganda wanazungumza lugha hiyo.

    Gou anasema kwa kutumia kitabu hicho nchi za Afrika zihitajika kuongeza ushirikiano katika sekta ya Afya ili kuondokana na changamoto wanakabiliwa nchi hizo hususan ya watendaji katika afya.

    Anasema hiyo siyo haki kabisa kwani China inatoa elimu bora kuhusiana na masuala ya afya na madaktari wanaopelekwa kutoa huduma katika nchi za Afrika wamesoma katika vyuo hivyo na wanakubaliwa.

    Akizungumzia kitabu hicho, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Wafrika (AU) Dk Nkosazana Dlamini-Zuma anasema kitabu hicho ni cha kwanza kuandikwa na mmoja wa timu ya madaktari na wauguzi wanaofanya kazi Afrika tangu miaka ya 1960 wanaosaidia kuokoa maisha ya waafrika kwa kuwapatia matibabu.

    Hivyo anasema kwa niaba ya Kamisheni hiyo anashukuru kwa kusaidia Afrika na anatumai siko moja kitabu hicho kitachapishwa kwa lugha za Afrika ili iwe rahisi watu wake kuelewa kilichoandikwa katika kitabu hicho.

    Dakitari huyo ni miongoni mwa madaktari 20,000 waliofanya kazi katika nchi mbalimbali za kiafrika mpaka mwishoni mwa mwaka 2013 na kufanikiwa kuwapatia matibabu na vipimo wagonjwa zaidi ya milioni 300 katika maeneo tofauti hususan wale wa hali ya chini.

    Kwa sasa China imepeleka timu za madaktari katika nchi 49 duniani na kati ya nchi hizo 42 ni kutoka Afrika kwenye zile nchi ambazo bado maendeleo yake siyo mazuri hasa katika sekta ya afya, uchumi huku wakikabiliwa na vita, upungufu wa madaktari,vitendea kazi na madawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako