• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kuongeza wataalamu Afrika kupitia ushirikiano katika Elimu kati yake na China

    (GMT+08:00) 2017-05-22 09:53:44
    "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kuongeza wataalamu Afrika kupitia ushirikiano katika Elimu kati yake na China

    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    UKIFIKA nchini China katika miji mbalimbali utakutana na idadi kubwa ya waafrika wengi lakini licha ya kuwepo wafanyabishara wengi wao ni wanafunzi.

    Idadi kubwa ya waafrika katika vyuo mbalimbali nchini China inadhihirisha wazi kuhusu ushirikiano katika sekta ya elimu baina ya nchi za Afrika na China.

    Katika Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" pia sekta ya elimu imekuwa ikijikita kwa namna ya pekee kuongeza ushirikiano kwa serikali ya China kutoa ufadhili kwa wanafunzi kwa lengo la kuleta maendeleo.

    licha ya kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu pia imejikita katika masuala muhimu ya maendeleo kama Elimu,ikiwa ni pamoja na kubadilishana wanafunzi kwa serikali ya China kupitia Rais wake ,Xi Jinping wamezindua program ya ufadhili kwa wanafunzi 30,000 katika miaka mitatu.

    Mpaka sasa kuna wanafunzi 60,000 kutoka nchi za Afrika ambao wanasoma nchini China katika vyuo mbalimbali vya Nyanja mbalimbali ikiwemo Udaktari tena ule wa tamaduni ya asili ya China na nyingine mbalimbali.

    Mkurugenzi katika idara ya ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana wanafunzi katika Wizara ya elimu,An Yan anasema kwa kutumia program mbalimbali zilizowekwa na China wanafunzi kutoka Afrika waekuwa wakiongezeka kila mwaka.

    Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika wizara ya elimu, Tao Xu anazungumzia program ya 20+20 iliyoanza mwaka 2009 ambayo kwa sasa wanahusika katika kubadilishana walimu na wanafunzi kutoka Afrika na China.

    Anasema program hiyo inafadhiliwa na serikali ya China kwa kila kitu na vyuo kutoka Africa vilivyochaguliwa katika program hiyo vinafadhiliwa kwa kila kitu huku kupitia pendekezo la Ukanda Mmoja,Njia moja wanaangalia katika kukuza Teknolojia.

    Anavitaja baadhi ya vyuo vilivyochaguliwa katika program hiyo kutoka nchi za Afrika kuwa ni Kikuu cha Egerton na chuo kikuu cha Moi kutoka nchini Kenya,,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania ,Chuo Kikuu cha Zambia,Chuo Kikuu cha Makelele nchini Uganda,Chuo Kikuu cha Lagos,nchini Nigeria na vinginevyo.

    Vyuo hivyo 20 kutoka China vinakuwa na ushirikiano na vingine 20 katika masuala mbalimbali kama kubadilishana wanafunzi kusomea masuala kadhaa,kufanya tafiti mbalimbali, tamaduni na ufadhili kwa wanafunzi.

    "Pia tunashirikiana na kampuni katika maeneo wanayozalisha kwa kutoa mafunzo kwa wananchi kwa kuwapatia walimu na mitaala kwa program hizo huku wakiwaalika wanafunzi kujifunza nchini China" anasema.

    Anasema wana taasisi ya mafunzo ya elimu ya ufundi Luban ikiwa na lengo la kushirikiana na vyuo vya ufundi Africa kutoa mafunzo kama ya Uselemala au kazi za ufundi.

    Anasema katika Taasisi ya Confucius mpaka sasa Afrika wametoa mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya 460,000 huku wakisaidia mafunzo ya ufundi katika nchi mbalimbali za Afrika.

    "Ushirikiano katika mafunzo ya ufundi ni mkubwa kutokana na upungufu wa wataalam katika taaluma hii"anasema Xu Tao.

    Meneja Mkuu wa Kampuni China Educational Instrument and Equipment Corp (CEIEC) Huang Gang anasema taasisi hiyo imesaini makubaliano ya ushirikiano na taasisi mbalimbali 21 kutoka katika nchi za Afrika. Anasema wametoa vifaa mbalimbali ya elimu 900 katika nchi 15 za Afrika

    Huku Profesa kutoka Taasisi ya kutoa mafunzo ya kiafrika katika ChuoKikuu cha Zhejiang, Chen Mingku anaeleza kuwa chuo hicho kimekuwa kikishirikiana ya nchi za Afrika kwa zaidi ya miaka 50 sasa katika sekta ya elimu na idadi ya wanafunzi wa kiafrika wamekuwa wakiongezeka kila mwaka.

    Anasema kabla ya mwaka 2010 walidahili wanafunzi chini ya 100 lakini kufikia mwaka 2015 zaidi ya wanafunzi 500 kutoka nchi za Afrika walichaguliwa kusoma nchini China.

    Mkurugenzi wa Idara ya mafunzo ya Ufundi na Elimu ya watu wazima katika wizara ya Elimu China, Liu Hongjie anasema kuna vyuo 12,000 vya mafunzo ya ufundi vyenye wanafunzi milioni 30 na wamekuwa na ushirikiano na Africa kwa kujenga shule hizo au kubadilishana wanafunzi kupata mafunzo China.

    Anasema kwa sasa wameishajenga chuo cha ufundi nchini Ethiopia. Anasema pia kampuni za China zilizowekeza maeneo mbalimbali ya nchi za Afrika yanaajili wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao hawana uzoefu na kazi hizo na kulazimika kutoa mafunzo ka manufaa ya kampuni na wananchi

    Hongje anaeleza kuwa mikakati yao ni kupeleka elimu hiyo kwa wananchi wa Afrika hasa wale walioko mitaani ili kuboresha maisha na teknolojia na kwa mwaka jana walitoa udhamini kwa wanafunzi 10,000 wengi wakilipiwa na serikali za mitaa za China.

    Anasema kwa mwaka ujao wanatarajia kutoa udhamini katika mafunzo ya ufundi kwa wanafunzi 20,000 toka Afrika na hakuna maeneo maalum inatarajia serikali ya nchi husika inahitaji wataalamu gani.

    Naye Profesa Chen Mingkun kutoka Taasisi ya Masomo ya Kiafrika katika chuo kikuu cha Zhejiang Normal anasema wamekuwa na programu ya kubadilishana wanafunzi na wakufunzi kwenda kutoa mafunzo katika nchi za Afrika.

    Anasema kwa mwaka 2016 wanafunzi 41 kutoka nchini Afrika Kusini na wengine 142 wakienda Tanzania kwa lengo la kutoa mafunzo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wa vyuo rafiki katika program ya 20+20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako