• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yajiunga na China wakati dunia umeweka uhai ndoto ya Mkanda Mmoja Njia Moja

    (GMT+08:00) 2017-05-19 09:42:35
    Na Eric Biegon, Beijing

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ni miongoni mwa viongozi 29 wa nchi zilizokongamana Beijing kupumulia uhai pendekezo la Mkanda Mmoja Njia Moja.

    Kongamano hilo la kimataifa la siku mbili, lilikuwa linafanyika kwa mara ya kwanza tangu ulipopendekezwa na rais wa China Xi Jinping mwaka wa 2013, na limetajwa kuwa ya mafanikio makubwa kutokana na kwamba nchi wanachama wamepitisha utaratibu ambao wao watashirikiana ili kufikia maendeleo ya pamoja.

    Katika tamko la pamoja lililotolewa na rais wa China baada ya mazungumzo ya pamoja, viongozi kutoka mataifa 30 zilizowakilishwa na mashirika tatu kuu za kimataifa waliazimia kupitisha mpango huo kuwa njia ambayo nchi 68 na mashirika ambayo yamejiunga yatashirikiana.

    "Sisi tunafahamu kwamba uchumi wa dunia unashuhudia mabadiliko makubwa, kwani inawasilisha mazuri pamoja na changamoto. Hili ni fursa ya nchi kuendelea kutafuta amani, maendeleo, na ushirikiano." Ilisema taarifa iliyosomwa na Rais Xi.

    Mradi wa Karne

    Katika hotuba yake ya ufunguzi, kiongozi huyo wa Kichina alisisitiza jukumu zima la mpango huo katika maendeleo ya dunia akilitaja kuwa "Mradi wa karne." Alitangaza kwamba serikali yake imeongeza ufadhili kwa mradi huo kwa jumla ya bilioni 8.7 dola za Marekani za kusaidia nchi na mashirika ya kimataifa ambazo zimejiandikisha katika mfumo huo.

    Xi, ambaye ni rais wa taifa lenye uchumi mkubwa wa pili duniani, hata hivyo aliweka bayana kuwa mataifa wanachama lazima zitilie mkazo kupunguza kupanda kwa umaskini.

    "Tunakaribisha ushirikiano wa baina ya nchi, pembe tatu, kikanda na kimataifa ambapo nchi zitatilia mkazo kutokomeza umaskini, kujenga ajira, kushughulikia madhara ya mgogoro wa kifedha wa kimataifa, kukuza maendeleo endelevu na kuendeleza soko ya viwanda na mabadiliko pamoja na mseto wa uchumi." Yeye alisema.

    Hisia zake zilipokea uungwaji mkono kutoka viongozi wa dunia ambao hadi sasa wameingia kwenye mpango huo. Hakika, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema mpango huo utafungua fursa zaidi ya biashara na uwekezaji kando na kuchochea mipango ya Afrika ya ushirikiano.

    "Mpango wa Belt & Road inatoa nafasi kwa bara letu kufanya mabadiliko ya dhana. Afrika baada ya kujipatia uhuru bado imekwama." Alisema rais Kenyatta.

    Akizungumza wakati wa kufungwa kwa kongamano hilo la kimataifa katika jumba la mikutano la kimataifa la Yangi Lake, Kenyatta alisema mpango huo umebeba maono ya ushirikiano wa muda mrefu. Kwa maoni yake, utaratibu wa Belt & Road una uwezo wa kuingiza "nguvu chanya" katika kukuza ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi iwapo Afrika itakumbatia fursa zinazotokana na mpango huo.

    Kwa sababu hiyo, Kenyatta aliwarai viongozi kutoka bara zima kukumbatia mpango huo huku akipongeza China kwa kuchukua jukumu kuu katika kupigania uchumi wa pamoja.

    "Kuwa sehemu ya Mkanda Mmoja Njia moja unaruhusu bara kuhamia jukwaa mpya, kwa njia ambayo kushirikiana kimataifa kunaruhusu kuongezeka kwa thamani, uvumbuzi, na mafanikio." alisema Rais Kenyatta.

    Kando na Kenya, taifa lingine ambalo liliketi katika jukwaa lile ni Ethiopia ambalo Waziri Mkuu wake Haile Mariam Desalegn alikiri kuwa nchi nyingi zinazoendelea, hasa katika Afrika, wanaendelea kutazama China kama mfano wa mafanikio ya kiuchumi na rafiki wa kuaminika katika mapambano dhidi ya umaskini na jitihada kwa ajili ya mafanikio.

    "Hatuhitaji kutazama mbali zaidi ya China kwa mafanikio yake katika kipindi cha miongo michache yaliyopita ili kufahamu faida ya mbinu wazi kwa ukuaji wa uchumi na ustawi." Alisema

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres pia alikuwa hapa. Yeye alitoa sifa nyingi kwa taifa la China kwa kusukuma mfumo huu wa kiuchumi kama moja ambayo itaharakakisha utambuzi wa Maendeleo ya Milenia.

    "China imekuwa nguzo kuu ya ushirikiano wa kimataifa. Mpango huu utasaidia nchi zinazoendelea kufikia ukuaji kwa haraka na kukidhi ajenda ya Umoja wa Mataifa wa maendeleo wa mwaka 2030." Bwana Gutteres alibainisha.

    Ndani mwa maazimio yaliyopitishwa wakati wa mkutano huo wa siku mbili, wanachama wahusika walihaidi kwa pamoja kujenga uchumi wa wazi, kuhakikisha biashara huru na umoja, kupinga aina zote za ulinzi ikiwa ni pamoja na katika mfumo wa ukanda mmoja njia moja.

    Miongoni mwa mambo mengine, mfumo huo hasa unasukuma uratibu wa sera, kuunganishwa kwa miundombinu na vifaa, misaada ya biashara, ushirikiano wa kifedha na mahusiano ya karibu ya watu.

    Haya yote, kwa mujibu wa China, yataafikiwa kwa njia ya mchakato wa mashauriano na juhudi ya pamoja, kwa lengo la kuleta manufaa kwa wote.

    Waandaaji wa mkakati huu wenye sura tano wanashikilia maoni kwamba vipengele hivi muhimu vitazaa jamii ya maslahi ya pamoja, jukumu la kushirikiana na siku za baadaye za pamoja kwa mataifa yaliyoko katika mfumo wa Belt & Road ambayo kwa sasa ina idadi ya pamoja ya watu bilioni 4.4.

    Kwa sura hii na kulingana na jinsi mambo yalivyo kwa sasa, Afrika inatazamia kunufaika kutokana na kwamba viongozi wa OBOR wameliangazia sana, huku kukiwa na wito kwa ajili ya kuimarisha miundombinu, taasisi na watu kwa watu kuunganishwa kati ya nchi.

    Kikao hicho hatimaye kilidumisha kuwa mataifa ambayo bado hayajaendelea, nchi isiyo na bandari zinazoendelea, visiwa vidogo na nchi ya kipato cha kati yanastahili shughuli maalumu ya kuondoa vikwazo ya maendeleo na kufikia ufanisi wa kuunganishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako